Polisi watukutu wa nchini Saudi Arabia wanatarajia kupata utaalam wa masuala ya uchawi kama ule alionao Profesa Albus Dumbledore, ambaye ni mkuu wa shule ya Hogwarts. Wajumbe thelathini wa Tume ya Kusimamia Maadili na Kukabiliana na Maovu wamehitimu mafunzo ya siku tano ambayo yanatarajiwa kuwawezesha kukabiliana na uchawi, kuwatambua walozi na hata kuvunja laana zao.
Bila hata kusemwa, kujihusisha na uchawi ni jambo linalopingwa vikali kwenye Falme za Wahafidhina halisi, ambapo yeyote atakayekutwa na hatia ya kujihusisha na uganga na ulozi ananyongwa.
Kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu,UAE, mchambuzi Sultan Al Qassemi anasema:
Mafunzo muhimu kwa karne ya 21 — Polisi wa kidini wa Saudia wapata mafunzo ya kukabiliana na uchawi| Emirates 24|7 https://t.co/A06wNxej0q
— سلطان سعود القاسمي (@SultanAlQassemi) Februari 18, 2016
Wengine waliliangalia jambo hili kwa kufananisha na yale yaliyokwishafanywa na wengine na kujaribu kuwaiga, mfano ukichukuliwa kutoka kwa J K Rowling's mwandishi mashuhuri wa makala za riwaya ya Harry Potter.
Nadim Rifai alimtwiti mwandishi wa riwaya moja kwa moja kwa kusema:
@jk_rowling Harry Potter na Ufalme Uliojificha. Tafadhali hakikisha hili linatokea. Mimi 'll nitachukua hapo asilimia 1 tu https://t.co/aHnXeLxOg7
— Nadim Rifai (@NadimRifai) Februari 19, 2016
Pia, Hassan Cha anasema kuwa kuwapatia mafunzo haya polisi wa kidini ni “toleo la Harry Potter lililosanifiwa”:
Polisi wa kidini wa Saudia wapata mafunzo ya kukabiliana na uchawi https://t.co/RaLaU06Hka toleo la Harry Potter lililosanifiwa's ulinzi dhidi ya msmbo ya ulimwengu wa giza.
— Hassan Cha. (@c_ha93) Februari 8, 2016
Ukiweka pembeni Harry Potter, inaonekana kuwa programu kama hizi zilishaanza kitambo. Mtumiaji mmoja wa Facebook alichapisha makala iliyoandikwa mwaka 2013 iliyokuwa inazungumzia mafunzo yanayofanana na haya. Kiuhaliasia, kupambana na ulozi ni moja ya maeneo muhimu matano ambayo polisi wa kidini wanapaswa kuyashughulikia wawapo kwenye majukumu yao. Mambo mengine manne ni: “kuulinda Uislam, kuzuia kushurutisha mtu kutoa taarifa zake, kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna yeyote anayekaidi kuwatii watawala.”