Watu Watano wa Yemeni waliokuwa wametiwa hatiani kwa mauaji na ujambazi walinyongwa kwa kukatwa vichwa vyao nchini Saudia Arabia na miili yao kutundikwa hadharani katika mji wa Jizan ulio kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Kunyongwa kwa watu hao, waliosemekana kuwa sehemu ya genge la majambazi, limefanya idadi ya watu walionyongwa nchini humu mwaka huu kufikia 47. Mauaji, ujambazi wa kutumia silaha, usafirishaji wa madawa ya kulevya, ubakaji, na kufuru za kidini ni makosa yanayoongoza chini ya sharia ya dini inayotumika katika nchi hiyo ya Kiislamu.
Nchi ya Yemen pia inayo hukumu ya kifo na inashikilia nafasi ya sita duniani kwa idadi ya hukumu hizo, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International. Saudi Arabia iko kwenye nafasi ya nne, nyuma ya China, Iran na Iraq. Marekani ni ya tano.
Picha za miili ya watu watano ikining'inia kwenye kamba juu ikiwa imefungwa kwenye winchi zilisambazwa kwenye mitandao ya twitter na facebook tarehe 21, 2013 zikiwasikitisha watumiaji wengi, ikiwa ni pamoja na raia wa Yemeni walioogopeshwa na kukerwa na picha za miili ya raia wenzao.
Kwenye mtandao wa Twita, profesa na mhariri nchini Saudi Arabia, Bayan (@BintBattuta87) aliandika kwa mshangao:
@BintBattuta87: INATISHA: Picha za watu watano walionyongwa leo, miili yao ikiwa imening'inizwa sasahivi kwenye mitaa ya #Saudi. Upuuzi uliopitiliza, wallah. pic.twitter.com/LwztwvfpAB
Akaongeza:
@BintBattuta87: INATISHA: #KSA: Watu wamekaa wakikodolea macho miili ya marehemu hao. Hakuna mtu anasimama kulaani vitendo hivi?! Hicho ndicho kinachoniua mimi: pic.twitter.com/za72LMdNDQ
Haykal Bafana (@Bafana3), mwanasheria wa ki-Yemeni aishie Yemen, alitwiti picha ya tukio hilo na akawa na maoni haya:
@Bafana3: Hivi ndivyo Saudi Arabia inavyowanyonga majambazi. Wanaume watano wa ki-Yemeni wamenyongwa jana. #KSA https://www.facebook.com/haykal.bafana/posts/469019226511426 … pic.twitter.com/0NcWDxYBHc
Sana2 Al-Yemen (@Sanasiino), mwandishi wa habari wa Yemeni anayeishi Uingereza, alitanabaisha:
@Sanasiino: Saudi imewanyonga wa-Yemeni watano huko Jizan; na kuwaning'iniza ili dunia yote iwaone. Hawa ndio watu wanaotawala katika Nchi Takatifu pic.twitter.com/JP6QpnzXsE
Mwandishi na mhariri wa zamani wa Mashariki ya Kati kwa Jarida la The Guardian Brian Whitaker (@Brian_Whit) alitwiti kiungo cha makala aliyokuwa ametoka kuiandika:
@Brian_Whit: Unyongaji Uliokubuhu Saudi Arabia. Miili isiyo na vichwa yaanikwa hadharani http://bit.ly/YYULRz (http://al-bab.com)
Katika makala hiyo, mwandishi alionyesha namna mtandao wa intaneti unavyoathiri taswira ya Saudi Arabia duniani kote:
Wazo nyuma ya unyongaji wa hadharani jinsi hii ni kuwafanya wengine waogope kufanya vitendo hivyo hivyo, ingawa haijulikani kama ni kweli watu wanaogopa kufanya uovu kwa kutazama miili ya wenzao. Lakini siku hizi, kwa sababu ya mtandao wa intaneti, si raia wa nchi hiyo tu wanaoona picha za miili hiyo na hiyo inaongeza nguvu madai ya jumuiya za kimataifa kwamba nchi hiyo ya Kifalme ni ya kikatili.
Akiinukuu Amnesty International, shirika la kutetea haki za binadamu anaongeza:
. Amnesty International linasema:
“Mamlaka za Saudi Arabia mara kwa mara zimekiuka viwango vya kimataifa vinavyoongoza mashitaka ya haki na kuhakikisha usalama wa watuhumiwa, ambao mara nyingi wananyimwa haki ya kuwakilishwa na wanasheria wala haki ya kujulishwa mwenendo wa mashitaka yanayowakabili.
“Wanaweza kuhukumiwa kwa kutumia ushahidi wa “kukiri” unaopatikana kwa kuwatesa au vitendo vingine vya kinyama.”
Mwanablogu wa Yemeni Afrah Nasser (@Afrahnasser), ambaye anaishi Sweden, aliitaka Yemen ilaani unyongaji wa kikatili uliofanywa kwa raia wake:
@Afrahnasser: Ninamwomba Mhe. Hadi au yeyote kutoka kwenye wizara ya ushirikiano wa kimataifa ya #Yemen kutoa tamko la kulaani kunyongwa kwa watu watano wa ki-Yemeni kitendo kilichotekelezwa na #Saudi!. http://afrahnasser.blogspot.com/2013/05/saudi-excutes-five-yemeni-men.html?
1 maoni