Habari kuhusu Qatar

Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala

  8 Oktoba 2012

Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.

Twita Kutoka Beirut: Siku ya Pili ya Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni

  12 Disemba 2009

Siku ya pili ya Warsha ya Wanablogu wa Kiarabu ilianza na mada inayohusu Mtandao wa Herdict, tovuti inayotumia vyanzo vya watumiaji kukusanya taarifa za uchujaji wa habari kwenye intaneti kutoka kwa watumiaji duniani kote. Mshiriki wa warsha kutoka Qatar Muhammad Basheer alituma picha kutoka kwenye mada hiyo katika ujumbe wa...

Palestina: Maoni Juu ya Kuzinduliwa Kwa Huduma ya Google.ps

  16 Agosti 2009

Google imeongeza anwani ya google.ps (google palestina) kwenye orodha yake zana inayotoa huduma za utafutaji zinazolenga sehemu mbali mbali. Anwani hiyo mpya inakusudiwa kufanya kazi katika ukanda wea Magharibi na Gaza, ambako watoaji huduma za intaneti hufanyia kazi zao.