Mambo Si Kama Yanavyoonekana Kuwa: Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices

Kipindi cha Yaliyojiri Wiki hii kinaangazia baadhi ya habari kubwa zilizojitokeza zaidi hapa Global Voices. Tunakuletea watu, maeneo mapya na matukio kutoka duniani kote ambayo hayapewi uzito wowote unaostahili.

Juma hili, tnasikiliza masimulizi kutoka Paraguay, Iran, Qatar na Caribiani yatakayojadili mitazamo inayoaminiwa na wengi.

Shukrani nyingi kwa mwigizaji wa ki-Trinidadi Michael Cherrie, mwanafunzi wa muziki wa Chuo Kikuu cha Trinidad na Tobago Janelle Xavier na wanafunzi wa uigizaji Tenisha Richards-Weekes na Karian Forde kwa kuratibu na kuweka sauti kwenye kipande cha #LifeInLeggings. Tunamshukuru mwandishi wetu wa Global Voices Andrea Arzaba kwa kutusaidia muziki.

Na hali kadhalika, shukrani nyingi kwa mhariri wa Global Voices wa Iran, Mahsa Alimardani, mhariri wa Global Voices Caribiani Janine Mendes Franco, na waandishi wetu wote, watafsiri na wahariri waliotusaidia kufanikisha kipindi hiki.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa Jahzaar; Co-Creators (Instrumental) wa Nick Jaina; Westside Chillers wa Little Glass MenBind thy wings wa krackatoa; Tiptoe (Instrumental) wa YEYEY; na The Bears just for show wa krackatoa.

Picha iliyotumika kwenye makala hii imepigwa na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Wendy, CC BY-NC 2.0.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.