Habari Kuu kuhusu Paraguai
Habari kuhusu Paraguai
Mambo Si Kama Yanavyoonekana Kuwa: Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices
Wiki hii, tunakuchukua kwenda Paraguay, Iran, Qatar na eneo la Caribiani.
Mjamzito wa Miaka 11 Agoma Kutoa Mimba Nchini Uruguay
Niña de 11 años embarazada que no quiere abortar genera polémica➝http://t.co/uPBo6NEKcC #Aborto #Embarazo #Uruguay — Periódico La Tribuna (@PLaTribunaFunza) May 8, 2015 Kugoma kwa mjamzito wa miaka 11 kutoa mimba kumesababisha utata. Hivi karibuniTuliandika kuhusu msichana wa miaka 10 aliyekuwa mjamzito nchini Paraguay kwa kudaiwa kubakwa na baba yake wa...
Wikipedia kwa Lugha ya Ki-Guarani
Mwaka huu, Wikipedia katika lugha ya Kihispaniola ilifikia makala milioni moja na kutolewa kwa mwongozo msingi wa mtumiaji katika lugha ya ki-Guarani. Wazo ni kufufua jamii ya wanaozungumza kiguarani katika jukwaa hili kubwa. Hadi sasa kuna makala 20 tu katika lugha hiyo. […] Kama una nia ya kushirikiana na mradi...
Paraguai: Rais Lugo Akiri Kuzaa Mtoto Wakati Bado Akiwa Askofu
Hivi karibuni Rais wa Paraguai Fernando Lugo alikiri kuwa alizaa mtoto wakati alipokuwa askofu wa kanisa la Katoliki la Roma. Habari hii imesababisha utata kati ya wanasiasa, vyombo vya habari, na wanablogu ambao wanaandika kuhusu kusikitishwa kwao na kiongozi huyo, na kadhalika jinsi ambavyo kuna matatizo mengine makubwa zaidi yanayotisha ambayo yanapaswa kutiliwa mkazo ikilinganishwa na vitendo vinavyofanywa na wanasiasa wengine.
Paraguai: Wahamiaji Wasimulia Visa Vyao
Ni jambo la kawaida katika Marekani ya Latini kwa wahamiaji kuondoka na kwenda kwenye malisho ya kijani zaidi kwenye nchi jirani au nchi za mbali. Hakuna tofauti kwa Waparaguai, ambao huwaacha nyuma marafiki zao na familia ili kufuata fursa nyingine. Simulizi kadhaa za namna hiyo zinasimuliwa kwenye blogu inayoitwa Paraguayos (sisi ni Waparaguai), ambayo inawaalika wahamiaji walioko duniani kote kuwasilisha simulizi zinazohusu uzoefu wao.
Paraguai: Rais Lugo Kutopokea Mshahara
Utawala wa Rais Ferdinand Lugo umeanza na tangazo kuwa hatapokea mshahara wake wa mwezi. "Sihitaji mshahara huo, ambao unapaswa kumilikiwa na masikini," alisema Lugo. Mabloga nchini humo wanatofautiana mitazamo, wakati mmoja anausifu uamuzi huo, mwingine anajiuliza ni vipi Rais lugo atajilipia gharama binafsi za maisha.
Paraguai: Kuapishwa Kwa Lugo Kwenye Flickr
Rais wa paraguai alianza kutumia Flickr mnamo januari 2008 kama njia ya kuorodhesha nyendo zake wakati wa kampeni. Baada ya kuapishwa kama rais wa nchi siku ya tarehe 15 Agosti, anaendelea kutumia chombo hiki cha uandishi wa kijamii. Karibia picha 2,500 baadaye na zote chini ya haki miliki huria, Lugo anategemea kuwajumuisha WaParaguai nyumbani na ughaibuni katika urais wake.