Habari kuhusu Uruguai

Watu wa Uruguay Waomboleza Kifo cha Mwanamuziki José Carbajal, ‘El Sabalero’

  11 Novemba 2010

Mwimbaji na mtunzi José Carbajal, anayejulikana kwa jina la utani kama “el Sabalero,” amefariki kutokana na shambulio la moyo mnamo Oktoba 21 akiwa na umri wa miaka 66. Carbajal anachukuliwa kuwa gwiji na utambulisho wa utamaduni wa Uruguay. Mwaka huu alikuwa akifanya kazi na wasanii wengine katika mradi wa Kompyuta Moja ya Mapajani kwa Kila Mtoto nchini Uruguay Uruguay, Mpango wa Ceibal, ili kutumbuiza kwenye maonyesho kwa ajili ya watoto wa shule nchini kote.