Mfungwa wa Zamani wa Guantanamo Ahatarisha Maisha Yake Kwa Kugoma Kula Akishinikiza Kuunganishwa na Familia Yake

jihad02

Jihad Diyab wakati wa mahojiano huko Montevideo. YouTube

Jihad Diyab atahitaji magongo ya kutembelea kwa maisha yake yote yakiwa ni kitu cha kumkumbusha mateso aliyoyavumilia kwa miaka 12, miezi 8 na siku 7 kama mfungwa katika gereza la Guantanamo Bay, mahali ambapo jeshi la Marekani lilikuwa likiendesha gereza likiweka washukiwa wa makosa ya kivita kwa muda usiofahamika na bila kufunguliwa mashtaka.

Akiwa na miaka arobaini na tatu leo, Diyab amepatwa na madhara ya kudumu katika mgongo wake akiwa chini ya uangalizi wa serikali ya Marekani. Katika mahojiano yaliyafanyika mapema mwaka huu huko Uruguai, alimwambia an mwandishi wa Ki-Agentina  kuwa jinamizi la Guantanamo bado linawawinda hata wafungwa waliokuwa na bahati ya kuondoka mahali hapo. Anasema kuwa “wote waliofanikiwa kutoka humo bado ni wafungwa wa Marekani kwa ndani”

Diyab ni kati ya wafungwa sita kutoka Guantanamo ( Wasyria wanne, Mpalestina mmoja na Mtunisia mmoja) ambao waliachiliwa huru na  kukaribishwa nchini Uruguai hapo Disemba 2014,shukrani kwa serikali iliyofanya makubaliano kati ya Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Uruguai José “Pepe” Mujica.

Kufuatia kushindwa kwa jitihada za kuungana na familia yake, iliyokimbia kutoka Syria kwenda Uturuki, Diyab alitangaza mgomo wa kula katikati mwa mwezi Agosti. Mwezi wa tisa tarehe 15, aliliambia told shirika la habari la BBC kuwa anailaumu serikali ya Uruguai na serikali ya Marekani kwa hali aliyo nayo kwa sasa.

Mi situación de salud está muy precaria, estoy mal, mi energía está muy baja y yo responsabilizo personalmente al gobierno de EE.UU. y también al de Uruguay si yo muero.

Hali ya afya yangu kwa sasa ni mbaya sana. Ninaumwa,nguvu zangu ni kidogo sana na kama nitakufa basi mimi binafsi nitazilaumu serikali za Marekani na Uruguai.

Mwishoni mwa Septemba, baada ya kupokea uhakika wa kuwa familia yake iko salama huko Uturuki, alianza tena kula vyakula vya majimaji .

Diyab alitengeneza vichwa vya habari mwezi Juni, alipokimbia Uruguai kupitia mpaka wa Brazili. Vyombo vya habari vya Uruguai vilimuita “muasi asiye na shukrani” kwa kuikimbia nchi iliyompokea kutoka utumwa wa Marekani. Baada ya mwezi usio na matumaini kuhusu mwenendo wake, Diyab aliibukia katika mji wa Caracas nchini Venezuela, ambapo alikamatwa na kuswekwa ndani na hatimaye kusafirishwa tena kwenda Montevideo.

Suala la kusafirishwa kwa Diyab limebaki kuwa kitendawili.Ingawa maofisa wameendelea kusema kuwa waliokuwa wafungwa wa Guantanamo ni “watu huru” ila katika uhalisia hicho kimekuwa ni kitu tofauti kabisa.

Kulingana na gazeti la Brecha,Uruguai inaonekana kukubali kuwachukua wafungwa walioachiliwa huru na kuwaweka nchini kwa miaka miwili kabla ya kutoa mguu nje ya nchi hiyo, ingawa maafisa wa serikali ya Uruguai wanakataa kuwa waliafikiana na taratibu hizo.  

Mpango wowote ambao Uruguai imefanya na Washington, ukweli unabakia kuwa wafungwa walioachiliwa kutoka Guantanamo wametengenezewa kadi za uraia wa Uruguai pekee ambazo hazitafaa kusafiria katika nchi za kigeni.

Leo, mtazamo wa jamii kuhusu wafungwa wa zamani wa Guantanamo umebadilika na hata raisi wa zamani wa Uruguai aliyejadili kuhusu uhuru wa wafungwa hao kwa sasa anasema kuwa, kuwapokea hao watu ilikuwa ndio gharama nchi yake ilipaswa kulipa ili iweze kuendelea “kuuza machungwa nchini Marekani” na kuimarisha mahusiano mema.

Maandamano ya Wafungwa

Four of the Six of Guantanamo protest in front of the US Embassy, in Uruguay | Photo: Reproduction/YouTube

Wafungwa wanne kati ya “sita wa Guantanamo” wakiandamana mbele ya ofisi za ubalozi wa Marekani nchini Uruguai.YouTube

Miezi mitano baada ya kuwasili nchini Uruguai wafungwa wanne kati ya “sita kutoka Guantanamo” walifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Montevideo. Diyab hakuwepo. Wanaume hao walijikusanya mahali hapo baada ya kugundua kuwa Marekani imekataa kuwapa msaada wa fedha.

Wakiandika katika blogu,wanaume hao wanasema kuwa wametelekezwa katika nchi ya kigeni bila ajira, bila familia zao au uelewa wa lugha ya asili ya mahali hapo. Kwa hili, na kwa miaka 13 waliyotumikia wakiwa wamefungwa bila mashtaka, wanastahili msaada kutoka kwa serikali inayowajibika, waliyasema hayo hapo April:

They [the U.S.] Wanatakiwa watupe namna ya kuishi kama binadamu wengine. Hawawezi kurusha makosa kwa watu wengine, wangetusaidia nyumba na misaada ya kifedha. Hatuombi yasiyowezekana kutoka kwao, walitufunga kwa miaka 13 hivyo wangepaswa kutusaidia kwa miaka kadhaa ijayo. Tunafikiri kuwa hiki ni kitu kidogo tu wanachoweza kufanya au tunachowaomba.

Katika makala kuhusu maisha ya Jihad Diyab huko Uruguai, jarida la Anfibia linasema kuwa mpango uliosababisha kufunguliwa kwake ulikuwa ni makubaliano “yasiyo rasmi” na Marekani. Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna nyaraka rasmi zinazothibitisha haki za wafungwa hao wa zamani. Nyaraka pekee ambazo ni rasmi ni barua iliyosainiwa na Katibu wa Ikulu ya Marekani John Kerry inayoorodhesha majina ya wafungwa hao sita ikisema “hakuna taarifa zinazoonesha kuwa [wafungwa hao] walijihusisha au kutekeleza vitendo vya kigaidi kwa Marekani au washirika wake.”

Jarida hilo la Anfibia pia lilichunguza maisha ya waliokuwa wafungwa wa Guantanamo ambao wengine wanaishi Ulaya na Afrika na kugundua kuwa wengi wanakutana na changamoto zinazofanana. Mmoja kati ya wanaume hao, kwa sasa anaishi nchini Slovakia aliliambia jarida kuwa “Huu sio uhuru. Bado tumefungwa. Nimeondoka Guantanamo lakini bado iko ndani yangu wakati wote.” Mfungwa mwingine ndani ya sinema aliyaita maisha yake baada ya kutoka gerezani “Guantanamo ya pili”

Tangu Aprili, wafungwa hao wote wa zamani walioko Uruguai isipokuwa Diyab walisaini mpango wa Huduma ya Kiekumeni kwa Utu (SEDHU huko Hispania)wa kuwapa msaada wa kifedha. Diyab alikataa kusaini, akisema kuwa hakubaliani na masharti ambayo yanajumuisha nyumba naxa
fedha kwa kipindi cha miaka miwili. Diyab anasema kuwa majeraha ya mgongo wake yanamzuia kufanya kazi na akaongeza kusema kuwa msaada huo wa fedha hautoshelezi kuendesha maisha yake achilia mbali familia.

Diyab ndie mfungwa pekee kati ya sita walioingia Guantanamo akiwa na mke na watoto wake. Katika kundi lake, ndiye pekee anayesema anataka kuondoka nchini Uruguay kwenda katika nchi ya Kiarabu anakotegemea kuishi na familia yake.

Kwa hiyo, Ni wapi sasa?

Changamoto inayomkabili Diyab kwa sasa ni kupata makazi mapya. Ndani ya mahojiano aliyoyafanya na jarida huru liitwalo La Diaria, Senator Lucía Topolansky aliyefungwa enzi za serikali ya kidikteta ya Uruguai aliahidi kuwa serikali inaendelea kutafuta suluhu:

Lo que hay que hacer es buscar un país que lo quiera. Y ese no es un problema de Uruguay ni tampoco de él, es un problema del mundo. 

Tunachotakiwa kufanya ni kutafuta nchi itakayo mkubali. Na hili sio tatizo la Uruguai au la kwake pekee, ni tatizo la dunia nzima.

Mwezi Septemba serikali ya Uruguai ilitoa tamko kuthibitisha kuwa inatafuta nchi ambayo iko tayari kumpokea Diyab na familia yake. Maofisa wa serikali walisema kuwa wanafanya kila wawezalo kumuomba Diyab kusitisha mgomo wa kula ili “kuheshimu kanuni ya uhai.”  

Hata hivyo majadiliano hayo yameonesha mafanikio kidogo. 

Kulingana na faili la Gitmo katika mtandao wa WikiLeaks, Diyab ni mwana wa baba wa ki-Syria na mama wa ki-Agentina aliyekuwa akijipatia kipato chake kwa kazi ya udereva wa malori kwa miaka mingi huko Syria. Alipokamatwa huko mjini Lahore na polisi wa Pakistani mwaka 2002, alikuwa akiishi katika nyumba iliyofanyiwa marekebisho na Taliban na alikuwa akiuza asali ili kujikimu yeye na familia yake.

Jalada lililomuhusisha Diyab na wafuasi wa al-Qaida, lilimtambulisha kama ” mtu hatari” “intelijensia ya hali ya juu” na “tishio kwa Marekani.” Alidaiwa kuhusika na kughushi nyaraka na hati za kusafiria kwa ajili ya jumuiya za kigaidi. Akiwa kizuizini mwa Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja, hakuwahi kufunguliwa mashtaka rasmi kwa kosa lolote. Diyab alikana mashtaka yote.

Watu wanao muunga mkono Diyab  style=”font-weight: 400;”>walitengeneza ukurasa wa Facebook  na wito wa Avaaz wakiitaka serikali kuchukua ” hatua za haraka kumuunganisha na familia yake, katika nchi itakayo kubali kuiunganisha familia hiyo.” Ni wakati wa kurudia kufanya kile alichokifanya miaka 13 akiwa gerezani, Diyab anasubiri. Ndani ya mahojiano na shirika la habari la CNN,alisema kuwa:

Yo no quería hacer esta huelga de hambre pero me cerraron las puertas y me dejaron sin solución y es el único camino que encontré.

Sikutaka kuingia katika mgomo wa kula, ila walinifungia milango yote na hawakuniachia ufumbuzi mwingine na hii ndio njia pekee niliyoipata.

Juma hili, baada ya siku 54 za kukataa kula, Diyab aligundulika kuwa na tatizo la “kupoteza fahamu juu juu.” Kulingana na gazeti la La Diaria, hapo nyuma alisaini nyaraka akikataa kuingiliwa kati na huduma za kitabibu “hata kama maisha yake yatakuwa hatarini” lakini baadaye alikubali kulishwa kwa njia ya mishipa. Daktari anayemuhudumia Diyab anasema kuwa hali yake ya sasa ni “mbaya” inayoweza kusababisha “kifo cha ghafla”. Pamoja na hali yake inayotetereka, msulihishi baina yake na serikali ya Uruguai ameiacha kesi yake.

Hata hivyo, mgomo wa kula utaendelea wakati Diyab anasubiria majibu ya ombi lake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.