Habari kuhusu Honduras
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Kiongozi wa Jamii za Wazawa Berta Cáceres Auawa nchini Honduras
Baada ya miaka kadhaa ya uanaharakati wa masuala ya mazingira na kuzitetea jamii za wazawa, mtetezi nguli wa haki za binadamu Berta Caceres ameuawa nchini Honduras hii leo.
Kwenye Jiji Lenye Machafuko Zaidi Duniani, Wasanii wa Uchoraji Kuta Watumia ‘Silaha zao’ Vizuri
San Pedro Sula, Honduras, limechorwa kuwa ni jiji ambalo limekuwa na machafuko kuliko jiji lingine lolote duniani kwa muda wa miaka minne mfululizo. Wasanii wa uchoraji kuta wanamategemeo ya kubadili hali hii kwa michoro ya picha za rangi za kupuliza pamoja na ubunifu wao.
Honduras Yazalisha Ajira kwa Kuhamasisha Shughuli za Jamii
Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandes amezindua mpango wa “Desarrollemos Honduras” (Tuiendeleze Honduras), na maofisa na jamii walishiriki katika tukio hilo. Hernandes alieleza kwamba kama nyumba imebomoka au sakafu yake...
Uhamaji wa Watoto Wachukuliwa kuwa ni Baa la Kibinadamu
Kutoka Mexico, Katia D'Artigues, ambaye ni mwandishi wa blogu ya Campos Elíseos (Champs Elysées), aandika kuhusiana na watoto kulazimika kuhama wao wenyewe [es], hali inayompelekea kuiita hali hii kuwa ni...
Honduras Yazindua Kamusi ya Mtandaoni ya Lugha za Asili
Kamusi ya lugha za asili nchini Honduras ilisambazwa mtandaoni hivi karibuni[es]. Gazeti la Honduras liitwalo Tiempo [es] linaeleza kuwa kamusi hii “imejumuisha maneno yanayofanana katika lugha ya Kihispaniola, chortí, garífuna,...
Honduras: Zelaya Akamatwa na Kuondolewa Madarakani
Nchini Honduras siku ilianza na habari zinazosema kwamba Rais Mel Zelaya amekamatwa akiwa nyumbani kwake na wanajeshi wenye silaha mnamo siku ya kupigwa kura tata ya maoni. Siku chache kabla, Zelaya alimuondoa madarakani mkuu wa majeshi. Maoni yanatofautiana kutokea yale yanayosema kwamba hali iliyopo ni sawa na mapinduzi ya kijeshi mpaka yale yanayosema kuwa hii ilikuwa ndio njia pekee ya kukomesha jitihada za Zelaya za kutaka kugombea urais kwa awamu nyingine tena.