Kutoka Mexico, Katia D'Artigues, ambaye ni mwandishi wa blogu ya Campos Elíseos (Champs Elysées), aandika kuhusiana na watoto kulazimika kuhama wao wenyewe [es], hali inayompelekea kuiita hali hii kuwa ni “baa la kibinadamu”:
Son niños que son orillados a cruzar la frontera solos. No lo hacen por aventura, sino porque muchas veces no les queda de otra, por pobreza; porque buscan reunirse con un familiar quizá su padre o su madre que ya está en Estados Unidos. Su número crece día con día. Ya se cuentan en miles y al menos un centenar son detenidos todos los días de acuerdo a cifras no oficiales.
Ni watoto wanaolazimika kusafiri hadi nchi nyingine peke yao. Hawafanyi hivyo kwa sababu za kitalii, sababu kubwa ni kuwa hawana namna nyingine, ni umasikini, ni kwa sababu wanajaribu kuwatafuta ndugu zao ili waungane nao tena, yawezekana ni baba au mama zao ambao tayari wameshafika Marekani. Idadi ya wahamiaji watoto inaongezeka siku hadi siku. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, maelfu ya watoto husafiri na idadi isiyopungua mia moja hukamatwa kila siku.
Anaongeza kuwa:
Cómo están estos niños? Independiente de su estatus y nacionalidad son niños y tienen derechos. […] Lo cierto es que ya se estipuló que se les asignará un abogado gratis para ver su proceso que, como es obvio, es único en cada caso. Ahora, son solo 100 abogados que comenzarán a trabajar en diciembre de este año o enero de 2015.
No van a alcanzar.
Vipi kuhusu hao watoto? bila kujali hali yao na uraia wao, bado ni watoto na wana haki. […] Imekwisha fahamika kuwa, watoto hawa, kila mmoja atapewa mwanasheria wake. Hadi sasa wameshapatikana wanasheria 100 tu ambao wataanza kazi mwezi Disemba mwaka huu au mwezi Januari, 2015.
Hawatatosha.