Habari kuhusu Chile

VIDEO: Kuelekea Mfumo wa Haki na Jumuishi Nchini Chile

  20 Februari 2014

Katika video hiyo hapo juu iliyowekwa na Mfuko wa Jamii Wazi , Giorgio Jackson, kiongozi wa zamani wa wanafunzi na mbunge mpya kabisa nchini Chile, anajadili mfumo wa elimu nchini mwake na maanaa hasa ya kuwa “jamii wazi”. Trine Petersen anaandika: Mfumo wa haki na jumuishi unaoifanya elimu ipatikane kwa...

Video: Tetemeko la Ardhi Chile Kwa Kupitia Macho ya Raia

  1 Machi 2010

Wakati siku inakaribia kuisha, video zaidi za tetemeko la ukubwa wa 8.8 ambalo liliikumba Chile majira ya saa 9.30 usiku zinajitokeza. Tetemeko hilo, ambalo halikuathiri maeneo ya bara pekee kwa njia ya kusogea sogea kwa ardhi, kadhalika lilisababisha mawimbi ya tsunami mabyo yalizua tahadhari katika eneo zima la Pasifiki huku mataifa mbalimbali yakijiandaa kwa mawimbi hayo pindi yatakapofika kwenye fukwe zao.

Amerika ya Kati: Kasi Kubwa ya Ueneaji wa Jangwa

  6 Novemba 2009

Ueneaji wa jangwa unasambaa kimyakimya lakini kwa kasi kubwa mahali pengi duniani na Amerika ya Kati haijaweza kukwepa hali hii iliyo na athari mbaya za kutisha. Wakati ambapo majangwa ni maumbo ya asili, ueneaji wa jangwa ni mchakato wa kuharibika kwa nyanda za ardhi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu unaofanywa na binadamu.