Chile: Mkutano wa McCain na Pinochet Mwaka 1985

Mwaka 1985, Mbunge wa bunge la Marekani aitwaye John Mccain alizuru nchini Chile na kukutana na mtawala wa kiimla Augusto Pinochet, akiwa na viongozi wengine wa serikali. Mkutano huo ambao haujawahi kuripotiwa hapo awali umewekwa wazi na mwandishi wa habari John Dinges, ambaye amechapisha habari hiyo kwenye blogu yake CIPHER [es], kadhalika katika blogu ya Huffington Post, ambako huwa anaandika masuala yanayomhusu John McCain “ambaye amekuwa akishutumu vikali dhana ya kuketi na watawala wa kiimla bila ya masharti yoyote, inaonekana kuwa alifanya hivyo na “Pinochet, mmoja wa watawala wakiukaji wa haki za binaadamu ambaye anashutumiwa kuua zaidi ya raia 3,000 na kuwasweka gerezani makumi ya maelfu wengine”

Bloga wa KiChile juan Guillermo Tedeja anaandika kuhusu baadhi ya yaliyojiri kwenye mkutano huo [es]:

Seneta aliketi kwa saa moja na nusu na ka-zimwi ketu, pia alikutana na Jenerali wa jeshi Merino, ambaye utesi wake tunaujua fika… Mkutano huo, ulioandaliwa na aliyekuwa balozi wakati huo Hernán Felipe Errázuriz, haukutokea kwenye vyombo vya habari na Seneta hakutoa maoni yoyote.

Dinges aliandika kuhusu baadhi ya mazingira ya mkutano huo katika blogu ya Kituo cha uandishi wa Habari na Upelelezi (CIPER kwa kifupi katika lugha ya KiHispania)

Wakati wa mkutano, majira ya alasiri mnamo Desemba 30, Idara ya Sheria ya Marekani ilikuwa ikiwasaka maswahiba watatu wa Pinochet – aliyekuwa mkuu wa DINA (Idara ya Taifa ya Upelelezi) Manuel Contreras na maafisa wengine wa DINA Pedro Espinoza pamoja na Armando Fernández Larios – kwa vitendo vya kigaidi walivyovifanya jijini Washington D.C. Kesi iliyoendeshwa huko Washington ilibaini kwamba watu hao walipaswa kushitakiwa kwa ajili ya mauaji ya aliyekuwa balozi wa Chile nchini Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Orlando Letelier na pia mauaji ya raia wa Marekani Ronny Moffit, ambaye alikuwapo na Letelier. Mlipuko wa bomu kwenye gari sehemu za Sheridan Cirlce katika mji mkuu wa Marekani ulielezewa wakati huo kama moja ya tendo la kuchefua zaidi katika ugaidi wa kimataifa ambalo limewahi kufanywa na taifa la nje katika ardhi ya Marekani.

Wakati wa mkutano wa McCain na Pinochet, makundi ya upinzani wa kidemokrasia nchini Chile yalikuwa yakitafuta kuungwa mkono na viongozi wa Kidemokrasia duniani katika juhudi zao za kumshinikiza Pinochet aruhusu kurejeshwa demokrasi na kusitisha utawala wa kiimla kwa njia za amani, utawala ambao tayari ulikuwa umeshadumu kwa miaka 12. Viongozi wengine wa Bunge la Marekani waliozuru Chile walitoa matamko rasmi ya wazi yaliyopinga utawala wa kimabavu na kuunga mkono kurejeshwa kwa demokrasi, na wakati mwingine viongozi hao wa Bunge walilengwa kwenye maandamo yalioandaliwa na mashabiki wenye ghasia wa Pinochet.

Bloga Mchile-Mmarekani Tomás Dinges ameweka viunganishi vya makala zilizoandikwa katika blogu yake ya Chile From Within, na “mtaalamu-mahiri pamoja na baba” kadhalika ameweka viunganishi vya ziada vinavyohusiana na habari hiyo, kikiwemo cha majibu kutoka kwenye Kampeni ya Bwana McCain ambayo imetokea kwenye blogu ya gazeti la Miami Herald, Naked Politics.

Mabloga wengi wa kutoka Marekani ya Kusini na Chile wanaichapa makala ya John Dinges, kama njia ya kusambaza habari hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.