Chile: Mchakato wa Ujenzi Mpya Baada ya Tetemeko la Ardhi

Akihimiza “Umoja wa kitaifa” katika viwanja vya wazi vya Concepcion mnamo tarehe 27 Machi, mwezi mmoja kamili baada ya nchi kupigwa na tetemeko baya kabisa, Rais Sebastián Piñera alitangaza Mpango uliobatizwa jina la “Hebu Turejee kwenye Kazi” (“Manos a la Obra”) [Es], ambalo ni vuguvugu lililoanzishwa na Serikali ya Chile ili kujenga mpya miundombinu ya nchi pamoja na majengo. Siku mbili baadaye, tarehe 29 Machi, Piñera pia alitangaza mpango wa kutoa ruzuku ya dola za Marekani 2,543 ili kuzisaidia familia zipatazo 195,950.

Video kutoka YouTube mtumiaji EVRDIPUTADO44, ilichukuliwa katika viwanja vya wazi vya Concepción mnamo tarehe 27 Machi, 2010.

Huko Concepcion, Rais alieleza kwamba hatua za muhimu zilikuwa zimekwishaanza kuchukuliwa ili kujenga upaya madaraja, barabara, bandari na viwanja vya ndege. Pia alitangaza kwamba vituo vya dharura vya afya vitasaidia kazi za mfumo mzima wa afya kuanzia mwezi Aprili, na kwamba feri na madaraja ya dharura kuvuka Mto Bio-Bio utasaidia katika usafirishaji wa mizigo mizito na vifaa kwenda San Pedro de la Paz na Talcahuano. Hatimaye, Rais alieleza kwamba kutakuwa na mfuko maalumu ambao utagawanya jumla ya peso bilioni 8 (sawa na dola za Marekani milioni 15,107,160) kwa kupitia vocha maalumu zitakazogawanywa kwa familia zipatazo 200,000 ili ziweze kununua vifaa vya ujenzi.

Julio Segovia, ambaye ni msomaji wa makala iliyochapishwa na gazeti la La Nación[es] na ambayo ndiyo ilibeba tangazo hilo la mfuko huo maalumu, alikosoa mfuko huo maalumu wa nyuma akisema:

¿8 mil millones de pesos que serán distribuido entre más de 200 mil familias? O sea, $40 mil por familia, ¿con eso van a reconstruir sus casas?. Parece que Piñera no está dando “el ancho ni el largo” como Presidente.

Je, peso bilioni 8 ndiyo zitakazogawanywa kwa zaidi ya familia 200,000? Kiasi hicho kina maanisha kila familia itapata peso 40,000 (sawa na wastani wa dola za Marekani 75.5). Na kwa kiasi hicho cha fedha familia hizo zinapaswa kujenga upya makazi yao? Yaelekea Piñera Rais ameanza “kushindwa kazi”.

Mtumiaji wa Twita Viviana Meneses (@vivipazz) alipokea [es] tangazo la Rais na kukubaliana na kauli iliyotolewa na Seneta Camilo Escalona wa kutoka Chama cha Kisoshalisti ambaye alipata kusema hapo kabla kwamba Rais hakuwa na mpango wowote wa maana wenye kuikwamua nchi kutoka katika tatizo hilo:

Me carga Escalona, pero sus dichos son ciertos. Piñera no cuenta con un plan de reconstrucción efectivo. Ideas sueltas no sirven.

Simpendi Escalona lakini kauli zake ni za kweli. Piñera hana mpango wenye ufanisi wa ujenzi mpya. Mawazo mepesi hayasaidii.

Hata hivyo, raia wengine wa Chile wanaunga mkono mwito wa serikali wa kushikamana na waliwatia changamoto viongozi wa upinzani nao kuunga mkono mtazamo huo. Kupitia Twita, Manuel Blanco (@manuelblancoc), alituma ujumbe ufuatao kwa Guido Girardi, ambaye ni kiongozi maarufu wa upinzani wa Chama cha Demokrasia:

@guidogirardi Ojalá que todos, al igual que Guido, “estén” con el Pdte. Piñera en el proceso de Reconstrucción, sin polítiquería pequeña

@guidogirardi Ninatumaini kila mmoja, kama Guido, “atakuwa pamoja” na Rais Piñera katika mchakato wa ujenzi mpya, na kuweka siasa nyepesi pembeni.
Wasichana wakicheza katika mediagua (nyumba za dharura) katika kambi ya watu waliokimbia kwao huko Lipimávida,Vichuquén, Mkoa wa Maule. Picha ilipigwa na Rodrigo Alvarez na kutumiwa chini ya leseni ya Creative Commons.

Wasichana wakicheza katika "mediagua" (nyumba za dharura) katika kambi ya watu waliokimbia kwao huko Lipimávida,Vichuquén, Mkoa wa Maule. Picha ilipigwa na Rodrigo Alvarez na kutumiwa chini ya leseni ya Creative Commons.

Mipango ya ujenzi mpya iliibua mijadala mingi nchini Chile hata kabla ya tangazo la Rais Piñera’s. Moja ya masuala yaliyojadiliwa katika vyemba vya vyombo vya habari vya kijamii ni suala la nani atafanya ujenzi huo mpya na je hao watakaopata kazi hizo (watu binafsi au makampuni) watateuliwa kwa mtindo gani.

Katika makala kwa ajili ya Revista La Página [es] iliyobeba kichwa cha habari “Ujenzi Mpya wa Chile: Kila Mmoja hakupoteza katika janga la Tetemeko la Ardhi [es],” mwanafunzi wa uandishi wa habari, Martina Orrego anatoa dukuduku lake kuhusu namna kandarasi zitakavyogawanywa katika tenda za umma:

Una cosa sí debería estar clara para todos: mucha gente perdió todo lo que tenía, incluso a seres queridos, pero sólo unos pocos comenzarán a ganar con este desastre.El negocio para quienes serán los encargados de poner a Chile de pie es enorme. Los 30 mil millones en contratos de reconstrucción (o tal vez calza mejor “construcción” sencillamente) es plata que a alguien se le debe pagar […] Pero vivimos en Chile, donde sólo algunos “califican” y tienen los “méritos” necesarios para ganarse este tipo de concursos públicos.

Jambo moja lieleweke kwa kila mmoja: watu wengi sana walipoteza karibu kila walichokuwa nacho, hata wapendwa wao, lakini ni wachache tu ndio watakaoanza kuvuna kutokana na janga hili. Ukubwa wa biashara ya wale watakaosimamia ujengaji mpya wa nchi ya Chile ni usiokadirika. Peso bilioni 30 (sawa na dola za Marekani 56,651,874) zitakazoingia kwenye kandarasi za ujenzi mpya (au labda “ujenzi” ni neno bora zaidi) ni kiasi cha fedha ambacho mtu/watu fulani lazima walipwe […] Lakini tunaishi nchini Chile, ambapo ni wachache tu “ndiyo wanaokidhi viwango” na wana “sifa” zinazostahili ili kushinda zabuni za namna hii zinazotangazwa hadharani.

Anakumbusha kuhusu kashfa mbalimbali za ufisadi nchini Chile ili kuwaonya raia wa Chile kuhusu yale yatakayotokea:

Pero hagamos algo de historia para entender lo que podría venir. Cuántos casos de irregularidades en la adjudicación de licitaciones hemos escuchado este último tiempo. Transantiago y sus deficiencias […] y como dejar pasar el escandaloso caso Mirage donde se compraron aviones por más de 100 millones de dólares, los que resultaron ser defectuosos y sólo habrían sido adquiridos debido a que altos mandos de la Fuerza Aérea, e incluso dos ministros de Defensa, fueron receptores de “comisiones”. Esto es el ejemplo de lo que NO queremos que pase, pero que podría pasar, cuando se habla de adquisición de implementación para una nación.

Hebu tujikumbushe historia ili kuelewa kile kitakachotokea mbele yetu. Tumesikia juu ya kesi nyingi za ufisadi katika kutoa tenda. Transantiago pamoja na upungufu wake […] na jinsi ya kupuuzia kesi yenye kashfa nyingi ya Mirage, ambapo ndege ambazo baadaye ziligunduliwa kuwa na hitilafu, zilinunuliwa kwa dola za Marekani milioni 100 na ambazo zilichukuliwa eti kwa sababu tu maafisa wa ngazi ya juu wa Kikosi cha Anga, na hata mawaziri wawili wa ulinzi walikuwa wamepokea “chochote”. Huu ni mfano wa kile ambacho HATUTAKI kitokee, lakini pamoja na hayo bado kinaweza kutokea pale tunapozungumzia manunuzi yanayofanywa kwa ajili ya taifa.

Jambo lingine lililoibuliwa na mipango ya ujenzi mpya ni ugawanyaji madaraka katika Taifa la Chile. Mwanablogu Pablo Monje katika makala iliyoitwa “Ujenzi Mpya wa Chile: Fursa ya Kugawanya Madaraka? [es]” anapendekeza kwamba ujenzi mpya wa Chile utakuwa mgumu sana katika mfumo wa sasa ambapo madaraka yapo mikononi mwa serikali kuu, na kwamba kwa kiasi fulani anadai mfumo huo unahusika na jinsi mambo yalivyokwenda polepole katika kushughulikia matukio ya janga hilo mikoani:

Aprender de este fracaso exige avanzar a un Estado que se conforme por comunidades, regionales y locales, autónomas en sus formas de gobierno con respecto al gobierno central. Solo así se podrá enfrentar una nueva emergencia y el actual proceso de reconstrucción, ya que las comunidades contarán recursos y competencias institucionales propias, pudiendo responder con mayor velocidad a este tipo de crisis.

Kujifunza kutokana na kushindwa huku kunahitaji maendeleo ya Dola linalokubali uwezo wa kujitawala wa jamii za watu – mikoa na vijijini – kwa kupitia serikali zao licha ya kuwepo kwa serikali kuu. Ni kwa njia hiyo tu kwamba tungeweza kukabili dharura mpya na mchakato wa ujenzi mpya unaoanza, kwa sababu jamii za watu zitakuwa na rasilimali zao wenyewe na utaalamu wa kitaasisi, ambao (pengine) ungeruhusu kushughulikia kwa kasi zaidi aina kama hizi za migogoro.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.