Tetemeko Kubwa Laitikisa Chile Kaskazini, Lafuatiwa na Tahadhari ya Tsunami

Tetemeko kubwa lenye vipimo vya tetemeko 8.2 limeikumba Chile kaskazini majira ya saa 2:46 usiku na kusababisha tsunami aliyosababisha wasiwasi nchini humo kama video ifuatayo inavyoonyesha:

https://www.youtube.com/watch?v=Wg6du5bhVqE&feature=youtu.be

Kiini cha tetemeko hilo kilikuwa takribani kilometa 89 kusini mashariki mwa Cuya, mbele kidogo ya pwani ya Tarapaca.

Ramani: Kiini cha tetemeko hilo la ukubwa wa 8.2 kaskazini mwa Chile

Serikali iliwaomba wananchi kuondoka eneo lote la pwani kufuatia mawimbi ya kwanza ya bahari yalifika eneo la Iquique.

Katika mkusanyiko huu wa habari katika tovuti ya Nacion.cl, kuna picha kadhaa za watu wakielekea kwenye maeneo ya vilima na madhara ya kiwango fulani yalisababishwa na tetemeko hilo. 

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twita walisambaza taarifa za muhimu, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Taifa ya Mambo ya Dharura (ONEMI):

Wakati wa tishio la Tsunami, endoka kwa mguu nenda kwenye eneo la karibu zaidi kukutania.

Usisahau mbwa wako, ni lazima waondoke kwa dharura pamoja nawe. Tafadhali chukua tahadahri ya #Tsunami #Terremoto [tetemeko] #Iquique #Arica

Wengine walitoa maoni yao kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali wakilinganisha na tetemeko kubwa lililowahi kutokea mwaka 2010:

Wamejifunza kwa makosa waliowahi kuyafanya: wametoa tahadhari ya kutokea tsunami, na kushauri watu kuondoka maeneo yenye hatari na tayari jeshi liko mtaani. Mwisho, wamejiandaa.

Habari zinazoendelea

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.