Amerika ya Kati: Kasi Kubwa ya Ueneaji wa Jangwa

Pengine maneno ueneaji jangwa yanaweza kusikika sawa na jangwa, lakini kuna tofauti kubwa ya msingi kati ya maneno hayo: wakati ambapo majangwa ni moja kati ya maumbo mazuri ya kipekee ya asili, ueneaji jangwa ni mchakato wa kuharibika ambako kanda za ardhi hupitia baada ya kuathiriwa vibaya na mabadiliko ya hali ya hewa, shughuli za binadamu na majanga ya asili mpaka hatimaye zinageuka na kuwa majangwa.

Picha na Macnolete na inatumika chini ya leseni ya Creative Commons.

Picha na Macnolete na inatumika chini ya leseni ya Creative Commons.

Ingawa athari ya mabadiliko ya hali ya hewa katika ueneaji jangwa bado haijaeleweka vema, yaani kwa mujibu wa GreenFacts, inafahamika kwamba viwango vya juu vya joto vinavyotokana na kuongezeka kwa viwango vya dioksidii ya kaboni kunaweza kuwa na athari mbaya kutokana na kuongezeka kwa upotevu wa maji kutoka ardhini na kupungua kwa viwango vya mvua katika maeneo yenye ukame. Wakati huohuo ueneaji jangwa nao huchangia katika mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuruhusu kaboni iliyohifadhiwa kwenye mimea ya maeneo yenye ukame na udongo kurushwa kwenye anga.

Ueneaji jangwa unazidi kuwa na athari mahali pote duniani. Kwa sasa hivi ueneaji huo unaathiri mavuno, unasababisha kupanda kwa bei za vyakula vilivyopo, na katika baadhi ya maeneo, hata wanyama wanakufa. Watu wanalazimika kuhamia maeneo mengine ya mbali na nyumbani kwao, kama anavyoeleza mwanablogu Miguel Angel Alvarado anayetokea El Salvador kuhusu mpango wa kuhamisha makazi ya rais kwa sababu ya ueneaji jangwa[es]:

El traslado de casa presidencial, del Barrio san Jacinto al local en donde estaba el Ministerio de Relaciones exteriores, según informes extrajudiciales, obedece a la prevención del ejecutivo ante un posible hundimiento del suelo generado por cárcavas en este sector.

Kwa mujibu wa nyaraka zisizo rasmi kisheria, kuhamishwa kwa makazi ya rais kutoka maeneo ya San Jacinto kwenda ilipokuwa Wizara ya Mambo ya Nje hapo awali, ilikuwa ni hatua ya kujihami iliyofanywa na mhimili wa dola ili kuepuka kutitia kwa ardhi kutokana na makorongo yaliyotokea pale.

Bara lililoathiriwa zaidi ni Afrika, na jambo hili linaweza kuonekana zaidi nchini Kenya, ambapo moja ya sekta zinazoweza kupata athari kubwa za ueneaji jangwa na ukame ni wasichana. Pale maji yaliyohifadhiwa kwenye matenki yalipokuwa yametumika yote katika Nyumba ya Watoto Yatima ya Dago Dala Hera huko Magharibi mwa Kenya, akina mama wanaojitolea na watoto wanalazimika kuteka maji yasiyo salama kutoka katika mto ulio karibu kwa ajili ya kupikia na kunywa. “Kwenda mtoni kuteka maji peke yao nyakati za jioni kunawaweka wasichana katika hatari ya kukumbana na wanaume wanaoweza kuwanyanyasa kingono,” alisema Edwin Odoyo, ambaye mama yake anayeitwa Pamela ndiye aliyeanzisha makazi hayo ya watoto yatima.

Ingawa ueneaji jangwa una athari kubwa zaidi barani Afrika, hali ya mazingira ya Amerika ya Kati nayo inapitia mabadiliko makubwa, kama ilivyojadiliwa siku za karibuni katika Mkutano wa Tisa wa Kongamano kuelekea Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kukabili Ueneaji Jangwa uliofanyika jijini Buenos Aires, Ajentina. Mtaalamu wa Kiitaliano, Massimo Candelori, aliyekuwa mwakilishi wa Mkataba wa Kukabili Uenejaji Jangwa, alisema katika mahojiano na Tierramerica kwamba hali ilivyo Amerika ya Kati inatisha kwa kuzingatia kwamba hakuna taarifa za kutosha kuhusu kiwango cha ueneaji jangwa katika eneo hilo. “Hatuna takwimu za sasa hivi. Moja ya lengo lililojadiliwa katika Mkutano wa Tisa lilikuwa ni kupata viashirio vinavyoturuhusu kuelewa vizuri zaidi hali halisi … takwimu tulizonazo mpaka sasa ni zile za miaka kumi iliyopita,” alisema Candelori.

Katika nchi za Amerika ya Kati ambapo kilimo na ufugaji ni moja ya sekta kuu za uchumi, ueneaji jangwa unaweza kuwa wa kimyakimya, lakini wenye madhara makubwa kama mnyama hatari mwindaji. Walau asilimia 25 ya sehemu ya eneo zima tayari imeharibiwa na wakati huohuo watu wanazidi kuwa na wasiwasi juu ya suala hili, kama inavyojionyesha katika blogu mbalimbali.

Eco Briefings [pt], blogu ya KiBrazili, inaonyesha kwamba WaBrazili waishio Kaskazini Mashariki mwa nchi wanashuhudia ueneaji wa kasi sana wa jangwa[pt]:

Mais um alerta está ligado. Temos pouco tempo para corrigir as coisas. (…)

No Brasil a desertificação tem avançado na caatinga, e zonas do polígono da seca no Nordeste e Norte de Minas Gerais, e também em Estados que antes não tinham áreas secas ou desertificadas como o Rio Grande do Sul. O Rio Amazonas viveu já uma grande seca a pouco tempo, grande com mortandade de peixes.

Kiitia hatari kingine kinanguruma. Tuna muda mfupi sana wa kurekebisha mambo (…)

Nchini Brazili, ueneaji jangwa umeongezeka sana katika Caatinga, katika ukanda wa maeneo kame Kaskazini Mashariki na Kaskazini mwa jimbo la Minas Gerais, na vilevile katika majimbo ambayo hayakukumbwa na ukame wala ueneaji jangwa hapo kabla kama vile Rio Grande do Sul. Mto Amazon umepitia ukame mkubwa kabisa katika kipindi kifupi kilichopita, jambo lililosababisha samaki kufa kwa idadi kubwa.

Ajentina nayo ina maeneo kadhaa yaliyoathiriwa. Katika mkoa wa Valles Aridos, Kaskazini Mashariki, ambapo shughuli kuu ya kiuchumi ni ufugaji kondoo, inakadiriwa kwamba katika miaka 100 iliyopita, walau watu 180,000 walilazimika kuhama. [es] (katika mfumo wa .pdf). Kusini mwa nchi ya Ajentina nako hakujapona na ueneaji jangwa. Mwanablogu Ailen Romero, anaandika maoni katika blogu inayoitwa Geoperspectivas [es] kwamba katika mkoa wa Patagonia, juhudi za serikali za kukabili ueneaji jangwa bado hazitoshi:

En la Patagonia, la amplitud del problema es de tal magnitud que ha comenzado a adquirir estado público. Pocos ignoran el tema, pero pocos tienen la posibilidad de actuar de alguna forma o con el conocimiento para hacerlo. El problema de la desertificación en el caso de la Patagonia supera a los planes que se han elaborado para combatirlo. Es por eso que no deben ahorrarse esfuerzos, ni limitar la imaginación de soluciones alternativas.”Si la geografía es la manifestación de la sociedad en el espacio físico, un espacio físico deteriorado refleja una sociedad deteriorada” afirman del Valle y Coronato(investigadores del Centro Nacional Patagónico)

Katika Patagonia, ukali wa tatizo ni mkubwa kiasi kwamba umma wote umetambua tatizo hilo. Ni watu wachache tu ndiyo wanaolipuuza na ni wachache tu walio na nafasi au maarifa ya kufanya juhudi kulikabili. Tatizo la ueneaji jangwa huko Patagonia unazidi mipango iliyokwishaainishwa kulikabili. Ndiyo sababu kila juhudi haina budi kufanywa, wala kusiwe na mipaka katika kufikiria ufumbuzi mwingine wowote. ‘Kama Jiografia ni kielelezo cha jamii katika nafasi halisia, kuharibika kwa nafasi halisia huko kunaakisi kuharibika kwa jamii, wanasema Valle na Coronato (watafiti kutoka katika Kituo cha Taifa cha Patagonia).

Huko Chile, ambapo takribani asilimia 62 ya eneo la taifa tayari imeathiriwa na ueneaji jangwa [es], mwanablogu Alfredo Erlwein alieleza wasiwasi kupitia katika blogu inayoitwa El Ciudadano [es](Raia) kuhusu jinsi gani watu wasiyo na maarifa ya kutosha kuhusu ueneaji jangwa.

Efectivamente la desertificación es el problema ambiental más grave de Chile y muy poco conocido. Existen grandes zonas, como en la costa de la octava región, donde la erosión severa supera el 50% de la superficie: esto es que literalmente más de la mitad de los suelos se ha perdido por completo. En esas zonas se encuentran cárcavas de más de 50 metros de profundidad. Una tasa normal de formación de suelo puede ser de 0.2 cm por año, lo que evidencia la gravedad del asunto.

Ueneaji jangwa kwa hakika ni tatizo kubwa kabisa lakini lisilofahamika miongoni mwa matatizo ya kimazingira nchini Chile. Kuna maeneo makubwa, kama vile pwani ya Nane ya Mkoa, ambapo mmomonyoko mkali wa udongo unazidi asilimia 50 ya ardhi: hii ina maana kwamba zaidi ya nusu ya ardhi imepotea, huo ndiyo ukweli. Katika maeneo hayo kuna makorongo yenye kina cha mpaka mita 50. Kiwango cha kawaida cha utengenezekaji ardhi ni kama sm 0.2 kwa mwaka, huo ndiyo uthibitisho wa ukali wa tatizo lililopo.

Kwa mujibu wa mtaalamu Mwitaliano Candelori, kutumia udongo katika soko la Kaboni kutasaidia kupambana na ueneaji jangwa; jambo hili pengine litaamuliwa katika Kongamano litakalofanyika jijini Copenhagen. Tayari kongamano hilo limeanza kuhesabiwa siku na ulimwengu unalisubiri kwa hamu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.