Wiki hili, tunakupeleka Azerbaijan, Chile, Ufilipino, Poland na China.
Kwanza, tunaelekea Poland ambako hedhi zimechukua sura ya kisiasa, kufuatia waziri mkuu mwanamke nchini humo kuunga mkono muswada unaopendekea kupigwa marufuku utoaji mimba. Muda mfupi baadae, a Tukio la Facebook liitwalo “Hedhi Nzito kwa Serikali” lilipata umaarufu kuwahamasisha wanawake kusimulia vipindi vyao vya hedhi kwenye ukurasa rasmi wa waziri mkuu. Mwandishi wetu Anna Gotowska alituandalia habari hiyo.
Kisha tunaelekea Chile, ambako mwandishi wetu Shirley Campbell aliripoti kwamba raia wa Chile wenye asili ya Afrika nchini humo wanapambana kutaka kumbuliwa kwenye sensa. Kisha tunakupeleka Nagorno Karabakh, eneo linalowaka moto kufuatia kulipuka kwa mapigano kati ya vikosi vya Azeri na vile vya ki-Armenia mnamo Aprili 2. Habari hii iliripotiwa na mwandishi wetu Winston Obertan.
Mhariri wetu wa Asia kusini mashariki Mong Palatino anatutambulisha kwa Gregoreo Y. Zara, injinia anayetoka Ufilipino. Zara alikuwa mbunifu wa kifaa kinachoitwa simuvideo kinachomwezesha mtumiaji kumwona anayeongea naye.
Tunamalizia kipindi chetu kwa mahojiano na Oiwan Lam, Mhariri wetu wa Asia Kaskazini Mashariki, kuhusu nyaraka za Panama. Nyaraka hizo zilivuja juma lililopita na hivyo kuweka wazi namna matajiri wa sehemu mbalimbali duniani wanavyotumia mbinu ya kukwepa kodi — wakati mwingine kinyume na sheria. Kuvuja wa nyaraka hizo kumekuwa kukigonga vichwa vya habari duniani — isipokuwa China — ambako wadukuzi wa mtandao wamekuwa wakifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha wa-China hawafahamu au wafahamu machceh kuhusiana na nyaraka hizo.
Katika kipindi hiki cha Yaliyojiri Wiki Hii Global Voices, tunasindikizwa na muziki wenye leseni ya Creative Commons unaopatikana bure mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa Jahzzar, Halbi Gijh wa Thiaz Itch, Cumbia Bichera wa El Remolón, Mario Bava Sleeps In a Little Later Than He Expected To wa Chris Zabriskie, Can I Talk To You wa Podington Bear, and Body Parts wa Gary Lucas.
Kipindi hiki kinaendeshwa na Mhariri wa Habari wa Global Voices Lauren Finch akisaidiana nami— Mhariri Mtendaji wa Global Voices. Unaweza kutusikia kwa mara nyingine katika kipindi cha majuma mawili.
Podcast: Play in new window | Download