Chaneli za vichekesho kwenye mtandao wa YouTube zinasherehekea msimu wa Krimas barani Amerika Kusini, na maudhui yake yanasema mengi kuhusu utamaduni wa nchi hizo.
Baadhi ya video zinakejeli matarajio makubwa ambayo wengi wanayo kwa sikukuu hizi —na namna matrajio hayo hayavyotofautiana mno na ukweli halisi. Nyingine zinaangazia namna familia na marafiki zinavyokutana na kusimuliana mambo.
Woki Toki ni chaneli maarufu ya vichekesho kutoka Chile. Video yao inajaribu kuonesha aina mbalimbali za zawadi ambazo watu huzipokea, na watu wanaozitengeneza. Kuna rafiki anayesema uongo kuhusu zawadi, rafiki anayeweza kuwa na hasira kali (akimpa barafu rafiki yake wa kike), na mwingine akimpa rafiki yake wa kike chuma, na mwingine akimpa mwanamke pete, kwa mshangao wake, mwanamke huo bado anamchukulia kama rafiki wa kawaida tu:
Wakati huo huo, pia kutoka Chile, Laf anataja mambo yanayotokea watu wanapotafuta zawadi za Krismas dakika za mwisho:
Kutoka Ajentina, Ceci Saia analinganisha ukweli na matarajio, na kubainisha umuhimu wa maandalizi ya sherehe, tofauti za kifamilia na kiangazi cha joto kali kinachoambatana na Krismas ya Ajentina:
Kaskazini mwa Colombia, chaneli hiyo ya ucheshi Humor Latino inafafanua habari za Krismas nchini Colombia, namna watu wanavyokutana, kusikiliza hadithi za ndugu wazee na kufuata mila za kidini kwa lengo la kupata zawadi:
Mwisho, kwenye cheneli ya ya Flama inayoendeshwa nchini Marekani, Joanna Hausman anataja sherehe tisa za ajabu za Kimagharibi zinazofanyika kwenye nchi nyingi za Amerika Kusini, na kuonesha tofauti kubwa ya rangi na upekee wa sherehe hizo kwenye bara la Amerika Kusini: