[Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa zilizo kwenye lugha ya Kihispania.]
Maandamano ya kwanza kudai elimu wakati wa utawala wa sasa wa Rais Michelle Bachelet yalifanyika Mei, 8, 2014, yakiwa na ruhusa.
Maandamano yalihudhuriwa na makundi kadhaa. Kuyataja kwa uchache ni pamoja na Shirikisho la Wanafunzi la Chile (Confech), Mkutano wa Taifa wa Wanafunzi wa Sekondari (ACES), Mratibu wa Taifa wa Wanafunzi wa Sekondari (Cones), Vuguvugu la Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Mesup), Muungano wa Mashirikisho ya Sekta Binfafsi ya Elimu ya Juu (Ofesup) na Chama cha Maafisa wa Wizara ya Elimu (Andime).
Maandamano yalidai elimu inayotolewa kwa usawa na bure pamoja na ushirikishwaji wa moja kwa moja kwenye mageuzi ya elimu yanayoendelea hivi sasa. Gazeti la La Tercera liliandika:
Marcha estudiantil: ¿Qué está en juego? Pdta de la Feuc dice que estudiantes quieren “participación en la reforma” http://t.co/kkESMigWrC
— La Tercera (@latercera) May 8, 2014
Maandamano ya wanafunzi, nini hakiendi sawa sawa hapa? Rais wa Feuc anasema wanafunzi wanadai “kushirikishwa kwenye mageuzi”..
Maandamano yalifanyika wakati huo huo kwenye mji mkuu wa Santiago sambamba na maeneo mengine ya nchi hiyo. Ushiriki na uwepo wa idadi nzuri ya wanafunzi ulikuwa bayana:
Qué bueno ver que la marcha estudiantil fue masiva en #Santiago y regiones. Todos por una nueva educación, que construya un mejor #Chile
— René Naranjo S. (@renenaranjo) May 8, 2014
Inapendeza kuona kuwa maandamano ya wanafunzi yalikuwa makubwa jijini Santiago na kwenye maeneo mengine. Tumeungana pamoja kwa ajili ya elimu pya itakayoijenga Chile mpya.
Miles de jóvenes participan en la primera marcha estudiantil del año en #Concepción http://t.co/Tu0LiT2jIT vía @biobio
— Radio Villa Francia (@rvfradiopopular) April 24, 2014
Maelfu ya vijana walishiriki kwenye maandamano ya kwanza ya wanafunzi yaliyofanyika mwaka huu mwezi Machi huko Concepción.
Kulikuwa na maandamano kwenye miji mingine kwenye maeneo ya mashambani pia, kama vile Iquique, Valparaíso, jiji ambalo ndiko liliko Bunge la Taifa, na Valdivia.
K abahati mbaya, kwenye baadhi ya maeneo maandamano yalikabiliwa na usumbufu wa hapa na pale, hasa uliosababishwa na watu wengine wasiokuwa wanafunzi na ambao hawakuwa na maslahi yoyote kwenye madai hayo.
Naschla Aburman, rais wa Feuc, aliviita vitendo hivyo vya usumbufu kama “matukio machache” na kusema kwamba vitendo hivyo havikuwa wajibu wa waandaaji.
Watumiaji wa Twita walitoa maoni yao kuhusu ukweli huo, wakisambaza picha na taarifa kuhusu matukio hayo:
AHORA: Intendente @orrego dice que “no hubo ningún incidente” durante marcha estudiantil. Sí “violentistas organizados” al final de ella
— Mauricio Bustamante (@tv_mauricio) May 8, 2014
SASA: Gavana Orrego anasema, “hapakuwa na matukio yoyote” wakati wa maandamano ya wanafunzi. Hata hivyo, kulikuwa na “watu waliokuwa wamepangwa kufanya vurugu” katika maandamano hayo.
Universidad Central denunció daños por 20 millones de pesos tras marcha estudiantil http://t.co/FzRaeoNUa8 pic.twitter.com/bFNv4ACkKL
— Cooperativa (@Cooperativa) May 8, 2014
Chuo Kikuu cha Central kilitoa taarifa kuwa kulikuwa na matukio ya uharibifu wa mali zenye thamani ya pesos milioni 20 [kama dola za Marekani 36,000] baada ya maandamano ya wanafunzi.
General Ricardo Solar informa que el número de detenidos tras la marcha estudiantil son 101
— La Tercera (@latercera) May 8, 2014
Jenerali Ricardo Solar anasema kuwa idadi ya watu waliokamatwa baada ya maandamano ya wanafunzi inafikia 101.
@romina_ms @CNNChile Romina, yo soy estudiante, y estoy de acuerdo con la marcha pacifica, pero estos grupos son organizados.
— Rodrigo Gacitúa G (@RGacitua_G) May 8, 2014
Romina, mimi ni mwanafunzi, na ninaunga mkono maandamano ya amani, lakini haya makundi yalipangwa.
2 maoni