Honduras: Zelaya Akamatwa na Kuondolewa Madarakani

Nchini Honduras siku ilianza na habari zinazosema kwamba Rais Mel Zelaya amekamatwa akiwa nyumbani kwake na wanajeshi wenye silaha. Kura ya maoni ilikuwa imepangwa kupigwa siku hiyo, kura hiyo ilikuwa inapingwa na mahakama ya juu, na majeshi ya nchi pamoja na baraza la wawakilishi. Siku chache kabla, Zelaya alimuondoa madarakani mkuu wa majeshi, Jenerali Romeo Vasquez Velasquez, jambo ambalo lilifuatiwa na kujiuzulu kwa wanajeshi wengine wa vyeo vya juu kwa sababu hawakukubaliana na kura hiyo ya maoni.

Mara baada ya hapo ilifahamika kuwa Zelaya amepelekwa nchini Costa Rica, ambako aliendelea kujiita kuwa yeye ndiye mkuu halali wa nchi. Kadhalika palikuwa na uvumi kuwa Zelaya amejiuzulu. Hata hivyo, barua inayodaiwa kueleza hivyo iligundulika kuwa ni ya uongo kama anavyobaini Juan Carlos Rivera wa Miradas de Halcón [es]. Maoni ya mwanzo katika ulimwengu wa blogu na ule wa Twita yalitofautiana kutokea yale yanayosema kwamba hali iliyopo ni sawa na mapinduzi ya kijeshi mpaka yale yanayosema kuwa ile ilikuwa ndio njia pekee ya kukomesha jitihada za Zelaya za kutaka kugombea urais kwa awamu nyingine tena.

Picha na Roberto Brevé na inatumika hapa chini ya hati miliki huria http://www.flickr.com/photos/breve/3668996322/

Picha na Roberto Brevé na inatumika hapa chini ya hati miliki huria http://www.flickr.com/photos/breve/3668996322/

Umeme umekuwa ukikatika-katika katika mji mkuu wa nchi, kama inavyoripotiwa na gazeti la Honduras Daily News ambalo linahisi kuwa kukatika huko kwa umeme ni moja ya “jitihada za kuzuia upashanaji habari.” Hata hivyo habari zimekuwa zikitoka kwa kutumia mitandao ya kijamii kama vile Twita na Blipea ambayo ilikuwa hai kutwa nzima.

Hibueras[es], mmoja wa wanaomuunga mkono Zelaya aliandika :

Manuel Zelaya fue detenido y sometido por la furza bruta de la jauria criminal de nuestra historia esclavista para evitar que el pueblo hondureño posea el poder de inclusion y de construccion de su patria, los responsables de tan ignomioso acto son todos conocidos y pagaran caro su abuso.
Llegó la hora de buscar por otros medios, lo que se nos niega por la paz, y los responsables seran jusgados por sus actos de traicion a la patria.

Manuel Zelaya alikamatwa na kudhuriwa na nguvu katili za waovu ambazo zimewatia utumwani watu wa Honduras, ili kuwazuia watu wasijichukulie nguvu ambazo zingepelekea ushirikishwaji na ujenzi wa nchi yao, wale ambao wanawajibika na tendo hili chafu wanajulikana vizuri na wataulipia uonevu wao.
Huu ni wakati wa kutafuta kwa njia nyingine yale mambo ambayo tunanyimwa (tunapoyatafuta) kwa njia halali, na wale wanaowajibika kwa vitendo vya uhaini watahukumiwa.
Wanaomuunga mkono rais Mel Zelaya, picha na Roberto Brevé na inatumika hapa chini ya hati miliki huria. http://www.flickr.com/photos/breve/3668437385/

Wanaomuunga mkono rais Mel Zelaya, picha na Roberto Brevé na inatumika hapa chini ya hati miliki huria. http://www.flickr.com/photos/breve/3668437385/

Baadaye siku hiyo, Bunge lilipiga kura ya kumuondoa madarakani Zelaya kama rais na kumuweka Roberto Micheletti ambaye alikuwa ni mkuu wa baraza la wawakilishi. Mara tu baada ya kupewa madaraka, alitangaza kuwa uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa mwezi Novemba. Kuwekwa madarakani kwa Micheletti kama kaimu rais kumezua kauli za ukosoaji kutoka kwa maswahiba wa karibu wa Honduras, hasa Venezuela, ambayo imetishia kutumia nguvu za kijeshi ikiwa mfanyakazi yeyote wa ubalozi wake aliyepo nchini Honduras atatekwa au kuuwawa. Zaidi ya hilo, Rais Hugo Chavez ametamka kwamba serikali mpya inayoongozwa na Micheletti itashindwa.

Watumiaji wa huduma ya Twita kama vile Hugo Chinchilla wanahofu matamko yalitolewa na Chavez na wanayachukulia kama ishara kuwa maswahiba kama hawa wanahusika. Aliambiwa ‘kiholela’ kuwa jeshi linajiandaa kukabili uvamizi wa majeshi ya Venezuela na Nicaragua [es].

Na kuna wengine kama Jorge Garcia ambaye anaiunga mkono serikali mpya na anatoa rai kwa watumiaji wenzie wa Twita kutoa msaada maji na chakula kwa wanajeshi [es]. Kadhalika anaeleza:

En #honduras no hubo golpe de estado, el estado de derecho continúa, la constitución sigue vigente.

Nchini #honduras hapajatokea mapinduzi ya kijeshi, utawala wa sheria bado unaendelea, katiba bado inatumika.

Kwa kuwa hivi sasa macho ya dunia yako nchini Honduras, Wilmer Murillo anahofia kutengwa na jamii ya kimataifa. Anaomba:

que devuelvan a Mel! estamos quedando como retrogradas ante los ojos del mundo.

Turejesheeni Mel! Tunaonekana kama nchi duni katika macho ya dunia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.