Kwenye Jiji Lenye Machafuko Zaidi Duniani, Wasanii wa Uchoraji Kuta Watumia ‘Silaha zao’ Vizuri

Graffiti artist Rei Blinky at work in San Pedro Sula, Honduras. Credit: Nathaniel Janowitz. Used with PRI's permission.

Msanii wa uchoraji kuta, Rei Blinky akiwa kazini huko San Pedro Sula, Honduras. Shukrani kwa: Nathaniel Janowitz. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI.

Makala hii pamoja na ripoti ya radio vimeandaliwa na Susannah Roberson kwa ajili ya The World na kwa mara ya kwanza iliwekwa PRI.org mnamo tarehe 26 Juni, 2015, na inachapishwa tena hapa kwa makubalino ya ubia wa kubadilishana maudhui.

Uzio wa seng'enge, mitaa mitupu, na walinda usalama wakiwa na bunduki. Ni kama vile kipande cha filamu ya dystopia, lakini siyo filamu. Hii ni San Pedro Sula, Honduras, jiji ambalo limetajwa kuwa na machafuko kuliko jiji lingine lolote duniani kwa miaka minne mfululizo.

Hivi karibuni, jiji la San Pedro Sula limejaribu kujijengea jina lenye matumaini mema. tried to make a much more optimistic name for itself: mahali palipo shamiri kwa sanaa. Shukrani ziwaendee wasanii wa uchoraji kuta ambao picha zao za ukutani za kupendeza zinaonekana maeneo mbalimbali ya jiji.

Msanii wa uchoraji kuta, Rei Blinky ndiye haswa mwandishi wa habari Nathaniel Janowitz anamhesabu kuwa ndiye “mwanzilishi” wa harakati hizi kupitia sanaa iliyoenea maeneo mbalimbali ya Jiji. Blinky ndiye msanii wa kwanza kuvinjari kwenye mitaa ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imekimbiwa na watu. Hisia mbaya dhidi ya jiji hili zinahusishwa na magenge ya kihalifu. “Huwezi kufahamu ni wakati gani kurushiana risasi kunaweza kutokea kati ya genge moja na jingine. Kwa hiyo, unaweza kujikuta umepigwa risasi wakati unatembea mtaani,” anasema Janowitz.

Siyo tu magenge haya yanatawala mitaa, hata na uchoraji wa kuta pia umechukua nafasi katika mitaani. Blinky alifanya mageuzi makubwa kwa kuja na namna yake mpya ambayo Janowitz anaiita “pop-art indigenous.” Kazi yake inaonekana vizuri, yenye rangi za kuvutia na isiyo na makosa. “Huyu ni mmoja wa wale wasanii ambao ukipitia kazi zake utajua tu kuwa ni yuleyule Rei Blinky.Hakuna mwingine kama yeye” anasema Janowitz.

Blinky amefungua njia ya wasanii wengine wengi kujiunga naye. “Harakati hizi zimeshaenea kwa kiasi kikubwa, kuna michoro mingi ya kuvutia sana jijini”, anasema Janowitz. Wasanii wengi wengine wamejizolea umaarufu kwenye mitaa mbalimbali: Baruc, katika kazi zake, anawapa wanawake wa honduras nafasi kubwa, wakati Carlos Badia rbrbs anaandaa kazi zake katika maudhui tofauti tofauti.

“Inaonekana kuwa watu wa San Pedro Sula, wanatambua kuwa uwepo wa magenge ya wahalifu ni tatizo lililo dhahiri, wanatambua pia hawawezi kuishi maisha ya hofu vile vile. Hivyo, wanalazimika kwenda mitaani na kuitafuta amani kwa njia ya utulivu,” anasema Janowitz. “Kama hawapo tayari au hawana vitendea kazi ili waende kudai amani kwa bunduki, wataenda na vishungi vya kupaka rangi.”

Wasanii wa uchoraji kuta wana mategemeo ya kuwafikia vijana wadogo wa San Pedro Sula,wengi wao wakifanya juhudi za kulikimbia jiji kuliko kuendelea kuishi kwenye jiji lenye ghasia. “Kwa sasa, inaonekana idadi kubwa ya watoto jijini, kama siyo kujiunga na magenge basi wanachagua kukimbia,” anasema Janowitz. Blinky pamoja na wasanii wenzake wanafanya kila juhudi kuwapa vijana njia mbadala ya kujieleza kwa amani. Janowitz anasema kuwa, moja ya malengo yao makubwa ni kufanya kazi na watoto, kuwatoa mitaani na kuwafundisha sanaa.

Blinky ameanza kusambaza sanaa yake nje ya Honduras. Shukrani zimwendee yeye pamoja na wasanii wenzake, Janowitz anasema kuwa, kuna mengi mazuri yataanza kuonekana San Pedro Sula. Janowitz ana imani kuwa, Blinky atafanikiwa. Kazi ya Blinky ni ya kipekee, anasema hivi kwa kuwa, “kazi yake inaweza kuonekana ukutani au kwenye luva. Yeye ni aina ya wasanii wazuri kabisa.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.