Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices: Anahitaji Kutendewa Haki

Matangazo ya yaliyojiri wiki hii hapa Global Voices yanaangazia baadhi ya habari kubwa zilizojitokeza kwenye habari zetu za Global Voices. Wiki hii, tunakuletea habari za wanawake wanaosaka au waliokwisha kupata haki yao nchini Poland, Uruguay, Urusi na Syria.

Shukrani nyingi kwa Kasia OdrozekFernanda CanofreIsaac Webb, Marcell Shehwaro na Lara AlMalakeh na waandishi wetu wote, watafsiri na wahariri waliotusaidia kufanya kipindi hiki kikujie.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa Jahzaar; Mario Bava Sleeps In a Little Later Than He Expected To wa Chris Zabriskie; City Night Line wa Cobra (avec logo panthère); Clover wa Little Glass Men; Vintage Frames wa Kai Engel; na Am I The Devil (Instrumental) wa YEYEY.

Picha inayopamba habari hii ni ya wanawake na wanaume wakiwa wamevaa nguo nyeusi kama namna ya kuonesha upinzani wao kwenye #MaandamanoMeusi jijini Berlin. Picha ya Kasia Odrozek, CC BY.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.