Watu wa Uruguay Waomboleza Kifo cha Mwanamuziki José Carbajal, ‘El Sabalero’

Mwimbaji na mtunzi José Carbajal, anayejulikana kwa jina la utani kama “el Sabalero,” alikutwa amekufa nyumbani kwake huko Villa Argentina, Uruguay tarehe 21 Oktoba; alifariki kutokana na shambulio la moyo akiwa na umri wa miaka 66. José Carbajal anachukuliwa kuwa gwiji na utambulisho wa Uruguay “canto popular” [wimbo maarufu] wa Uruguay kama anavyoeleza Martin Charquero (@MartinCharquero) kupitia Twitter. Kwa siku nzima , watu wa Uruguay wamekuwa wakizungumza jinsi walivyositushwa na habari ya kifo hicho kupitia mitandao ya kijamii; na, kama Mariu (@mariu070) alivyosema kwenye Twitter,

La musica Uruguaya de luto por el fallecimiento del Gran Sabalero

Wanamuziki wa Uruguaya wanaomboleza kifo cha “Cabalero mkuu”

Picha ya Wikimedia Commons, kama ilivyotumwa na mtumiaji Zeroth na kutumika kwa idhini ya Attribution-ShareAlike 2.0 Generic Creative Commons license

José Carbajal [es] aliondoka Uruguay katika miaka ya 70 wakati wa utawala wa kijeshi. Aliishi nchini Argentina, Spain, Mexico, France, na mwishowe nchini Uholanzi. Alirudi nchini kwake mwaka 1984, lakini akaondoka kwenda kuishi Uholanzi tena mwaka 1992; amekuwa akienda na kurudi kati ya Uruguay na Uholanzi kwa kipindi cha miaka 14 iliyopita. Katika wimbo wake “Borracho pero con flores” [Amelewa lakini ana maua] anaimba:

Soy cantor, cantándole a mi pueblo voy
de país en país
dejo en versos lo mejor de mí
y me llevo su calor

Mimi ni mwimbaji, naiimbia nchi yangu natembea
nchi mpaka nchi
Ninaacha huko beti zangu nzuri
na nachukua uzuri wake pamoja nami

Katika wimbo huohuo ana staajabu juu ya Montevideo, “ipo mbali na inavutia”:

Watumiaji wa Twitter wamekuwa wakiukumbuka wimbo huo na nyimbo nyingine za Carbajal. Fernando Francia (@fernandofrancia) anaandika:

Haganme un favor… ríndanle un homenaje a EL SABALERO, trovador y luchador (youtube: angelitos, no te vayas nunca, a mi gente)

Nifanyieni fadhila…Mpeni heshima EL SABALERO, mwanamashairi na mpiganaji (youtube: angelitos, no te vayas nunca, a mi gente [nyimbo za Carbajal])

Pablo Olivera (@pabli31) anawachagulia wasomaji wimbo maarufu sana wa El Sabalero, “Chiquillada”:

hoy los uruguayos estamos tristes se nos fue un grande de nuestra musica se nos fue el sabalero . Chiquillada – Jose Carbajal.vía @youtube

Leo sisi watu wa Uruguay tuna huzuni [kwa sababu] mtu muhimu sana katika muziki wetu ametutoka, el sabalero. Chiquillada- Jose Carbajal. kupitia @youtube

Kwenye Blogu Pensamientos… [fikra], Fiaris kwa kifupi anatafakari [es] juu ya kifo cha José Carbajal, akitaja wimbo “Chiquillada”:

Nos dejo muchas canciones que sabemos todos desde que eramos muy jóvenes qué son vivencias Uruguayas como esta que se llama “Chiquillada”y relata la niñez de antaño.

Ametuachia nyimbo nyingi ambazo tulizijua tangu tukiwa wadogo, zimezoeleka na zitakumbukwa na wana Uruguay hasa zaidi ule unaoitwa “Chiquillada” ambao unatukumbusha enzi za utoto wetu.

Hii video ya kiraia inamuonesha El Sabalero akiimba sehemu ya wimbo “Chiquillada”:

José Carbajal na Mpango wa Ceibal

Mwaka huu, José Carbajal alikuwa akifanya kazi sambamba na wasanii wa Uruguay katika mradi wa “Ceibal Canta” [Ceibal aimba]. Mradi huo ni sehemu ya Mpango wa Ceibal, wa Kompyuta za Mapajani Moja kwa Kila Mtoto mpango ambao utampatia kila mtoto anayesoma shule za serikali nchini Uruguay kompyuta ya mapajani. Mnamo mwezi Januari, tovuti ya 180 [es] ilimuhoji José Carbajal na ikamuuliza kuhusuiana na mradi huo “Ceibal Canta.” Hapa inauchambua mradi huo:

Se trata de una serie de más de 120 conciertos que dará para todos los alumnos de cuarto, quinto y sexto de las escuelas públicas. El proyecto se inscribe en el Plan Ceibal ya que el espectáculo estará disponible en ese portal.

Huu ni mtiririko wa matamasha zaidi ya 120 ambayo yatawezesha kupatikana kwa laptop watakazogawiwa wanafunzi wote wa shule za serikali kuanzia daraja la nne, tano na sita. Mradi huu ni sehemu ya mpango wa Ceibal kwa sababu maonesho yatafanyika katika tovuti hiyo.

Carbajal alielezea mradi huu kwa mtazamo wake binafsi:

Vamos a hacer una especie de estampa del Uruguay geográfico: ríos, montes, arroyos, barriadas, pueblos en canciones y palabras. Además, vamos a dar datos de la producción de cada región, proyectando cosas, con buena iluminación. […] Es una especie de aula abierta.

[…]

Vamos a hablar de todo un poco. En cada región de Uruguay cambia la producción y entonces le vamos a contar a los chiquilines las cosas de su lugar. Hacemos una pintura del Uruguay, de todo el territorio, y también del lugar donde estamos.

Tutatengeneza aina fulani ya muhuri wa jiografia ya Uruguay: mito, vilima, mikondo ya maji, majirani, miji katika nyimbo na maneneo. Pia tutawapatia maelezo ya kweli juu ya ya uzalishaji mali katika kila mkoa, tukionesha vitu kwa mwanga mzuri. […] Ni kama darasa la wazi.

[…]

Tutaongelea kidogo kuhusu kila kitu. Katika kila mkoa nchini Uruguay uzalishaji hubadilika na kwa hiyo tutawaambia watoto mambo kuhusu maeneo yao. Tunatengeneza picha ya Uruguay, eneo lote, na pia eneo ambalo tutakuwapo.

Tovuti ya “The Plan Ceibal” imetengeneza ukurasa unaoitwa “Homenaje al Sabalero” [es] [heshima kwa El Sabalero] ambao unatoa taarifa kuhusu José Carbajal ambazo wanafunzi wanaweza kuzipata kupitia OLPC laptop.

Wanamuziki Washington Carrasco na mkewe Cristina Fernández walikuwa wakifanya kazi na Carbajal katika mradi wa “Ceibal Canta”; hata siku ya kifo cha Carbajal, Carrasco alisema [es]:

Quien escuche al Sabalero, está escuchando al Uruguay, el lenguaje uruguayo, sus costumbres.

Yeyote anayemsikiliza Sabalero, anaisikiliza Uruguay, Lugha ya watu wa Uruguay, na utamaduni wake.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.