Tamko Kuhusu Mustakabali wa Ushirikiano katika Mtandao wa Intaneti.

Wawakilishi wa mashirika yanayoratibu miundombinu ya kiufundi ya huduma ya intaneti waliokutana huko Montevideo; Uruguay, wametoa tamko kuhusu mustakabali wa ushirikiano katika masuala ya Intaneti [es], ambapo walifanya uchanganuzi kuhusiana na changamoto zinazoathiri mustakabali wa mtandao wa Intaneti.

Pamoja na mambo mengine, walizungumzia umuhimu wa upatikanaji wa mtandao wa intateti usio na mashaka na kuonya dhidi ya tofauti za upatikanaji wa mtandao wa intaneti zilizopo katika ngazi ya kitaifa, huku wakionesha mashaka yao dhidi ya kuongezeka kwa kukosekana kwa uhuru wa watumiaji wa mtandao ulimwenguni kufuatia matukio ya hivi karibuni ya kuchunguzwa na kufuatiliwa.

Hatua hii, kwa namna moja, inaweza kuchukuliwa kuwa ni matokeo ya mapendekezo yaliyokuwa na muelekeo wa namna hiyo, kama vile maoni yaliyoelekezwa Umoja wa Mataifa (UN) na Rais wa Brazil, Dilma Roussef na maoni juu ya utendaji kazi wa uwepo wa vikwazo vya mtandao wa intaneti(NSA).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.