Baraza la Seneti la Urugwai lilipiga kura 16 kwa 13 kuhalalisha uzalishaji na uuzaji wa bangi.. Rais Mujica anatarajiwa kutia saini sheria, ambayo itakuwa na ufanisi kuanzia mwaka ujao.
Estoy a favor de legalizar la Marihuana pero estaria bueno ser noticia en el mundo por nuestra Seguridad y Educacion
— Colorado # 36.048 (@Colorado7411) December 11, 2013
Mimi ninaunga kuhalalishwa kwa bangi, lakini itakuwa vizuri kugonga vichwa vya habari duniani kote kwa sababu ya usalama wetu na elimu.
Ignacio de los Reyes, mwanahabari wa BBC Argentina na Southern Cone, alitwiti mnamo Desemba 10:
Mamia ya vijana tayari wanasheherekea kukaribia kwa kuhalalisha bangi katika #Uruguay pic.twitter.com/Ac9MLiOBbd
— Ignacio de los Reyes (@BBC_DelosReyes) Desemba 10, 2013
Stay tuned for more citizen reactions.
1 maoni