Margarita Mbywangi alipokuwa na umri wa miaka mitano, alichukuliwa kutoka kwenye uangalizi wa wazazi wake na kuuzwa mara kadhaa ili kutumikishwa katika nyumba za tabaka la kitajiri la wa-Paraguai. Jambo hili lilikuwa la kawaida sana kwa jamii ya watu wa Aché nchini Paraguai hususani wakati wa utawala wa kimabavu wa Alfredo Stroessner(1954-1989). Taratibu hizi lilikuwa namna ya wamilikaji wa ardhi kuwaondoa wa- Aché katika ardhi ya mababu zao na kisha kuzimiliki. Matokeo ya kuondoshwa huku kwa nguvu ni kuwa, vijana wadogo wa jamii ya Aché walijikuta wakiwa mbali na nyumba zao na pia mbali na sehemu walipozaliwa.
Kwa sasa, Mbywangi anajihusisha na mradi wa Sauti Zinazoinukia (Rising Voices Project) Aché djawu (The Aché word) [es], na siku za hivi karibuni aliandika makala fupi katika blogu yake [es] kuhusiana na maisha yake:
Yo Mbywangi me contaron que nací en Kuetuvy en el año 1962, a los 5 años me robaron de mi madre en la época de la dictadura, crecí en una familia paraguaya hasta los 16 años, a la edad de 20 años volví con mi familia aché en la comunidad Chupapou en 1980. No encontré a mis padres, sólo encontré a mis hermanos.
Mbywangi aliporejea nyumbani katika miaka ya 1980 hivi, alifanikiwa kupata mafunzo ya unesi na pia alijaaliwa kuwa na watoto. Katika blogu yake, aliongeza kuwa:
En el 81 tuve mi primer hijo y dije, ahora sí tengo un compañero, en ese dia estuve completa. Pasé aquellos años criando mi hijo y atendiendo la salud de la gente de mi comunidad.
Hata hivyo, miongo kadhaa baadae, alijihusisha sana na siaza za kutetea haki za wazawa. Kwa mara ya kwanza, alikuwa mgombea wa kwanza katika Bunge la Paraguai na pia aliwahi kuhukumiwa na kwenda jela kwa sababu ya kuitisha maandamano ya kupinga hifadhi za uoto wa asili zisiharibiwe kwa ukataji wa magogo kinyume cha sheria [es]. Mwaka 2008, Mbywangi alipokea mwaliko kutoka kwa utawala wa Rais wa zamani Fernando Lugo ili awe Waziri anayeshughulika na mambo ya wazawa. Hatimaye akawa mtu wa kwanza kutoka katika jamii ya wazawa kushika wadhifa huo.
Kama sehemu ya mradi wa Sauti Zinazoibukia (Rising Voices Project), Mbywangi ameamua kutumia blogu kwa lengo la kuujulisha ulimwengu kuhusiana na yale aliyoyapitia. Pia, ameshafungua ukurasa wake wa Twita (@MargaMbywangi), lakini bado anaendelea kujijengea mazoea ya kuiboresha mara kwa mara. Katika video hii, anaelezea kuhusu umuhimu wa kuweka bayana historia ya maisha yake kwa wanajamii wenzake wazawa na hata hadhira yake pana ulimwenguni kote.
Anahitimisha makala katika blogu yake kwa kuelezea jina lake katika utamaduni wa ki- Aché:
Me encanta que me llamen Mbywangi porque es el nombre que me puso mi mamá de sangre, y Margarita me puso mi segunda mamá aunque no fui reconocida por ellos como hija. Sólo tengo mi nombre y me siento feliz con los dos nombres que tengo.