Paraguai: Rais Lugo Kutopokea Mshahara

Utawala wa Rais Ferdinand Lugo umeanza na tangazo kuwa hatapokea mshahara wake wa mwezi. “Sihitaji mshahara huo, ambao unapaswa kumilikiwa na masikini,” alisema Lugo. Mabloga nchini humo wanatofautiana mitazamo, wakati mmoja anausifu uamuzi huo, mwingine anajiuliza ni vipi Rais lugo atajilipia gharama binafsi za maisha.

Carlos Rodriguez wa Rescatar [es] anatoa muhtasari wa jinsi baadhi ya wanahabari ambao wanarahisisha kitendo hicho kwa kusema kuwa padri huyo wa zamani hana mke wala watoto wa kuwalea, wakati wengine wanajiuliza iwapo atatumia fedha alizokwisha kuzihifadhi. Hata hivyo, Rodriguez anaangalia mambo tofauti:

Katika tangazo la Lugo kusamehe mshara wake, tunaona ujumbe wake ni kwamba “sipo hapa kwa ajili ya pesa.” Ni ujumbe ulio juu na wenye umuhimu mkubwa kwenye nchi ambayo asilimia kubwa ya wanasiasa, huingia kwenye nyanja hiyo kutafuta nguvu za kisiasa ambazo huwakisha kwenye nguvu za kiuchumi kwa muda mfupi inavyowezekana, kwa kuiba.

Hata hivyo, jorge Torres Romero wa Detras del Papel [es] haoni mambo katika njia hiyo na anfikiri ulikuwa uamuzi usio makini:

Siku baada ya tangazo la Lugo, wanahabari wachache waliuliza swali je ni nani ana hiyari ya kufuata mfano wa rais. Ni wazi, hakuna mmoja, Federico Franco (Makamu Mpya wa Rais), kwa mfano, alisema yeye ana familia ya kutunza na kwamba hataghairi haki yake ya kupokea mshahara.

Rais ataishi kwa kutumia nini? Nani atakayelipia gharama za mavazi yake, chakula chake, na gharama nyingine atakazozikabili? Je ana akiba kubwa kiasi hicho? Je ataishi kutokana na kodi ya mali zake? Je atajilipia kodi? Au atasubiri misaada, zawadi na mialiko kutoka kwa marafiki zake?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.