Paraguay: Wenyeji Wanyunyiziwa Dawa za Kuua Wadudu kwa Ndege

Huko Mashariki mwa Paraguay, jumla ya watu 217 wa jumuiya ya wenyeji ya Ava Guaraní walianza kusumbuliwa wakionyesha dalili mbalimbali za kiafya zinazoaminika zilisababishwa na unyunyiziaji wa makusudi wa dawa za kuua wadudu hasa baada ya wao kuwa wamegoma kuhama kutoka katika ardhi waliyoirithi kutoka kwa mababu zao.

Watendaji wa serikali wamethibitisha kwamba baadhi ya sehemu za ardhi ya wenyeji iliyo katika Wilaya ya Itakyry katika Idara ya Alto Paraná ilinyunyiziwa wakati ambapo hakukuwa na mazao yoyote [es]. Ishara nyingi zinaelekezwa kwa walima maharage ya soya wa KiBrazili kwamba ndiyo wanaohusika na unyunyiziaji huo, kwani kwa kiasi kikubwa ardhi iliyo mikononi mwa jamii za wenyeji ingefaa sana kwa zao hilo na kwamba hawa wamekuwa katika mgogoro na Ava Guaraní kuhusu umiliki wa takribani hekta 3,000, kwa mujibu wa blogu ijulikanayo Interparaguay [es].

José Ángel López Barrios wa Bienvenidos! [es] akielezea eneo la jamii lililo mbali na mengine ambapo tukio hilo lilitokea:
Itakyry es uno de los distritos del Departamento de Alto Paraná, distante a unos 450 kilómetros de Asunción, capital de la Republica, se llega a el por caminos no pavimentados, su época de esplendor se dio en la época de las explotaciones yerbateras. Que termino al cabo de 100 años abriendo paso a la explotación de la soja en estos últimos tiempos……

Itakyry ni moja ya wilaya za Idara (Mkoa wa) Alto Paraná, iliyo umbali wa kilomita 450 kutoka katika mji mkuu wa Asunción. Kufika huko mtu huna budi kutumia barabara za vumbi, katika kilele cha mafanikio yake ilikuwa ni wakati wa ulimaji wa yerba maté. Jambo hilo lilikoma baada ya miaka 100, na kupisha ulimaji soya katika miaka ya hivi karibuni……

Ni mahitaji ya maharage ya soya na bei yake inayozidi kupanda ambayo inaifanya ardhi hiyo kuwa inayofaa kwa zao hili lenye kipato kikubwa sasa. Sehemu ya ardhi hii iko kwenye ardhi ya kurithi ya mababu wa jamii za wenyeji, kama vile Guaraní. Mwanablogu Carlos Rodríguez wa Rescatar [es] hafikiri kwamba tukio la unyunyiziaji dawa dhidi ya makundi ya wenyeji ni tukio dogo, analiita tendo hilo kama “mauaji ya halaiki“:

Hubo un tiempo en que en Paraguay los aborígenes no eran considerados seres humanos. Eran cazados como animales y sus crías rescatadas como trofeos.
(…)
Otros fueron apropiándose a bala y sangre de sus tierras y como los indígenas no hacían gestiones ante las instituciones encargadas de titular las tierras que siempre les pertenecieron, el hombre blanco si lo hizo y se plantea el contrasentido de que los legítimos dueños de estas tierras, hoy son “los invasores”.
Y siguen siendo tratados como animales. Sólo así se puede entender que los productores de soja les envíen aviones fumigadores para lanzarles venenos encima, tal como lo ha comprobado el Ministerio de Salud que socorre en estos momentos a los indígenas intoxicados por plaguicidas para soja.

Kuna kipindi hapa Paraguay ambapo WaAborigino hawakudhaniwa kuwa ni binadamu. Waliwindwa kama wanyama na watoto wao walichukuliwa kama mapambo fulani hivi.
(…)
Sehemu ya ardhi yao iliporwa kwa risasi na damu, na hasa kwa kuwa wenyeji hawa hawakwenda kwenye mamlaka zinazohusika na utoaji hati miliki za ardhi kuhusu ardhi ambayo daima wameimiliki, Wazungu hawakwenda kwenye taasisi hizo, na katika jambo ambalo ni la kushangaza, hawa wanaochukuliwa kwamba wao ndiyo wamiliki wa ardhi hiyo ni hawa “wavamizi”.
Wanaendelea kutendewa kama wanyama. Ni kwa njia hii tu ambapo mtu anaweza kuelewa kwa namna gani wazalishaji wa soya wanaweza kutuma ndege za kunyunyiza dawa ya sumu dhidi ya wenyeji, jambo ambalo limethibitishwa na Wizara ya Afya, ambayo sasa inajaribu kuwasaidia wenyeje walioathiriwa na sumu hiyo.

López Barrios pia anaona aibu kwa hitoria ya vitendo vibaya vinavyofanywa na jamii za wenyeji huko Paraguay [es]. Kama mtoto wa wahamiaji kwenye nchi hii, anaandakika kwamba matukio hayo “yanamfanya atamani kurejea Ulaya… lakini kwa kweli …angependa wanyonyaji hao waondoke zao.”

Ensañarse con un pueblo indígena que tiene más de 38 siglos de existencia en sus propios y verdaderos territorios, no me parece apropiado…. Si no respetamos a nuestros mayores nuestros días se acortaran sobre la tierra y si anteponemos la avaricia a cualquier otra virtud caeremos sin remedio…..

Kuwachukia wenyeji ambao wameishi hapo kwa zaidi ya karne 38 kwenye ardhi yao wenyewe, si jambo la kukubalika kwangu …. Kama hatuwaheshimu wakubwa zetu, basi siku zetu duniani zitafupishwa, na kama choyo (tamaa) ikiwekwa mbele ya kitu chochote, ipo siku tutaangamia ….

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.