Paraguai: Kuapishwa Kwa Lugo Kwenye Flickr

Askofu wa zamani wa kanisa Katoliki, Fernando Lugo, hivi karibuni aliapishwa kama rais mpya wa Paraguai, tarehe 15 Agosti. Kuibuka kwake kukamata uongozi kumewasisimua WaParaguai walio nyumbani na walio ughaibuni. Kwa wale ambao walishindwa kuwepo kwenye mji mkuu wa Asuncion kushuhudia sherehe, picha zinaweza kupatikana katika ukurasa rasmi wa picha za kiongozi huyo kwenye Flickr.

Juhudi za kuorodhesha nyendo na shughuli za Lugo zilianza wakati wa kampeni yake mwezi Januari 2008. Hivi sasa karibia picha 2,500 zilizo katika haki miliki za huria kwa umma, inatarajiwa kuwa matumizi ya chombo hiki cha habari yataendelezwa hata wakati wa serikali yake mpya.

Katika siku chache zilizopita, picha za lugo wakati wa kuapishwa kwake zimeonyesha msisimko wa tukio hili la kihistoria.

Wakati wa Kuapishwa. Picha na Fernando Lugo zilizo chini ya haki miliki huria.

Na zaidi, picha pamoja na viongozi wenzie wa nchi za Marekani ya Kusini pia zinaweza kupatikana.

Hugo Chavez wa Venezuela na Lugo. Picha na Fernando Lugo zilizo chini ya haki miliki huria.


Evo Morales wa Bolivia na Lugo. Picha na Fernando Lugo zilizo chini ya haki miliki huria.


Lula da Silva wa Brazil na Lugo. Picha na Fernando Lugo zilizo chini ya haki miliki huria.


Cristina Kirchner wa Argentina na Lugo. Picha na Fernando Lugo zilizo chini ya haki miliki huria.


Rafael Correa wa Ecuador na Lugo. Picha na Fernando Lugo zilizo chini ya haki miliki huria kwa umma.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.