Mashariki ya Kati: Mawasiliano ya Siri Ambayo Sio Siri ya Ubalozi wa Marekani

Secret US Embassy Cables Unveiled

Wakati vyombo vya habari vikuu Uarabuni vimeyapokea mawasiliano ya siri ya Ubalozi wa Marekani yaliyotolewa jana kwa bega baridi, wanablogu na watumiaji wa Twita kutoka Mashariki ya Kati walipata habari zinazohitajika sana kwa uchambuzi.

Toleo lililokuwa linatarajiwa sana, release, kutoka tovuti inayotoboa siri Wikileaks, linatarajiwa kuweka hadharani zaidi ya mawasiliano 250,000 ya waya – ambayo ni seti ya nyaraka za siri kubwa zaidi kuwekwa hadharani. Kuanzia furaha mpaka kutia shaka, na kejeli mpaka hisia hasi, wananchi wa mtandaoni waliyapanga mawasiliano yanayohusiana na Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na kuwasha cheche za majadiliano, huku wakihoji nia na kutafuta majibu.

Kwingine katika Mashariki ya Kati, hali ya msuguano inaendelea kukua kufuatia kuwekwa wazi kuwa nchi za Kiarabu zimejadili mashambulizi ya pamoja na Marekani dhidi ya Irani, wakati ambapo kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu nia ya Irani ya kuwa na nguvu za nyuklia; wanasiasa wa Kiarabu na Kiisraeli wanalala kitanda kimoja; kadhalika simulizi mbalimbali za misuguano kati ya majirani ndugu, ambao wanaunda ulimwengu wa nchi za Kiarabu.

Mmisri Sandmonkey anaelezea uvujaji wa nyaraka hizo za za siri kama tukio “tukufu”::

Wakati ambapo serikali ya Misri ilipodhani kuwa imemalizana na
maumivu ya kichwa ya uchaguzi, imekuja Wikileaks (mvujo wa nyaraka za siri) na ******.
Yalikuwa na malipo ya vitendo vyao. Shukurani kwa Wikileaks nilijihisi kama vile mtoto
ambaye aliruhusiwa kusikiliza maongezi ya watu wazima kwa mara ya kwanza.
Na kama hiyo haikuwa tamu vya kutosha, kuona kila tathmini
ya sera ya nchi za nje ambayo nimewahi kuifanya imehakikishwa kwa njia hii? Kutosheka, ndio elezo lake. Kwa
miaka mingi nimekuwa nikiongelea ushirika wa Sunni-Israel. Kwa
miaka mingi nimekuwa nikiusubiri wakati ambao maneno
ya mitaani Uarabuni yatakapokutanana ukweli na kwa mhimili wa siasa
kupangwa upya kama ilivyotakiwa miaka mingi iliyopita. Hivi sasa kuna ushahidi kuwa Misri inaisaidia Israel katika kuitenga Hamas, na kwamba Mubarak hana jingine zaidi ya chuki dhidi ya Jamaa ya Kiislamu (Muslim Brotherhood) pamoja na kutowaamini kabisa waQatar na waSyria, na kuwa ghuba yote ya Uarabuni, pamoja na Qatar wamechoka na uongo wa Irani na wangependa kuiona Irani imetoweka au imenyang’anywa silaha na kwamba kwa siri wangeunga mkono shambulio ldhidi ya Iran kutoka ama kwa Marekani au kwa Israel.

Tofauti kati ya maneno yao na vitendo hatimaye viliwekwa wazi kama
unafiki na undumilakuwili kwa watu wao na kwa dunia.

Nilikwambia (hili jambo) ni tukufu!

Halafu anaongeza:

Kuna nchi mbili ambazo zinaweza kuburudika nazo: Irani na Israel.
Israel hivi sasa inafarijika kwamba ni ukweli unaojulikana kuwa kila mmoja katika kanda anataka Irani ishughulikiwe na wapo upande wao, na kwamba ushirika wa Sunni-Israel hivi sasa umehakikishwa kuwa ni wa kweli na kwamba unawajumuisha wachezaji wote wa kiSunni katika kanda hiyo. Kwa umma wa Israel hii inaeeza kuwapa ahueni, lakini kwa serikali ya Netanyahu, itawaongezea nguvu. Hakuna tena mchuuzi wa vita anayepiga mayowe jangwani; hata maadui wao wa muda mrefu wanaafikiana nao. Na kwa Irani, jambo hili linathibitisha maneno yao kuwa kila mmoja anafanya njama dhidi yake na kwamba wametengwa kutokana na Marekani ovu na vibaraka wake wan chi za Kiarabu, na hivyo kuipa sababu serikali (ya Irani) kuimarisha nguvu zake dhidi ya idadi ya maadui wanaoizunguka ambao wanaendelea kuongezeka, wote (maadui) kutoka nje au ndani. Na kwa siri ndani katika mioyo yao, watakuwa wanafarijika kwa hili: siku zote walitaka kutambulika kama mchezaji mkubwa katika kanda hiyo, na nyaraka hizi zimethibitisha bila ya shaka kuwa ni kweli, (Irani ni mchezaji mkubwa).

Katika Egyptian Chronicles, Zeinobia amepokea nyaraka hizo za siri kwa mshangao:

Nilitarajia iwe kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwani hakuna mmoja aliyesema lolote kuhusu Misri katika siku chache zilizopita kwani wote tulifikiri kuwa mawasiliano ya siri Wikileaks yangezijumuisha GCC, Israel, Uturuki na Irani. Kwa uchache hivi ndivyo tulivyoelewa kutokana na taarifa za habari kuhusu jinsi Marekani ilivyopigwa ngeu katika mahusiano yake na nchi hizo ukiiondoa Irani.

Kadhalika anatarajia kasheshe na anauliza:

Mpaka hivi sasa sielewi ni kwa jinsi gani Julian Assange alivyoyapata nyaraka ¼ milioni za mawasiliano au ni kwa nini anayachapisha ukuzingitia ukweli kuwa amesababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia sio tu kati ya Marekani na mataifa mengine bali pia baina ya mataifa kwa mfano Misri na Qatar kama utakavyoona.

Akiendelea na kwenda kwenye hali ilivyo huko Gaza, Zeinobia anablogu:

Naam, magazeti ya Misri ambayo yalithubutu kuchapisha taarifa kuhusu Wikileaks kama vile Al Masry Al Youm zilionyesha tu sehemu inayohusika na kukataa kwa Misri kuidhibiti gaza baada ya ushindi wa Israel ambao haukutukia kama ishara ya uzalendo wa Mubarak bali pia tukumbuke kitu fulani ambacho maofisa nchini Misri walipinga kukifahamu kabla ya “Operesheni Fua Chuma” katika siku za awali za operesheni ambayo iligeuka na kuwa vita. Ni jambo la kustaajabisha jinsi mbavyo Israel ilijiamini sana katika ushindi wake dhidi ya Hamas!!

Katika makala nyingine, Sandmonkey anachambuamajibu kutoka katika vyombo vya habari vya Kiarabu kuhusiana na mvujo huo. Anaandika:

Nilitania leo kwenye Twita
kwamba naamini inawezekana dunia itakabiliana na suala hili katika njia sawa na ile ambayo watu wa kawaida hukabiliana na aibu inayotokea baada ya ngono ya kushtukiza:
Kila mmoja alipata uroda sipokuwa kuonana wakiwa uchi na hivi sasa wanataka kumaliza haraka aibu ile na kujidai kuwa hakuna lililotokea.Nimekuwa nikifuatilia tovuti za habari siku nzima ili nione ni kwa jinsi gani vyombo tofauti vya habari vya Kiarabu vinavyotaarifu juu ya jambo hili, na kuweka dau kuwa ama watalidharau kabisa au watamakinikia kilichosemwa kwa jina la viongozi wa nchi nyingine za Kiarabu badala ya viongozi wao wenyewe. Inaonekana kuwa wadau wa habari wameamua kuwa hawawezi kuidharau kabisa habari hii, kwa hiyo wamechukua chaguo #2.

Kwenye Twita, watumiaji wametingwa na shughuli ya kutenganisha mawasiliano hayo ya waya na kutoa maoni juu ya maudhui yake kwa kutumia ujumbe wa herufi 140.

Mashambulizi ya maoni kwenye Twita yaliwafanya watumiaji wapendekeze alama (hashtag) mpya ili kujadili nyaraka zinazohusiana na ulimwengu wa Kiarabu. Saudi Essam Al Zamelanatuma ujumbe wa twita::

اقترح احد الاخوة استخدام الهاش تاج التالي للكتابة عن تسريبات الويكي ليكس الأخيرة
Kuna mtu amependekeza tutumie alama ya #wikiarab ili kutuma ujumbe wa twita kuhusu mvujo mpya zaidi wa Wikileaks

Kutoka Bahrain, Waziri wa Mambo ya Nje Khalid Al Khalifaanatania:

Watumiaji wa Twita jihadharini, safisheni makasha yenu ya ujumbe binafsi la sivyo kuna mtu atafungua kwa nguvu na kugawa mawasiliano yako binafsi kwa

Katika ujumbe mwingine wa Twita anaongeza:

The balozi wa Marekani amenitumia barua pepe yenye kichwa “NYARAKA ISIYO YA SIRI..

Mmisri Wael Ghonim anang’aka:

Ikivuja, inamwaga.

Halafu anauliza:

أنا أسال المواطن العربي الغيور على أمته .. هل معقولة يعني نصدق يعني مصدر أخبار اسمه ويكي؟
Ningependa kumuuliza mwananchi wa Uarabuni ambaye anaijali nchi yake, je inawezekana kuamini jambo lolote kwenye tovuti ya habari inayoitwa wiki?

Wakati huo huo, Abdulla Almannai, kutoka Bahrain, anaandika:

Siri nyingine ni bora ziachwe bila kutobolewa!

Ahmed Naguib, kutoka Misri , anaongeza:

Nitatumia muda wangu wangu wa mapumziko ya majira ya baridi kupitia mafaili ya . Hatimaye nimepata kitu cha kuvutia kusoma.

Na Mpalestina Ali Abunimah anaweka kipande kingine katika mchezo:

ni kipande kingine katika mchoro wa ushahidi wa ushirika wa Abbas-Fayed katika mauaji ya Gaza na jinsi walivyofucha ukweli.

Suad Alkhawaja, kutoka Bahrain, anahitimisha:

تسريبات ويكيليس لم تأت بجديد للمواطن أو الحكومات العربية، جميعنا يعرف من على وفاق او خلاف مع من وماسيحدث هو تعميق للشرخ الموجود
Uwekaji wazi wa hivi jkaribuni kabisa wa Wikileaks hauleti jambo lolote jipya kwa serikali za Kiarabu na watu wake. Sote tunajua nani ni rafiki na uhusuani wa akina nani ambao unatetereka na nini kitakachotokea ikiwa mpasuko uliopo utapanuka zaidi.

Halafu anaongeza:

لذلك أعتقد ان هذه التسريبات ستؤثر أكثر على علاقات الحكومات مع بعضها البعض وسياساتها الخارجية أكثر مما ستؤثر على المواطن.
Na hiyo ndiyo sababu inayonifanya nifikiri kuwa mvujo huu utaathiri uhusiano baina ya serikali na sera zao za kigeni, zaidi ya ambavyo itawaathiri wananchi.

Na mwisho, Mmisri Wael anaweka kiungo hiki:

Ili kufuatilia mazungum,zo katika twita, Twitter pitia #wikileaks na #cablegate, ambako watumiaji kutoka dunia nzima wamekuwa wakiongeza senti zao mbili kwenye mjadala.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.