Palestina: Maoni Juu ya Kuzinduliwa Kwa Huduma ya Google.ps

“Kwa miaka kadhaa google imekuwa ikiongeza anwani za sehemu maalum kama vile google.co.uk na google.jo ambazo zinatoa huduma za utafutaji maalum kwa sehemu hizo,” anasema mwanablogu ArabCrunch, alipokuwa akitangaza uamuzi wa Google wa kuongeza anwani maalum ya google.ps katika orodha. Anwani hiyo mpya ya sehemu maalum inakusudia kufanya kazi katika Ukanda wa Magharibi na Gaza, ambako ndiko watoaji uduma za intaneti wanapofanyia kazi.

Wiki iliyopita blogu ya Google Arabia ilitangaza ongezo hilo na sababu zilizopelekea uamuzi huo:

Leo tunaongeza anwani nyingine katika orodha yetu, google.ps. Anwani hii mpya itawapa watumiaji wanaoongea Kiarabu waliopo katika majimbo ya Kipalestina, ambao wanatumia huduma zinazotolewa na watoa huduma za intaneti wa Kipalestina, uwezo wa kutumia Google kwa Kiarabu – na hatimaye, kuzifikia habari zinazolenga zaidi sehemu hiyo. Ukijumuishwa uzinduzi wa google.ps, tutatimiza jumla ya anwani zaidi ya 160 za google duniani.

Katika tamko kwa ArabCrunch, Google pia ilifafanua kwa jinsi gani mabadiliko hayo yataathiri huduma ya maneno ya kutangazia biashara – AdWords:

Kwa kutumia AdWords unaweza kulenga matangazo yako kwa nchi au majimbo, au kwa maeneo maalum pamoja na miji. Mfumo wa AdWords unatumia vigezo kadhaa ili kuamua kulionyesha tangazo lako pamoja na kujumuisha anwani ya Google inayotumiwa (.fr, .de, .kr, na kadhalika.), neno halisi analulitumia mtafutaji wakati wa kutafuta na ikiwezekana, tanweza kufahamu sehemu alipo mtumiaji kutegemeana na anwani ya kiitikadi ya intaneti ( au anwani ya IP). “. Mfumo wa AdWords unatumia vigezo kadhaa ili kuamua kulionyesha tangazo lako pamoja na kujumuisha anwani ya Google inayotumiwa (.Com, .De, .Kr, na kadhalika.), neno halisi analulitumia mtafutaji wakati wa kutafuta na ikiwezekana, tanweza kufahamu sehemu alipo mtumiaji kutegemeana na anwani ya kiitikadi ya intaneti ( au anwani ya IP).

Blogu ya Window into Palestine inaelezea kwamba wapalestina walioko Yerusalem Mashariki hawatakuwa na uwezo wa moja kwa moja kuifikia huduma ya google.ps (zingatia: Mtu yeyote anaweza kuipata anwani ya google.ps kwa kuchapa anwani hiyo moja kwa moja):

Ukiitoa Yerusalem Mashariki, ambayo inaangukiwa kwenye utawala wa Kiisraeli, Wapalestina walioko Ukanda wa Magharibi na Gaza wamekuwa wakiitegemea anwani ya google.jo, anwani ya Jordan, na ile ya Misri www.google.com.eg.

Mtumiaji wa Twita migueldeicaza alionyesha msisimko wake wa ongezo hilo kwenye familia ya Google:

daiski, mtumiaji mwingine wa Twita mwenye makazi huko Qatar, aliishukuru google kwa kufanya hilo:

Google.ps inapatikana kwa Kiingereza na kwa Kiarabu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.