Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma
Baada ya uongozi mpya wa Qatari kutangaza kuwa wafanyakazi 250 watapunguzwa kazi katika mtandao wa habari unaosomwa sana wa IslamOnline (IOL), mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao. Hali ilizidi kuwa mbaya kwa kasi sana pale uongozi ulipotishia kuita vikosi vya usalama ili kuvunjilia mbali mgomo huo baridi, lakini wafanyakazi walithibitisha kwamba walikuwa imara na kuwa wangeendelea na mgomo wao mpaka matakwa yao yatimizwe.
Pengine ni jambo linalostahili kutajwa kwamba huenda mgomo huu ni wa kwanza wa aina yake unaotumia kwa ufanisi na vizuri zaidi njia za kisasa za upashanaji habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.
Nadia El Awady, aliyekuwa mwandishi wa habari wa IOL, alikuwa akifuatilia kwa karibu hali ya mambo na alituma kwenye blogu yake tamko lililotolewa na wafanyakazi wa Islamonline:
Hali imezidi kuwa mbaya ndani ya Makao Makuu ya IOL huko Cairo, baada ya kuwa menejimenti ya Qatari kutuma wanasheria kulishika jengo na mali zake zote pamoja na nyaraka, na kuwachunguza wafanyakazi 250 waliotuma tamko lao kwa Shehe Qaradawy, ambaye ni mwenyekiti wa Bodi, wakilalamikia vitendo visivyo vya haki vilivyofanywa na menejimenti mpya.
Baadhi ya vyanzo vilidokeza kuwa sababu iliyojificha ya kuwachunguza wafanyakazi hawa ni kuwafukuza kazi kisha kuwapiga marufuku kudai haki zao zozote za kifedha.Watu walio vyanzo vya habari na walio na uhakika wa kile wanachokieleza ambao wamo ndani ya taasisi hiyo wanasema kwamba lengo la uchunguzi dhidi ya wafanyakazi ni kuwaondoa mara moja na kuwanyika madai yao mbalimbali ya fedha waliyo nayo.
Kwa upande wake Tadamon Masr alieleza [Ar] kwamba mgogoro huo huenda umetokana na lengo la uongozi mpya wa Qatari kutaka kuhamisha makao makuu ya IOL kutoka Cairo kwenda Doha. AbdelMoniem alikuwa na wasiwasi [Ar] na alijiuliza kama ilikuwa ni njama za wenye siasa kali kutaka kunyamazisha sauti zinazotaka maelewano zaidi zilizo katika tovuti kama ile ya IslamOnline.
Zeinobia alitoa maoni yanayotaka kufanana na hayo kwa AbdelMoniem akisema:
Inasemekana kwamba Uongozi mpya wa Qatari ni ule wenye msimamo wa kihafidhina unaoamini kwamba uendeshaji wa tovuti hiyo hauna budi kushikilia mitazamo ya kidini yenye msimamo wa kihafidhina na kuondolea mbali vipengele vingine.
Kupitia Twita, mwandishi mwingine wa habari wa zamani wa IOL, Mohammed, alikuja na taarifa inayosema:
@MohammedY: Kwa waandishi walio Misri na ulimwengu wa Kiarabu: Waandishi wa habari wanaofanya kazi katika Islamonline wanatendewa vibaya na uongozi wao mpya ili kuwanyamazisha kutoa matamko dhidi ya vitendo vibaya vya uendeshaji kampuni.
@MohammedY: Kwa hiyo, pale wafanyakazi wanapotia saini maelezo kuhusu matatizo yanayowakabii, basi uongozi unawaweka wafanyakazi chini ya uchunguzi. Hivi jambo hili limesababishwa nini hapo Islamonline?
Abdullah El Shamy na Muhammad Ghafari, ambao ni miongoni mwa wanaogoma, walikuwa wakishughulikia taarifa zinazoingia moja kwa moja, kwa hiyo walikuwa wakituma taarifa hizo moja kwa moja kwenye akaunti zao za Twita na kutuma picha za eneo hilo la kazi.
@Ghafari: Kwa wale wanaoguswa na hali hii, ili kupata taarifa mpya kuhusu mgomo wa wafanyakazi wa Islamonline, tafadhali bofya hapa: http://www.ustream.tv/channel/iol-on-air
Ghafari hakusahau kueleza jinsi gani wanawake wanavyoshiriki katika kuupa mgomo huo nguvu:
@Ghafari
#IslamOnline #mgomo #wanawake
Hakuna sababu ya kueleza jinsi wanawake wanavyosaidia kuutia nguvu mgomo huu, zaidi ya hilo wanatunga nyimbo za hamasa pia!
Nadia El Awady vilevile alikuwa akiwapa taarifa rafiki zake kupitia Twita karibu kila dakika, alieleza:
@NadiaE: Mfanyakazi wa kike pale Islamonline analeza nia yake ya kulala ofisini kutumia begi la kulalia ili kuendeleza mgomo.
@NadiaE: #mfanyakazi wa islamonline, @mos3abof, anatoa wito wa wafuatiliaji kutoa uungaji mkono kwa yale yanayochapishwa na tovuti [mipango ya Bodi ya Qatar na uchukuaji wake haileweki]
Mwanablogu wa Misri, Ahmed Shokeir, alitoa maoni kwamba karibu kila mtu aliona, akielezea kuhusu zana za vyombo vya habari vya kisasa, jinsi vinavyotumiwa tofauti katika wakati huu:
@Shokeir
Nafikiri kuwa mgomo wa Islamonline huenda ukawa wa kwanza kutumwa moja kwa moja mtandaoni. Naamini njia hii itakuja kuwa yenye ufanisi na kuwa zana itakayotumiwa sana katika siku za hivi karibuni.
Pia inafaa kutaja kwamba kuna uvumi kwenye Twita kwamba huenda El Qaradawi akajiuzulu nafasi yake, hiyo ni kwa mujibu wa Mohammed:
@MohammedY : #Menejimenti ya IslamOnline huko Qatar imekuwa ikikataa kupokea simu kutoka kwa Al-Qaradawi kwa sababu inamtuhumu kwamba alitaka kujiunga upande wa wafanyakazi (kupitia Fathi katika IOL)
Na hiyo ilipata uungaji mkono kutoka kwa mwanaTwita mwingine, Nadia:
@NadiaE: Motaz Al-Khateeb, ambaye ni mtayarishaji wa kipindi cha televisheni cha Shehe Al-Qaradawi's katika Aljazeera alizungumza na katibu muhtasi wa Shehe huyo akimkariri akisema kuwa bado anafikiria kujiuzuru.
Kabla ya kwenda kulala, Ghafari alihitimisha utoaji taarifa zake za kila mara kwa kusema kwamba hawatasimamisha mgomo wao mpaka matakwa yao yote yatimizwe:
@Ghafari: #Mgomo wa wafanyakazi wa IslamOnline utaendelea mpaka asubuhi, yaani mpaka uamuzi ufanyike unaothibitisha kwamba haki zetu zipo palepale.
Picha zaidi zipo hapa.
Mada za Habari

Anza mazungumzo
Kumbukumbu za Mwezi
- Disemba 2020 1 ujumbe
- Oktoba 2020 4 jumbe
- Septemba 2020 8 jumbe
- Agosti 2020 2 jumbe
- Julai 2020 1 ujumbe
- Juni 2020 1 ujumbe
- Aprili 2020 1 ujumbe
- Februari 2020 2 jumbe
- Oktoba 2019 2 jumbe
- Agosti 2019 2 jumbe
- Juni 2019 3 jumbe
- Mei 2019 10 jumbe
- Aprili 2019 14 jumbe
- Machi 2019 10 jumbe
- Februari 2019 11 jumbe
- Januari 2019 2 jumbe
- Disemba 2018 2 jumbe
- Novemba 2018 1 ujumbe
- Oktoba 2018 1 ujumbe
- Agosti 2018 3 jumbe
- Julai 2018 11 jumbe
- Juni 2018 12 jumbe
- Mei 2018 12 jumbe
- Aprili 2018 6 jumbe
- Januari 2018 2 jumbe
- Disemba 2017 3 jumbe
- Septemba 2017 1 ujumbe
- Agosti 2017 8 jumbe
- Julai 2017 8 jumbe
- Juni 2017 5 jumbe
- Mei 2017 5 jumbe
- Aprili 2017 9 jumbe
- Machi 2017 15 jumbe
- Februari 2017 8 jumbe
- Januari 2017 6 jumbe
- Disemba 2016 2 jumbe
- Novemba 2016 12 jumbe
- Oktoba 2016 16 jumbe
- Septemba 2016 7 jumbe
- Agosti 2016 5 jumbe
- Julai 2016 15 jumbe
- Juni 2016 15 jumbe
- Mei 2016 8 jumbe
- Aprili 2016 8 jumbe
- Machi 2016 10 jumbe
- Februari 2016 8 jumbe
- Januari 2016 1 ujumbe
- Disemba 2015 1 ujumbe
- Novemba 2015 10 jumbe
- Oktoba 2015 7 jumbe
- Septemba 2015 4 jumbe
- Agosti 2015 4 jumbe
- Julai 2015 2 jumbe
- Juni 2015 15 jumbe
- Mei 2015 12 jumbe
- Aprili 2015 30 jumbe
- Machi 2015 3 jumbe
- Februari 2015 25 jumbe
- Januari 2015 5 jumbe
- Novemba 2014 9 jumbe
- Oktoba 2014 21 jumbe
- Septemba 2014 32 jumbe
- Agosti 2014 2 jumbe
- Julai 2014 51 jumbe
- Juni 2014 24 jumbe
- Mei 2014 57 jumbe
- Aprili 2014 60 jumbe
- Machi 2014 67 jumbe
- Februari 2014 43 jumbe
- Januari 2014 12 jumbe
- Disemba 2013 29 jumbe
- Novemba 2013 50 jumbe
- Oktoba 2013 32 jumbe
- Septemba 2013 25 jumbe
- Agosti 2013 9 jumbe
- Julai 2013 34 jumbe
- Juni 2013 33 jumbe
- Mei 2013 28 jumbe
- Aprili 2013 18 jumbe
- Machi 2013 3 jumbe
- Februari 2013 12 jumbe
- Januari 2013 20 jumbe
- Disemba 2012 16 jumbe
- Novemba 2012 8 jumbe
- Oktoba 2012 21 jumbe
- Septemba 2012 13 jumbe
- Agosti 2012 16 jumbe
- Julai 2012 26 jumbe
- Juni 2012 21 jumbe
- Mei 2012 3 jumbe
- Aprili 2012 19 jumbe
- Machi 2012 10 jumbe
- Februari 2012 2 jumbe
- Januari 2012 10 jumbe
- Disemba 2011 16 jumbe
- Mei 2011 10 jumbe
- Aprili 2011 22 jumbe
- Februari 2011 4 jumbe
- Januari 2011 10 jumbe
- Disemba 2010 4 jumbe
- Novemba 2010 7 jumbe
- Oktoba 2010 6 jumbe
- Septemba 2010 10 jumbe
- Agosti 2010 13 jumbe
- Julai 2010 20 jumbe
- Mei 2010 2 jumbe
- Aprili 2010 16 jumbe
- Machi 2010 22 jumbe
- Februari 2010 22 jumbe
- Januari 2010 41 jumbe
- Disemba 2009 47 jumbe
- Novemba 2009 56 jumbe
- Oktoba 2009 29 jumbe
- Septemba 2009 3 jumbe
- Agosti 2009 6 jumbe
- Julai 2009 10 jumbe
- Juni 2009 11 jumbe
- Mei 2009 5 jumbe
- Aprili 2009 7 jumbe
- Machi 2009 3 jumbe
- Februari 2009 18 jumbe
- Januari 2009 12 jumbe
- Novemba 2008 3 jumbe
- Oktoba 2008 9 jumbe
- Septemba 2008 12 jumbe
- Agosti 2008 9 jumbe