Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

GV Face: Wanawake Nchi Saudi Arabia Wanuia Kuendesha

Mnamo Octoba 26, 2013 maelfu yaa wanawake wa ki-Saudi wameapa kuvunja amri ya Ufalme kuwazuia wanawake kuendesha magari.

Katika toleo la GV Face wiki hii, tunakutana na mwanablogu wa Jeddah na mwandishi  Tamador Alyami, anayeunga mkono kampeni ya #WanawakeWataendesha. Tunaungana na Hadeel Mohammed, Mwandishi wetu wa Saudia anayeishi Dammam na Mhariri wetu wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Amira Al Hussaini. 

Tumezungumzia kampeni hiyo, maisha ya wanawake nchini Saudi, na jinsi wanaharakati walivyowachukulia wapinzani wa kampeni hiyo kama alivyofanya mhubiri mmoja siku za hivi karibuni aliposema, “tumegundua kuwa wale [wanawake] wanaoendesha magari wanajifungua watoto wenye vilema vya aina mbalimbali.”

GV Face inaandaliwa na Mhariri Mtendaji Solana Larsen na Mhariri Msaidizi Sahar Habib Ghazi.

Pia unaweza kusoma:

Septemba 2013 Imamu wa Saudi aeleza Sayansi mpya ya sababu ya wanawake kuzuiwa kuendesha
Sep 2013 Octoba 26: Siku ya kuvunja amri ya Saudi kuwazuia wanawake kuendesha
Octoba 2012 Saudi Arabia: Kampeni ya Wanawake Kuendesha Yapamba moto; Yalaumu sera za serikali
Novemba 2011 Saudi Arabia: Hasira dhidi ya Makofi 10 kwa dereva mwanamke
Juni 2011 Saudi Arabia: Wanawake kwenye Usukani 
Mei 2011 Saudi Arabia: Wanawake Wawekwa kizuizini kwa Kuendesha
Mei 2011 Saudi Arabia: Mwanamke Apingana na sheria kwa Kuendesha mjini Jeddah

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.