Blogu na Uhuru wa Saudi Arabia

Saudi Arabia huadhimisha Sikukuu ya Kitaifa ya Uhuru tarehe 23, Septemba. Wakati kwa kawaida hii huwa ni siku ya watu kusherehekea ufalme wa nchi hiyo kuliko nchi yenyewe, miaka miwili iliyopita imekuwa tofauti kidogo. Wa-Saudi, kwa kutumia mitandao ya kijamii na blogu, wamekuwa na nafasi ya kujieleza kwa uhuru -wakiblogu matumaini yao kwa taifa linaloheshimu na kuthamini watu wake na matarajio yao.

Mwandishi na Daktari, Bader Al-Ibrahim aliandika:

Sherehe hizo za kitaifa hazitoshi kuhamasisha hisia za utaifa wakati kumbukumbu muhimu hazipo, utambulisho wa pamoja na taasisi zinazofadhili uraia hazipo.

Mtetezi wa Haki za Raia wa Jordan, Fadi Al-Qadi, alitwiti:

Abdullah Al-Hamed na wafanyakazi wenzake katika shirika la ACPRA wanatumia siku ya maadhimisho ya uhuru wa Saudia wakiwa gerezani. Mojawapo ya mashitaka ni “kukwaza maendeleo” wakati mtawala anashitakiwa kwa “kukwaza utu”.

Mwandishi Abdullah Al-Malki alitwiti:

Siku yetu ya Uhuru, tunakumbuka ACPRA, Al-Hamed, Al-Qahtani, Al-Bjadi, Tawfeeq Al-Amer, Al-Mnasif na Jeddah ambao ni wanaharakati wa mabadiliko pamoja na wengine wote waliopigana kwa ajili nchi hii kubadilika na kufanikiwa. Amani iwe kwenu.

Wakati Eman Al-Qaffas anabaini:

Yeyote anayedhani kuipenda nchi yake maana yake ni kuipenda serikali yako ni mtu asiyeipenda nchi.

Na Rehab Al-Hamdan anaongeza:

Watu wameelimika sasa. Hawadanganyiki kwa maneno matupu tena.

Wanablogu wengi walitoa maoni tofauti kuhusu siku hiyo ya uhuru.

Sultan Al-Amer, mwandishi na mwanablogu, aliandika kwa mtazamo wa kizalendo wa Kiarabu:

إن تاريخنا “القومي” كعرب ليس محصورا بحدود الدولة السعودية وتاريخها.
إن تاريخنا القومي هو تاريخ الشعوب الممتدة من الخليج إلى المحيط وليس تاريخ الأنظمة فقط.
وإن معنى “الوطن” لا يمكن الاحتفال به قبل تجسيده كحقوق سياسية وحريات.
وإن الأنظمة الحاكمة تستطيع بسهولة أن تبني شرعية متينة إذا تحولت إلى أنظمة مدافعة ومنحازة لقضايا أمتها ومستجيبة لآمالها وتطلعاتها.

Historia ya taifa letu kama Waarabu haijafungwa na mipaka na historia ya Saudi Arabia. Historia ya taifa letu ni kwamba watu wanaoishi kati ya Ghuba na bahari [Atlantic] na sio historia ya tawala mbalimbali tu. Maana ya “nchi” haiwezi kusherehekewa mpaka iwe imefungamanishwa na haki za kisiasa na uhuru. Tawala zilizomadarakani zinaweza kujenga uhalali kama zitaanza kutetea na kuungana na misimamo ya watu wake na kujibu matumaini yao na ndoto walizonazo.

Wakati mwandishi mwingine wa habari mzalenzo, Abdullah Al-Duhailan, aliblogu akikosoa aina mbili za watu. Moja ni tabaka la wasomi wanaokataa kusherehekea siku hiyo mpaka matakwa yote ya kisiasa na kiraia yatekelezwe. Wengine ni idadi kubwa ya watu wanaoshabikia propaganda za vyombo vya habari na kujikuta wakisherehekea watu fulani badala ya nchi yenyewe.
Familia za watu waliowekwa kizuizini wanaiona siku hii kama nafasi ya kukuza uelewa kuhusu malengo yao. Vikundi vya utetezi visivyofahamika majina @e3teqal [vimekamatwa] na @almonaseron [wafuasi wao] kutoa mwito wa maandamano madogo yaliyofanyika zaidi mjini Buraiydah.

From the women's protest in Buraydah

Kutoka kwenye maandamano ya wanawake mjini Buraiydah

Matairi yalichomwa katika maeneo yasiyo ya makazi huku kukiwa na mabango karibu yanayotaka watu waliokamatwa kuachiwa huru. Na mkutano ulifanyika mjini Buraiydah ambapo ndugu za watu waliokamatwa walikutana na kujadili njia zinazoweza kufanyika ili kuwasaidia wafungwa hao. Familia ya Abdulkarim Al-Khuder, mwanachama wa ACPRA aliyefungwa, walikuwa miongoni mwa familia chache zilifanya nyumba zao zizingirwe na magari ya polisi kwa kosa la kutundika picha za wapendwa wao waliowekwa kizuizini.

Mahdi Al-Zahir, mwanaharakati kutoka Qatif, alitwiti:

Ningependa kusherehekea siku ya Uhuru. Lakini kaka yangu yuko kizuizini, mpwa wangu naye yuko kizuizini, rafiki yangu naye yuko kizuizini, hata jirani yangu naye yuko kizuizini.

Na Shirika la Haki za Kiraia na Kisiasa la Kisaudi (ACPRA) lilichapisha tamko [ar] lililotaka kuachiwa kwa wafungwa wote wa dhamira na pia kuwepo kwa mjadala wa kitaifa wenye usawa kati ya serikali kwa upande mmoja na wawakilishi wa wananchi waliochaguliwa kwa kura kwa upande wa pili.

وإن هذا الشعب كباقي الشعوب فيه من هو مستعد للنضال السلمي للوصول للحقوق المشروعة والسجون لن تكفي فكلما سجن فوج جاء فوج آخر … فأما الحكومات وأحيانا الدول تتغير وتبقى الشعوب.

Kuna watu katika taifa hili, kama wengineo, waliotayari kuendelea kupambana kwa amani mpaka madai yao ya haki yatakaposikilizwa na kutekelezwa. Magereza hayatatosha. Kila kundi linapowekwa kizuizini, kikundi kingine kinaingia uwanjani…Serikali, na wakati mwingine nchi, hubadilika, lakini watu wake hubaki.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.