Makala za Global Voices Zilizosomwa Zaidi mwaka 2011

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Global Voices mwaka 2011.

Orodha yetu ya makala 20 bora zilizosomwa zaidi kwenye tovuti ya Global Voices kwa mwaka 2011 ni pamoja na nne kutoka Japan, tatu kutoka Misri, na mbili kutoka Ufilipino. Lakini habari moja tu inahusu yule mamba mkubwa!

Umekuwa mwaka wa ajabu kwa vyombo vya kiraia duniani kote ambavyo viliweza kufika mbali zaidi na kutambuliwa, na hiyo ina maana Global Voices haijabaki kuwa sauti pweke ya vyombo vya habari vya kiraia linapokuja suala la twita zinazotuma taarifa na posti za kwenye blogu. Bado, hata hivyo pale ambapo shauku kwa vyombo vikuu vya habari ikindelea kupungua, sisi ndio tunaojibidiisha kuendelea kuweka kumbukumbu ya kile ambacho wanablogu wadogo popote pale walipo wanataka dunia ikifahamu.

Self Defence Forces arrive at the scene of the tsunami in Japan. Image by cosmobot, copyright Demotix (13/03/11).

Kikosi cha Ulinzi kikiwasili kwenye eneo lililokubwa na Tsunami nchini Japan. Picha ya cosmobot, haki miliki Demotix (13/03/11).

Baadhi ya nyakati tulizojivunia zaidi mwaka 2011 hazitaweza kuakisiwa katika orodha ya makala bora 20 kama hii iliyopo hapa chini. Mwaka huu idadi ya waandishi na wafasiri hai ilizidi 500 wa lugha na nchi zisizo na idadi, na tulichapisha zaidi ya makala ndefu 2,600 na zile fupi fupi zipatazo 6,300 kwa Kiingereza peke yake.
Haikwepeki kwamba, habari nyingi ambazo huwa hazipati usomaji mkubwa kuliko zinavyostahili zinatoka kwenye nchi ambazo hupuuzwa na vyombo vikuu vya habari. Uhabarishwaji wa aina yake kuanzia Africa, Caucasus, Macedonia, the Mtandao wa lugha ya Kirusi, , Marekani ya Kusini na haki za wenyeji ni baadhi tu ya dondoo za habari hizi. Angalia mapitio ya kimaeneo kwa mwaka 2011 yaliyofanywa na wahariri na waandishi ili kupata taswira ya haraka ya kile ambacho huenda ulikikosa.

Timu yetu ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini inastahili kutambuliwa kwa uzito wa pekee mwaka huu. Wakati wote wa maandamano, kukatwa kwa mawasiliano, vitisho nk waliweza kujipiga moyo konde na kuendelea kuandika. Picha za mauaji bado zinashika kasi, lakini waandishi wetu wanatafuta sauti zinazojenga na mitazamo inayofaa kwa majadiliano. Mara nyingi wametushirikisha habari za ucheshi kutoka maeneo yao na mikhtadha ambayo huwa ni vigumu kuielewa ukiwa nchi nyingine bila miongozo yao.

Huenda ni kwa mara ya kwanza kabisa, China haionekani kwenye orodha yetu ya makala 20 bora zaidi kwa mwaka huu. Hizi pengine ni nyakati ngumu kublogu kuhusu mada tete –jambo ambalo kwa bahati mbaya sana waandishi wengi wa Global Voices katika nchi nyingine nyingi wanakabiliana nalo. Hali hii ndiyo inayozifanya habari zinazokuja kutoka mahali popote ambapo haki ya kujieleza imebanwa kuwa na uthamani wa pekee.

Makala za Global Voices Zilizosomwa Zaidi mwaka 2011

 1. Misri: Usiku waisha, Baada ya Mchana wa Ghadhabu
 2. Japan: Tunashindwa na Kampuni ya Apple, na hizi ni sababu
 3. Kuchora ramani ya Janga la mafuriko ya Thailand (na (and also hii hapa pia)
 4. Syria: “Msichana msagaji akamatwa mjini Damascus (na hii hapa pia)
 5. Ufilipino: Mjadala juu ya Mswada wa Talaka
 6. Japan: Kutuma ujumbe wa Twita kutoka Fukushima
 7. Ufilipino: Lolong, Mamba mkubwa zaidi Duniani
 8. India: Mtoto wa Aishwarya Rai na Wazimu wa Vyombo vya Habari
 9. Misri: Mtetezi wa Haki za wanawake achapisha picha ya uchi “kuonyesha uhuru wake”
 10. Japan: Kuhusu Majanga ya asili na Miujiza, Tafakari Binafsi
 11. Serbia: Miitikio kuhusu habari ya Wanajeshi wa Ki-Serbia wanaokodiwa kupigana nchini Libya
 12. Tetemeko kubwa zaidi katika Historia ya matetemeko nchini Japani
 13. Bendera mpya ya Myanmar na Jina Jipya
 14. Mexico: Hofu, Mashaka na Wasiwasi juu ya alama #OpCartel ya Mtu Asiyetumia Jina lake
 15. Mwandishi wa Nyimbo wa Ajentina Facundo Cabral Auawa huko Guatemala
 16. Afrika, Ufaransa: Nafissatou Diallo ni nani? Mwathirika au Haramia?
 17. Japan: Hofu mjini Fukushima
 18. Libya: Je, Khamis Gaddafi Amekufa kweli?
 19. Misri: Mapinduzi ya KFC
 20. Uhispania: Maelfu ya ya watu waingia mitaani

Kurasa zetu za:Habari Maalum zilizotembelewa Zaidi zilikuwa:

 1. Mapinduzi ya Misri 2011
 2. Tetemeko la Japan 2011
 3. Maandamano ya Bahrai 2011
 4. Maasi ya Libya 2011
 5. Mapinduzi ya Tunisia 2011

Mwaka 2011 dunia imejifunza zaidi juu ya nguvu ya mabadiliko iliyo kwenye vyombo vya habari za kiraia vya mtandaoni. Tunaamini njia bora zaidi ya kuunga mkono sauti hizi zinazochipukia kwa kiwango cha dunia ni kusikiza. Asante kwa kusoma tovuti ya Global Voices! Na tafadhali fikiria kuunga mkono kazi yetu kwamchango wako

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Global Voices mwaka 2011.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

 • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.