Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusu Maandamano nchini Bahrain 2011/2012.

Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamra shamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo.

Katika kuuanza mwaka mpya, Vyombo vya Habari nchini Bahrain vilitoa tamko la kusherehekea mafanikio ya mwaka uliopita linalosema:

Dola iliyoweka historia ya taswira ya kung’ara ya kutokuwa na chembe ya doa katika haki za binadamu inaendelea kuwa imara na isiyotikiswa kwa dhahania za uongo na zisizo na maana zinazosambazwa kwa uhasama kupitia vipaza sauti wakati wa dhifa mbalimbali za kitaifa.

Wakati huo huo, watu wa Bahrain walishuhudia siku ya kwanza ya mwaka mpya kwa changamoto mbalimbali. Kwa bahati nzuri, baadhi yao taarifa zao zilishakusanywa na watumiaji wa mtandao wa intaneti na hivyo kutumia tovuti kuuonesha ulimwengu “kumbukumbu nzuri ya usawa wa haki za binadamu usio na chembe ya doa” na “madai ya uongo” yanayosemwa na serikali.

Mwanablogu @chanadbh alitwiti kiungo cha video na kuambatanisha maoni yanayokinzana moja kwa moja na kauli za serikali:

@chanadbh: #Polisi wa Bahrain washambulia kwa matofali gari lililokuwa limeegeshwa, lengo lilikuwa ni kujilinda lakini http://www.youtube.com/watch?v=HraRTyuvpOY …

 

Video inaonesha polisi akifanya vurugu kwa kulirushia tofali gari lililokuwa limeegeshwa katika kijiji cha Jurdab.

Daktari Abdulhadi Khalaf, mwenye elimu ya uzamivu, ambaye siku za hivi karibuni alivuliwa uraia wa Bahrain, alipakia video nyingine na alichangia kama ifuatavyo:

بلطجية الداخلية تحاول كسرأحد أالأبواب****ألهذا السبب تكثر الإصابات بين البلطجية؟

@Abdulhadikhalaf: Wizara ya mambo ya ndani iliyo katili inajaribu kuvunja mlango**** ndio maana kuna idadi kubwa ya majeruhi miongoni mwa waonevu?

@AHRAR_MURQOBAN, Ukurasa wa Twita uliotolewa maalum kwa ajili ya kupakia habari za kijiji kilichopo Sitra, ilipakia video inayoonesha matukio aina hii. Katika video hii, maafisa wa polisi wanaonekana wakiongea katika lugha ya Urdu:

فيديو : المرتزقة وهم يخططون لأقتحام منزل – سترة – ميادين اللؤلؤhttp://youtu.be/sqQp3BJpy7s http://fb.me/2rcPUyfkP

@AHRAR_MURQOBAN: Maafisa wa polisi wanaoweka maslahi yao mbele wakijiandaa kufanya shambulizi la kushitukiza katika nyumba huko Sitra

Hali ya kutokuonekana vizuri siyo ya ukungu, ni matokeo ya mabomu ya kutoa machozi kutupwa mara kwa mara vijijini.

Mwanharakati wa kutetea haki za binadamu ajulikaye kwa jina la Maryam Alkhawaja pia alipakia video inayowaonesha maafisa wa polisi wakiwanyunyizia wanawake pilipili bila ya kujua haswa lengo ni lipi. Taarifa zilisema:

@MARYAMALKHAWAJA: Maafisa wa polisi wakiwanyunyizia wanawake pilipili usoni mwao bila sababu@: 1-1-13 http://youtu.be/0wokYBRrxpM

Mtumiaji wa Twita, Mahmood Alshaikh alitwiti tena video nyingine inayoonesha kuwa hakuna jambo zuri linalofanyika bila kufuatiwa na adhabu nchini Bahrain:

#البحرين – سترة: مطاردة الشباب بعد محاولتهم انقاذ عائلة مختنقة 1 1 2013:http://youtu.be/0sTkwcQxxD0

@M_Alshaikh: Bahrain – Sitra [Kisiwa kilichopo upande wa mashariki mwa Bahrain] : Vijana wakifukuzwa baada ya kujaribu kuwaokoa watu wa familia moja waliokuwa wamekosa hewa 2013 1 1

Mwaka uliopita, Wanafizikia wa Haki za Binadamu, walieleza katika [@P4HR] taarifa yao kuwa:

Waandamanaji waliojeruhiwa ambao wachunguzi wa Wanafizikia wa Haki za Binadamu (PHR) waliowafanyia uchunguzi waligundua kuwa walikuwa wanasumbuliwa na majera yaliyotokana na kupigwa, mipasuko ya ngozi vichwani, kukosa sehemu fulani za miili yao, mikono na miguu, hii inatokana na maguruneti ya chuma wanayotupiwa katika umbali mfupi na maafisa wa polisi na kuwalipukia.

Mfano halisi wa lizungumzwalo hapo juu liliwekwa katika ukurasa wa twita na 14 Feb Media Network, mtandao uliojishughulisha zaidi na kusambaza habari za Bahrain siku ya mwaka mpya:

#المنامة: طلقة مباشرة تصيب أحد الثوار #ميادين_اللؤلؤ 01 01 2013:http://youtu.be/_I-HhhSz87s

@Feb14Media: Bahrain | Manama : a straight shot hits a protester

Video nyingine ifananayo na iliyotangulia lakini yenye kuonekana vizuri zaidi ilipakiwa mapema na mtandao huo:

#سترة #سفالة : طلقة مباشرة تصيب رأس أحد المتظاهرين 1/1/2013#البحرين

@Feb14Media:
Sitra – Sufala [Kijiji katika kisia cha Sitra] : Risasi iliyomlenga moja kwa moja muandamanaji1/1/2013

Maafisa wa polisi ni lazima wafundishwe kuwa hawapaswi kunyanyasa, na hata unyanyasaji wa rika kama ilivyotokea kwa motto huyu mdogo ( maoni yanasema mvulana huyu alikuwa na umri wa miaka minne) ambaye hakuweza kuepushwa kutoka kwenye furaha ya kusherehekea mwaka mpya-kwa mfumo wa serikali ya Bahrain. Moawen anafafanua:

@Moawen: Polisi wenye vurugu wakiliwasha moshi wa kutoa machozi yaliyomzingira mototo mdogo http://youtu.be/4eQmT_M7_is ni muendelezo wa uvunjaji wa haki za watoto:

Mwandishi wa habari, Dima Khatib naye alipakia picha iliyoonesha vizuri zaidi tukio hili:

@Dima_Khatib: Bahrain… tena ! RT @mohmdashoor: dalili yoyote kuwa uliona hili tokea jana? Mototo wa miaka minne kuwashiwa moshi wa kutoa machozi pic.twitter.com/DW7lD5Gl

Picha inayoonesha jinsi motto mdogo alivyowashiwa moshi wa kutoa machozi, picha iliwekwa na @14febonline

Ikitumia ukurasa wake wa Twita, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa mrejesho rasmi wa matukio yaliyotokea siku ya mwaka mpya, ilisema:

@moi_bahrain: Msaidizi wa Naibu Katibu wa masuala ya sheriaAssistant Undersecretary of Legal Affairs: aliziambia tovuti mbalimbali kuwa kuitisha mikutano saa tisa na nusu usiku siku ya jumanne katika maeneo mbalimbali ya Bahrain ni kinyume na sheria

 

@moi_bahrain: Mikutano ya wazi na washenzi; Haki ya kujieleza inalindwa na katiba pamoja na washenzi; wale wanaotaka kufaidika kutokana na sheria hii wanapaswa kufuata sheria.

@moi_bahrain: Ulinzi na taratibu za sheria zitachukua mkondo wake dhidi ya wavunja sheria ili kuimarisha usalama

Mwisho wa maelezo yaliyotajwa mwanzoni mwa makala hii, Wakala wa Habari wa Bahrain alieleza:

Kwa kujiamini na kwa uhakika, Dola ya Bahrain inapiga hatua kuelekea katika mafanikio makubwa kabisa kwa mwaka 2013.

Binafisi nina matumaini kuwa, hili litafanikiwa.

Makala hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusiana na maandamano nchini Bahrain 2011/2012.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.