Bahrain: ‘Kususia michezo ya Olimpiki’

Makala haya ni sehemu ya makala zetu maalum michezo ya Olimpiki London 2012 na Maandamano Bahrain 2011/12

Mwana wa mfalme wa Bahrain, Nasser Bin Hamad Al Khalifa ni mwanamume aliyemstari wa mbele kwenye michezo Bahareni; hakuchaguliwa kidemokrasia bali aliteuliwa kama wengine kwenye familia yao, walioko madarakani.

Kijana huyu alipata umaarufu  baada ya mieleka mnano Februari 14 mwaka jana, ilipodaiwa kuwa aliwatesa wanamichezo wengi  wa Bahrain, waliojiunga na ranki za waandamanaji katika maandamano makubwa wakidai mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Nasser alitumia twita wakati wa myanyuko, akitwiti kwa kutumia jina lake halisi, akitishia kulipiza kwa wale wanaopinga utawala.  Wakati kampeni zilipoanza kutoa wito wa kuondolewa kwake kwenye mashindano ya Olimpiki jijini London, alifuta twiti zake.

Wafuasi 66,254 na twiti sifuri. Twiti zote zilifutwa mwezi jana wakati mkuu huyo alipoogopa kupigwa marufuku kutoka London kwa madai ya mateso.

Novemba mwaka uliopita, ESPN ilizua rabsha kwa kupitia upya swala la kukamatwa na kuwateza wanamichezo wa Bahrain. katika kanda ya video, wanamichezo hao walilalamika kuhusu kupoteza nafasi zao kwenye timu zao, kukamatwa kwao, kufedheheshwa kwa ukali kama wasaliti, kukana imani yao ya Shia, na kuteswa na mkuu huyo mwenyewe.

Akamatwe mtesaji huyo

Katika sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki, mwanaharakati Jamila Hanan (@JamilaHanan) alitwiti picha hii ya Nasser Bin Hamad akiwa na Waziri wa kigeni wa Bahrain:

@JamilaHanan: The guy front right with the red tie. VIP at the #Olympics. He's a torturer. Of athletes. Prince Nasser of #Bahrain.

@JamilaHanan: Mtu aliye mbele upande wa kulia na tai nyekundu. Mtu muhimu sana katika #michezo ya Olimpiki. Mtesaji wa wanariadha. Mkuu Nasser wa #Bahrain.

Bahrainu Citizen ilitoa maoni:

@Bahrainycitizen: Nasser Bin Hamad alihusika yeye mwenyewe kuwatesa waliokamatwa na hivi leo ameruhusiwa kuhudhuria sherehe ya ufunguzi #Michezo ya Olimpiki

Tweep Kenneth Lipp alibainisha:

@kennethlipp: Naskia familia ya kifalme ya Bahrain ni wahudumu katika michezo ya Olimpiki, nchi yoyote yenye ustaarabu ingewakamata mara moja.

Mwanaharakati wa Iraqi Khalid Ibrahim alitwiti:

@khalidibrahim12: Bila shaka kumwalika mtesaji # Bahrain kupitia serikali ya # Uingereza ni kupingana na maadili na kanuni ambapo zimetumika kuanzisha #michezo ya Olimpiki.

Katika kurudi, mwanaharakati wa haki za binadamu Maryam Alkhawaja (binti wa takwimu jela upinzani Abdulhadi Alkhawaja) alitoa wito kwa ajili ya kugomea michezo ya Olimpiki:

@MARYAMALKHAWAJA: RT kama unakubali: Ninagomea#michezo ya Olimpiki2012 kwa sababu licha ya kutolewa ushahidi, #Uingereza na#Olimpiki iliwaruhusu watesaji wanaodaiwa kuhudhuria. 

Wanariadha hawa hawatuwakilishi sisi

Only three of Bahrain Olympic athletes are born to Bahraini parents. Image by @Ali_Milanello on Twitter.

Ni wanariadha watatu tu wa Bahrain ambao wazazi wao ni wa Bahrain. Picha kwa niaba ya @Ali_Milanello kwenye twita.

Sababu nyingine  ya wito wa kugomea michezo ya olimpiki ni baadhi ya wanariadha umenawiri katika kikosi. Wakati wa sherehe za ufunguzi, Wa-Bahareni wengi walitwiti  kwamba hao wanariadha wameomba uraia na hawana uhusiano wowote na Bahrain isipokuwa kuwakilisha nchi katika michezo kwa kulipwa fedha tu kwa ajili hiyo.

Suala hili ni tata katika Bahrain ukizingatia jinsi wale wanariadha huja kuchukua nafasi  “zisizohitajika” wanariadha Bahraini na kwa sababu ya ‘kisiasa uraia’ ambayo imekuwa kwa muda mrefu inatekelezwa na serikali ya kupanua wigo wake wa wafuasi na kuwaajiri katika vikosi vya usalama.

Katika Maoni yake, Bahraini Ala'a Al Shebabi Alitwiti:

@alaashehabi: Hakuna furaha tunapotazama # Bahrain # michezo ya Olimpiki ya timu na moja inayoonekana kuwa ya Bahraini mioyo yetu inazama zaidi ya wanariadha 20 walioswekwa jela.

Na Kejeli, Mwanablogu wa Bahraini Amira Al Hussaini  aliandika:

@JustAmira: Karibu wachezaji wetu wote #Bahrain #timu ya michezo ya Olimpiki yote imeundwa na wachezaji waliozaliwa nchini Ethiopia na Kenya. Sikutambua tulikuwa na idadi kubwa ya jamii Bahraini hapo!

Pia aliongezea:

@JustAmira: Ingekuwa bora kwa #Bahrain kama kungekuwa na mashindano kwa# vilipua machozi katika#michezo ya Olimpiki

Vile vile, mtumiaji twita anayeishabikia serikali @ ATEEKSTER [ar] aliandika kukosoa waandamanaji kupambana na serikali:

حسافة والله الأولمبياد ماعندهم لعبة “رمي المولوتوف” جان عن خاطرنا ضمنا الميداليه الذهبيه
@ATEEKSTER: Ni vibaya Olimpiki haina michezo kwa ajili ya “Molotov kutupa”, tunaweza kuwa mshindi wa medali ya dhahabu katika hilo.

Tala alijibu, akimwambia:

@Taltool11: Ingekuwaje tungekuwa na mchezo wa kutumia risasi za moto ili kuona kama wewe kufa wakati ninapo fyatua risasi

Makala haya ni sehemu ya makala zetu maalum michezo ya Olimpiki London 2012 na Maandamano Bahrain 2011/12

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.