Mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ya kumfanya mtu kupoteza fahamu yalitumika kutawanya maandamano ya kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi nchini Kuwait. Kuitishwa kwa matembezi ya Karamat Watan ( Heshima ya Taifa), yaliyofanyika siku ya Jumapili, yaliyoandaliwa katika mtandao wa Twita, yaliyowavutia takribani watu 150,000 kati ya watu milioni 3 ambao ndio idadi ya watu wa Kuwait. Taarifa za vyombo vya habari zinaichukulia idadi hii kuwa ni kubwa kabisa katika historia ya Falme za ghuba ndogo.
Waandamanaji walipingana na amri ya Amir Sheikh Sabah al-Ahmad al-Sabah ya kubadili sheria ya uchaguzi inayowataka raia wamchague mgombea mmoja badala ya wagombea wanne kama ilivyokuwa awali katika chaguzi za bunge la Kuwait. Maandamano hayakulenga tu kupinga mabadiliko haya ya sheria ya uchaguzi, bali pia kupinga kubadili sheria hii bila ya kulishirikisha bunge na maoni ya wananchi. Tangu mwisho wa mwezi Juni, Bunge la Kuwait lilisimamishwa na Rais Amir na hatimaye kuvunjwa na mahakama ya kikatiba kwa ‘taratibu zisizo sahihi’ za kuvunja Bunge.
Upinzani umekuwa ukilalamikia jambo hili kwa muda sasa lakini kamwe haukufanikiwa kuhamasisha idadi kubwa ya watu kama ilivyo sasa; hata chama cha kiliberali cha “Tahalof” na kile cha mkusanyiko wa Waarabu “Manbar” walijumuika katika maandamano ya jumapili pamoja na kuwa hawakubaliani na upinzani wa waisilamu wenye msimamo mkali.
Katika hatua ya kipekee, maandamano haya yaliratibiwa kupitia mtandao wa Twita. Akaunti ya Twita @KarametWatan [ar] (ambayo maana yake ni Heshima ya Taifa) ilianzishwa ili kuitisha maandamano. Ilipendekeza picha ya rangi ya chungwa (kwa kurejea harakati za vijana za mwaka 2006 yaliyobadilisha sheria ya uchaguzi kutoka wilaya 25 hadi wilaya 5), na walipanga sehemu za mikutano kwa kutumia ramani ifuatayo:
Kama kawaida, watu wa Kuwait walitumia Twita kuweka picha na video za maandamano. Zifuatazo ni baadhi ya picha;
Ili kuonesha idadi, makundi makubwa ya waandamanaji na nyimbo zilizokuwa zikiimbwa mara kwa mara, video hii ilitumwa katika mtandao wa YouTube na Q8jo7a:
Hii hapa ni video nyingine inayoonesha kwa mbali, matembezi ya makundi makubwa ya waandamanaji jozifanto:
Mwanablogu Alziadi alituma video hii ikionesha waandamanaji wakikimbia kukwepa moshi wa mabomu ya machozi:
Siku ya Jumatatu [Oktoba 22], Gazeti la mtandaoni la Sabr lilitoa taarifa kuwa, waandamanaji waliokuwa wanashikiliwa walishaachiliwa:
@Sabrnews: عاجل/ إطلاق سراح جميع معتقلي مسيرة “كرامة وطن
Muhimu: Wote waliokuwa wanashikiliwa katika matembezi ya Heshima ya Taifa wameshaachiliwa
3 maoni
Mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ya kumfanya mtu kupoteza fahamu yalitumika kutawanya maandamano ya kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi nchini Kuwait. Kuitishwa kwa matembezi ya Karamat Watan ( Heshima ya Taifa), yaliyofanyika siku ya Jumapili, yaliyoandaliwa katika mtandao wa Twita, yaliyowavutia takribani watu 150,000 kati ya watu milioni 3 ambao ndio idadi ya watu wa Kuwait. Taarifa za vyombo vya habari zinaichukulia idadi hii kuwa ni kubwa kabisa katika historia ya Falme za ghuba ndogo.
agency imodels holdings
Kuwait: Ni Maandamano Makubwa Kabisa Kuwahi Kutokea? · Global Voices in Swahili