Kuwait Inacheza Dansi na Inayo Furaha

Kuwait inaonesha furaha yake kupitia video iliyobuniwa upya ya wimbo wa Pharrell unaofahamika kwa jina la Furaha. Video hiyo hapo juu, inayowajumuisha wakazi na raia zaidi ya 150, ni matokeo ya ubunifu wa muongozaji wa filamu, Taibah AlQatami, na video kuandaliwa na mtayarishaji wa filamu ajulikanaye kwa jina la Mohammed Al Saeed.

Kwa mujibu wa @Loft965:

Lengo lilikuwa ni kuandaa upya wimbo wa Pharell, “furaha” ili uwasilishe ujumbe wa hali halisi ya Kuwait kwa kuchukua picha kutoka katika maeneo maalum ya jiji ikiwa ni pamoja na kutambulisha tena “Fulana za Kuwait” za bure zilizovaliwa wakati wa vita ya Ghuba ya Uajemi wakati raia walipokuwa wakidai uhuru wa nchi yao. Kwa sasa, vijana wa Kuwait wanadumisha hali ya amani kwa kuonesha kupendezwa na kusherehekea uhuru wa kutoa maoni yao.

Muungano ulioongozwa na Marekani, ulifanikisha kuipatia uhuru nchi ya Kuwait mapema mwezi Februari, 1991, miezi nane mara baada ya kuvamiwa na nchi ya Iraq.

Katika ukurasa wake wa Twita, Nasser AlQatami anasema:

Imetazamwa mara 54,000 na bado inaendelea kutazamwa. Tuendeleze libeneke! Bofya: http://t.co/IgGFm8IMVc

Huda Aldakheel anasema:

Nimekuwa nikicheza kwa kuangalia video hii usiku kucha. Asante sana, inapendeza.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.