Kuwait: Nampenda Osama Bin Laden

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusu Kifo cha Osama Bin Laden.

Picha ya Khulood Al-Khamis kutoka kwenye akaunti yake ya Twita

Ni kitu gani kinachoweza kumfanya mwanamke aanguke katika penzi na mtu kama kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden? Inavyoonekana, ni ndefu ndefu, anasema mwandishi wa makala kutoka Kuwait Khulood Al-Khamis, ambaye aliwastua wasomaji kwa barua yake ya mapenzi aliyoandika kwa kiongozi wa ugaidi, ambaye aliuwawa na Marekani, huko Abbottabad, Pakistan, wiki iliyopita.

Katika barua yake, kwenye makala yake ya gazeti la kila siku la Kiarabu Al-Qabas, Al-Khamis alimuelezea Bin Laden kama mwanume wa ndoto zake, aliezea jinsi mabvyo angependa kwenda naye ndani ya pango lake, na kuosha ndefu zake na kuwa mmoja wa wake zake. Alimalizia makala yake yake kwa kuahidi kumngojea ahera ili kuendelea na simulizi zake hizi za Scheherazade.

Mwandishi huyo wa makala, ambaye pia ni mwandishi wa hadithi fupi fupi, ana akaunti ya Twita. Makala yake iliwastua wasomaji wengi. Kwenye Twita, Al-Khamis alitajwa tajwa kwa kejeli, pamoja na kutoka kwa Ayman Zawahari, akaunti ya kubeza ya kiongozi wa pili wa Al-Qaeda, ambaye alimuuliza alimuuliza swali dogo rahisi:

شدعوه خلود مالنا رب يعني؟

Oh Khulood, sasa vipi kuhusu mimi?

Saddam Hussein, akaunti nyingine ya kubeza, ilifuatia:

خاتون خلود خميس ، مو آني هم مجرم وچتلت بشر أكثر من أسامه .. ليش ماتفكرين بيا ؟!

Bi Khulood Khamis, Mimi pia ni mhalifu niliyeua watu wengi zaidi yawale aliwaua Osama, kwa nini haunifikirii?

Yahaya Teleb Ali, mwandishi kijana wa Kuwait, aliandika ujumbe mwingine wa kebehi wa Twita akisema:

ميخالف شباب، الأخت عبرت عن رأيها وإعجابها بأسامة بن لادن وتبي تمشط لحيته. هذا رأي والتعبير عنه حق مكفول. أنا عن نفسي أبي أمشط شنب نيتشه

Jamani, anaelezea maoni yake na mapenzi yake kwa Osama Bin Laden; anataka kuchana ndevu zake. Na hayo ndio maoni yake na kuyaeleza ni haki yake hakika. Mimi binafsi ningependa kuchana masharubu ya Nietzsche.

Mtumiaji mwingine wa Twita, ambaye anadai kuwa ni rais wa eneo la watu wa tabaka juu la Shuwaikh, aliandika twita tofauti tofauti kuhusu makala ya Al-Khamis, pamoja na hii:

بعد مقالة خلود الخميس..ڤيكتوريا سيكريتس تطرح تصاميم جديدة بعنوان( آآآآه فجرني)عبارة عن لنجيري مفخخ بالديناميت للإغراء الإرهابي

Baada ya makala ya hivi karibuni ya Khulood Al-Khamis, Victoria Secret itazindua toleo jipya la mkusanyo wa “Oh Nilipue kwa Bomu” ambalo litajumuisha nguo za ndani zilizosheheni baruti za kutongozea za kigaidi

Mtumiaji mwingine wa Twita wa kike, Ghadory, hakusita kumbeza Al-Khamis, lakinisasa kwa Kiingereza:

#kholoudalkhamees (Kwa sababu wewe ni kituko) Unataka sana, huba mbaya Na #OBL sasa hivi nimepata mtizamo mpya kabisa wa wimgo wa lady gaga

Molten86 aliandika kwa sauti isiyo ya mzaha:

#kholoudalkhamees تبي تشتهر ! بسرعة ! أمدح ظالم إرهابي .. مبروك انت نجم لامع الآن

Anataka umaarufu wa haraka. Kumsifia gaidi mdhalimu! Hongera, wewe ni nyota sasa.

Salman Al-Naqi naye alikabiliana na makala ya Al-Khamis bila masihara akisema:

أحذروا السلفية الجديدة التي تطل علينا برجال حليقي اللحية و نساء سافرات الوجه.. و لنا في الكاتبين بدر البحر و خلود الخميس خير برهان ! #kuwait

Kuwa mwangalifu na masalafi (wale wenye msimamo mkali) ambao wanakuja huku wamenyoa ndevu na wanawake wasiovaa baibui. Waandishi Bader Al-Bahar na Khulood Al-Khamis ni mifano mizuri

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusu Kifo cha Osama Bin Laden.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.