Japani: Iambieni Dunia isaidie

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011.

Picha zilizotafutwa na kuwekwa kwenye twita zinaweza kuleta mambo ya kushangaza.

Tafuta herufi hizi “宮城” (Miyagi) na picha chache zitatokea kutoka kwenye wilaya hiyo, moja ya maeneno yaliyoharibiwa sana nchini Japani baada ya tsunami. Nenda chini, na picha moja inaonekana, yenye rangi ya kahawia na bluu mpaka utakapoibofya…

Picture from Kesennuma

Picha kutoka Kesennuma, Wilaya ya Miyagi, Japani, moja ya maeneo yaliyoharibiwa sana na tsunami.

…kuonyesha nchi iliyoharibiwa. Hii ndiyo sehemu ya iliyobaki yaKesennuma, mji mdogo, wakati fulani uliwahi kuwa na makumi ya maelfu ya wakazi.

Soma maelezo ya picha, na habari inatokea ya mtu aliyewahi kuishi katika mji. Mtu huyu aliituma picha kwa rafikiCherie, anayeishi Sydney, aliyeituma picha hiyo kwa barua pepe kwa njia ya mtandao wa intaneti. Ujumbe unasomeka:

なんとか家族みな無事でいます。家は半分なくなりました
家の前の風景で家も駅も商店街も何にも無くなりました…

Kila mmoja katika familia yangu alinusurika na kutoka salama. Hapa ni sehemu ya nyumbani kwetu, ambayo nusu imeondoka. Kila kitu mbele ya nyumba yetu, kituo cha treni, sehemu ya maduka vyote vimesombwa mbali na maji….

宮城県気仙沼市の被害をネットで配信したいのですが、私には出来ません 助けが必要です。出来るだけ色んな国へ知らせたいと思います。このメールも電波が入る所まで車でやっときて打ってます。これから生き残った人達が生きるために少しでも援助お願いします

Ninataka kuonyesha madhara yaliyotokea katika Jiji la Kesennuma kwa njia ya mtandao wa intaneti, lakini siwezi kufanya lolote mwenyewe. Tunahitaji msaada. Ninahitaji kutuma ujumbe huu ulimwengu mzima, kwa wingi kadiri inavyowezekana. Niliendesha (gari) mpaka nilipopata mawimbi ya mtandao ili kuniwezesha kutuma barua pepe hii. Tafadhali saidieni kwa namna yoyote mnayoweza, kuokoa maisha ya wale walionusurika.

Cherie anaongeza maneno machache mwisho wa maelezo yake:

Ninawapenda, tafadhali msipoteze matumaini. Tunaweza kuonana tena, tunawaombea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.