Naijeria: Je, Teknolojia itaathiri uchaguzi wa mwaka 2011?

Wanaijeria wanaingia kwenye uchaguzi tarehe 16 Aprili 2011 kumchagua rais wao mpya. Uchaguzi uliahirishwa kutoka siku iliyokuwa imepangwa awali ya Aprili 9 kwa sababu ya kasoro za kimuundo. Katika makala hii tunatazama namna Wanaijeria wanavyotumia teknolojia kuwezesha uwazi katika uchaguzi, ushirikishwaji wa kisiasa na utawala bora.

Chukua Msimamo, hadharani!

Wanaijeria katika mitandao ya kijamii wanaweza kuchukua msimamo wa wazi kwa kutumia tovuti ya Take a Stand:

Tovuti ya TakeAStand inawawezesha watu kujitanabaisha kwa uwazi kwa misimamo yao katika masuala fulani. Wavuti hiyo ilitengenezwa kupambana na tabia ya kupuuzia masuala muhimu, unafiki na tabia ya kutokujitoa kwa moyo kunakofanywa na marafiki na jamaa zetu katika uchaguzi ujao wa Naijeria. Take A Stand ni kile kinachoitwa “Option A4” ya uchaguzi wa mtandaoni. Option A4 pia ikijulikana kama kura ya wazi ni mfumo wa uchaguzi uliotumiwa katika uchaguzi wa rais mwaka 1992. Wapiga kura walihitajika kujipanga kwenye mstari nyuma ya wagombea waliowaunga mkono. Uchaguzi wa mwaka 1992 ndio uchaguzi unaosemekana kuwa huru na haki zaidi katika historia ya uchaguzi wa Naijeria.

Maswali Yanayoulizwa Mara nyingi kuhusu wavuti hiyo ya TakeAStand:

Kuna tofauti gani kati ya [sic] na upigaji kura wa mtandaoni? Kupiga kura mtandaoni huhitaji kufahamika jina lako. Kwa kutumia Take A Stand, unaisimamia kura yako hadharani. Hata hivyo, unaweza kujipambanua kwa ajili ya mgombea mmoja tofauti na ilivyo katika upigaji kura wa mtandaoni ambapo unaweza kutumia anuani nyingi za barua pepe kuwapigia watu wengi. Kwa nini kuna wagombea wanne tu wakati wapo wapatao 18 wanaogombea? Kwa hakika sababu ni ile ile ya kwa nini vilabu 20 vya ligi kuu huwa havifuzu Ligi ya Mabingwa. Hata hivyo, kama watu wa kutosha watatuma barua pepe kwenda kwenye info@takeastand.com.ng wakipendekeza kuingizwa kwa mgombea fulani katika orodha, tutayafikiria maombi hayo. Niko kwenye nafasi inayonitaka kutokuwa na upande wowote kwa hiyo siwezi kuutaja upande huo hadharani (mfano mwanajeshi, Afisa wa Tume ya Uchaguzi ya Naijeria). Kuna mantiki hapa. Waandishi wa habari hawana hali ya tofauti sana hata hivyo (na hao tuliowataja), wanapaswa kuwa walinganifu, na sio kutokuwa na upande. Sina anuani ya Facebook wala Twita. Pole, hiyo ndiyo nyenzo pekee ya utambulisho wa wazi duniani kote.

Upigaji kura wa mtandaoni kwa ajili ya Uchaguzi wa Naijeria mwaka 2011

Upigaji kura wa mtandaoni kwa ajili ya Uchaguzi wa Naijeria mwaka 2011 ni wavuti inayowawezesha wa-Naijeria ambao hawatakuwa na fursa ya kupiga kura kufanya hivyo mtandaoni:

Kwa wa-Naijeria waiishio nje ya nchi ama wa-Naijeria wanaotumia mtandao kwa ujumla ambao hawatakuwa na fursa ya kupiga kura, kikusanya habari hiki cha mtandaoni kimepangiliwa kuyaruhusu makundi kupiga kura kwa ajili ya mgombea Urais aliye chaguo lao katika uchaguzi wa Naijeria mwezi Aprili 2011. Sheria za uchaguzi matokeo yataoneshwa mara tu unapomchagua mgombea mmoja na kubofya kitufe cha “umekamilisha”. Utahitaji kuwa wa mbari (asili) ya Naijeria. Unaweza kupiga kura mara moja tu –(Ili kujaribu kukaribiana na tukio halisi)

Wanaijeria Waamua

Tovuti nyingine inayowawezesha Wanaijeria kupiga kura mtandaoni inaitwa Nigerians Decide (wanaijeria waamua):

Ndugu zangu Wanaijeria, ni wakati wa kuamua mustakabali wetu kama taifa. Kura yako ni NGUVU ya kuamua ni nani ataiongoza NAIJERIA kuondokana na ufukara, ukosefu wa ajira, kutokuwepo kwa usalama, na mgombea atakayeirudisha heshima ya kweli ya Wa-Naijeria. PIGA KURA SASA! NA PIGA KURA KWA USAHIHI!

Hapa ni matokeo ya hivi karibuni:

1. Rais Goodluck Jonathan (Peoples Democratic Party) 621 21%
2. Muhammadu Buhari (Congress for Progressive Change) 1870 64%
3. Nuhu Ribadu (Action Congress of Nigeria (ACN) 343 12%
4. Pat Utomi (Social Democratic Mega Party) 24 1%
5. Dele Momodu (National Conscience Party) 7 0%
6. Ibrahim Shekarau (All Nigeria Peoples Party) 34 1%

ReclaimNaija (Ikomboe Naija):

ReclaimNaija ni jukwaa pana la ushirikishwaji maarufu wa wananchi wa kawaida katika kukuza uwazi wakati wa uchaguzi na serikali ya kidemokrasia. IkomboeNaija wanatumia jukwaa la Ushahidi kufanya uangalizi katika Uchaguzi wa Naijeria 2011.

ReclaimNaija: Kura yangu, Nguvu yangu!

Malengo ya ReclaimNaija ni:

Kumwezesha Raia mmoja moja wa Kinajeria kuwa mwangalizi wa matukio katika maeneo ya: Uchaguzi Huru na haki; Ufisadi wa maafisa wa ofisi za umma, watumishi wa umma na mashirika yanayoshughulika na sheria; uvunjifu wa haki za binadamu wanaokutana nao; Kufanyika chanzo cha habari kwa ajili ya tasnia ya mawasiliano ya umma katika kutangaza matukio yanayoripotiwa na raia wa Kinaijeria; Kutoa mfumo wa kuziunganisha na kuzichambua taarifa na kuzielekeza kunakotakiwa ili kufahamisha ufikiwaji wa maamuzi ya umma, sura na kusababisha mabadiliko ya matokeo ya sera.

Akiandika kwenye blogu ya ushahidi Linda alikuwa na haya ya kusema kuhusu ReclaimNaija:

Jukwaa la IkomboeNaija, linaloendeshwa na nyenzo ya wavuti ya Ushahidi, ni jukwaa la kutoa taarifa lililotengenezwa kama mfumo wa umma kupata namna ya kusikilizwa sauti zao kuhusiana na masuala kama uwazi wakati wa uchaguzi na utawala. Jukwaa litawawezesha raia kuuangalia mchakato wa uchaguzi na kuripoti matukio ya udanganyifu yanayovuruga uchaguzi na ukiukwaji wa taaratibu nyinginezo kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno ama kupiga simu kupitia nambari zilizotolewa katika lugha kuu nne (Kihausa, Ki-Igbo, Kiyoruba na Kipidgini). Kwa ujumbe mfupi, Frontline SMS ndiyo imekuwa ikitumika kama namna kuu ya kutumia huduma hiyo. Raia pia wanaweza kuripoti kupitia barua-pepe, kutoa taarifa moja kwa moja kwenye tovuti na kwenye twita. Mradi wa Maisha ya Jamii uliweza kwa mafaniko makubwa kulitumia jukwaa hili kwa ajili ya kukuza uwazi wakati wa uchaguzi katika kipindi cha kabla ya uchaguzi wa mwaka 2011.

Reclaim Naija inatafsiri upya dhana ya uangalizi wa uchaguzi nchini Naijeria:

Kwa kuongeza, wavuti ya reclaimnaija.net inafanya kazi kama hazina ya taarifa inayotegemewa mtandaoni kwa ajili ya habari za uchaguzi wa mwaka 2011. Inaonyesha vituo vyote vya kupigia kura, wilaya za kiseneta na kata, Katiba ya Naijeria, taarifa binafsi za wagombea, sheria uchaguzi ya mwaka 2010, ratiba ya uchaguzi, miongozo ya uchaguzi, idadi kamili iliyothibitishwa ya wapiga kura waliojiandikisha, vyama vya siasa na makarabrasha ya kutoa elimu kwa mpiga kura. Kwa mara ya kwanza katika histora yetu, raia wa nchi hii wanalo jukwaa la kuheshimika kwa ajili ya kukuza uwazi wakati wa uchaguzi na ushirikishwaji unaowafikia wengi. Raia walikuwa na nguvu ya kugeuza kwa faida mchakacho wa uchaguzi. Kwa mfano, taarifa nyingi zilikuja kutoka kwenye jamii zisizo na fursa ya kutosha kufika kwenye vituo vya kujiandikishia kupiga kura na jamii kadhaa kama hizo ilibidi ziongezewe muda wa mwisho wa kujiandikisha kwa siku mbili zaidi. Reclaimnajia.net tayari imefanikiwa kutafsiri upya mabadiliko ya mtazamo wa uangalizi wa uchaguzi nchini Naijeria.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.