Naijeria: Wafuatiliaji wa twita unaoweza kuwafuatilia wakati wa Uchaguzi wa Naijeria mwaka 2011

Ni msimu wa uchaguzi nchini Naijeria. Lakini ratiba ya uchaguzi huo imesogezwa mbele kwa juma moja zaidi kwa sababu ya matatizo ya kiuratibu. Uchaguzi wa Rais ulipangwa kufanyika tarehe 9 Aprilli 2011. Hii ni orodha yetu ya watumiaji wa twita unaweza kufuatilia kazi zao wakati wa uchaguzi wa Naijeria 2011 na miitikio yao kuhusiana na suala la kuahirishwa uchaguzi huo.

@MrFixNigeria ni Balozi wa Microsoft wa Usalama wa Mtandaoni na ndiye meneja wa kampeni za Urais mwenye umri mdogo kuliko wote katika Naijeria.

@EiENigeria (Imetosha sasa basi Naijeria) ni muungano wa Wa-Naijeria vijana wanaofanya kazi ya kuhamasisha ushiriki wa vijana katika uchaguzi wa mwaka 2011.

Kutokana na kuahirishwa kwa uchaguzi, tutakuwa tukizindua kura yetu ya mwisho ya maoni (“Nani utampa kura yako tarehe 9 Aprili”) siku ya Jumanne, Aprili 5. #NigeriaDecides

@toluogunlesi ni mwanasafu katika gazeti la Naijeria, liitwalo NEXT, mwanafunzi wa Uandishi wa Ubunifu katika Chuo Kikuu cha East Anglia (UEA).

Siku ya huzuni kiasi gani kwa Naijeria:

Siku ya huzuni kwa Naijeria: uchaguzi umeahirishwa, Ibori ameachiwa, na tena moja ya mpishiwyake smahiri anaunguza yai linalochemka WTF http://twitpic.com/4gb7yb

@feathersproject ni mwandishi wa ki-Naijeria, mchapishaji, na mwandishiwa Global Voices Online.

UCHAGUZI WA BUNGE: AFADHALI UMEAHIRISHWA KULIKO UNGEVURUGWA http://wp.me/pfoBI-jq

@TechLoy ni blogu inayoongoza katika masuala ya kiteknolojia, inayoleta habari mpya mpya za teknolojia, inayotoa tathmini za kampuni an kiradi inayozinduliwa pamoja na tathmini za bidhaa mpya.

Alama ya #Jega inaongoza kwenye Twita:

Inafurahisha kumwona “Jega” [Attahiru Jega, kiongozi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)] akiongoza kwa Twita duniani kote kama #Jega ataamua mustakabali wa Naijeria

@COOL2VOTE:

#BREAKINGNEWS (HABARI MPYA KABISA): UCHAGUZI UMEAHIRISHWA MPAKA APRILI 4.. IMETHIBITISHWA NA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI. #Cool2Vote #NigeriaDecides

@Africanelection ni mradi unaokuza uwezo wa waandishi wa habari, waandishi wa kiraia kutumia vyombo vipya vya habari kwa minajili ya kufanya uangalizi na kuripoti uchaguzi barani Afrika.

Naijeria:Harakati zimesitishwa mpaka saa 12 jioni . http://ow.ly/4rHrB #naijavotes2011

@delemomodu2011 ni mgombea wa urais kupitia chama cha National Conscience Party (NCP).

Tulichokishuhudia leo ni udhihirisho wa wazi wa kushindwa kazi na kukosa mipango kwa hali ya juu. #INEC

@DamiOyedele :

Posti mpya: ‘Tarehe mpya ya uchaguzi haiwezekani’ anasema Dele Momodu http://bit.ly/ewGfNh cc @mrfixnigeria


@gbengasesan
ni mjasiriamali wa kijamii wa Naijeria mwenye kuvutiwa sana matumizi ya TEKNOHAMA katika maendeleo; kuelekea kwenye kuzalisha fursa zilizo bora na zenye uhakika. Unaweza kusoma zadi kumhusu ‘Gbenga Sesan hapa.

Leo isingepaswa kutokea… soma blogu yangu ya hivi karibuni, “Wakati wa-Naijeria wakiamua (sehemu ya 6)”, kwa kwenda hapa http://gbengasesan.com #ReVoDa #NigeriaDecides

@forakin ni mtu asiye na ukinega katika tarakilishi, mwanablogu, na m-Naijeria azungumzaye Kifaransa anayeishi Amsterdam.

@AsylumAfricana Nilikuwa mtazamaji wa mtandaoni wa mkutano wa INEC [Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi], walipoambiwa hakuna maswali (yatakayoulizwa) waliokusanyika walilalamika kwa sauti.

@reclaimnaija ni jukwaa pana linalojihusisha na ushirikishwaji maarufu wa wananchi wa chini katika kunadi uwazi wakati wa uchaguzi na serikali ya kidemokrasia.

Taarifa zetu zinathibitisha kauli ya kijasiri ya Prof. Jega kwamba majimbo mengi hayana vifaa vya upigaji kura. #reclaimnaija #NigeriaDecides

Watumiaji wengine zaidi wa twita unaoweza kufuatilia kazi zao wanaweza kupatikana hapa.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.