Mghosya · Disemba, 2009

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Disemba, 2009

Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani

Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.

20 Disemba 2009

Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu

Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele. Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho. Tunazipitia baadhi.

20 Disemba 2009

Ghana: Rais Atta Mills Dhidi ya Chama Chake Mwenyewe?

Katika miezi michache kuelekea uchaguzi wa Rais Hohn Evans Atta Mills, wa-Ghana wengi, pamoja na wale walio nje ya nchi, waliohofu kwamba ushindi wa chama cha New Democratic Congress (NDC) ungeweza kugeuka kuwa utawala mwingine wa mwanzilishi wa chama hicho na mtawala wa zamani wa kijeshi, Rais Jerry John Rawlings.

13 Disemba 2009

Morocco: Kusherehekea Idi katika Sehemu za Mashambani

Wikiendi hii iliyopita, Wamoroko walisherehekea Eid Al-Adha. Wanablogu walioko sehemu za vijijini nchini Moroko wanasimulia simulizi zao kuhusu Eid ya mwaka huu. Kwa kuwa upatikanaji wa intaneti upo sehemu chache n amara nyingi ni wa aghali mno nje miji mikubwa, wengi wanaoblugu kutokea sehemu za mashamba ni Wafanyakazi wa Amani wa Kujitolea (PCVs) na kwa hiyo wako katika nafasi ya kuweza kutoa mitazamo kama wageni kutoka nje… walioko ndani.

13 Disemba 2009