Shiriki Zoezi la Kujifunza Lugha za Asili Mtandaoni

Screenshots from some of the participants of the Indigenous Language Challenge

Picha mnato za video za washiriki wa Shindano la Lugha za Asili

Soga la mtandaoni la Love it or hate it [Upende usipende], kuhusu Zoezi la Mabonge ya Barafu mapema mwaka huu lilikuza uelewa wa ugonjwa unaofahamika kama amyotrophic lateral sclerosis. Washiriki walijipiga picha wakijiwekea mabonge ya barafu vichwani mwao na kumtaka mtu mwingine kufanya vile vile na akishindwa alipaswa kutoa fedha kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa uliotajwa.

Sasa wazo kama hilo linalolenga kukuza uelewa kwa lugha za asili limepamba moto mtandaoni. Katika zoezi la Lugha ya Asili, yeyote anayekubali zoezi hilo lazima arekodi video akiongea lugha yake ya asili na kumtaka mtu mwingine aongee vile alivyoongea yeye. Matokeo yake watu wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatengeneza video, wengine kwa mara ya kwanza, kama njia ya kutangaza lugha zao mtandaoni na kuwafanya watu wengine kuitambua na kuitumia.

Kundi la mtandao wa Facebook lilianzishwa kukusanya viungo vya video hizo zinazoingizwa, na kwenye ukurasa huo washiriki wanaweza kutuma kazi zao na kuungana na wengine wanaoshiriki Zoezi hilo. Wengi huchagua kupandisha video zao moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook na huko husikia lugha zinazozungumzwa kwenye bara za Amerika Kaskazini kama vile Kwak'wala na Lakota, vile vile lugha ya Miriwoong kutoka Australia, kwa mfano.

Jitihada za kuweka kumbukumbu sawa kuhusu asili ya Zoezi hili zinaendelea, lakini kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo, mmoja wa washiriki wa mwanzo kabisa alikuwa James Gensaw, aliyekuwa anayezungumza maneno ya lugha ya Yurok.

Akina nani ni washiriki? Na kwa nini zoezi hili ni la muhimu? Colleen Fitzgerald, Mkurugenzi wa Maabara ya Lugha za Asili za Amerika Kaskazini kwenye Chuo Kikuu cha Texas mjini Arlington, anatoa maoni yake kupitia posti yake kwenye blogu yake kwenye makala ya Huffington:

Video nyingi kama hizi zimetoka kwa watu wazima wanaojifunza lugha ya pili. Kwa miaka mingi, shule za bweni zinazoendeshwa na serikali nchini Marekani na Kanada ziliwachukua watoto kutoka familia za wenyeji. Hatua hii ilikuwa na matokeo makubwa kwenye kujifunza lugha za asili. Watoto waliopoteza bure miaka mingi ya kukosa mazingira muafaka ‘ya nyumba’ na wazazi wao waliweza kuwasiliana kwa lugha zao za asili. Nyumba ni mahali ambapo maendeleo ya lugha za watoto huongezeka na kukua, na ndipo watoto hujifunza lugha nyingine tofauti zinazowafanya wawasiliane. Kinachopotea ni nini? Vingi, kuanzia lugha ya kila siku ya mawasiliano, kutaniana, mbinu na hata lugha za namna ya kuomba, hotuba za kwenye sherehe, au hata kusimuliana hadithi za kale.

Hapa kuna mifano miwili ya washiriki wa zoezi hili, walioweka video kwenye mtandao YouTube. Jackelyn Seitcher akizungumza kwa lugha ya Nuu-chah-nulth anasema maneno ya kukubali kuingia kwenye shindano.

Monica Peters anachukua fursa ya kushiriki zoezi hili kwa kuonesha tafsiri za kazi zake kwenye Kanienkeha. Kisha anakwenda kwenye ukurasa wa Facebook wa washiriki wa zoezi hili unaoitwa “Kutunza Uimara wa Lugha ya Kanienkeha “, linaloundwa na viongozi na walimu, na wanafunzi ambao ndio kwanza wameanza kuzungumza lugha hiyo.

Zipo video nyingine zilizokusanywa kwenye blogu ya Habari Kutoka California ya Asili.

Konwennenhon Marion Delaronde vile vile alichapisha video yake kwenye kundi linalozungumza lugha ya Kanien'keha (Mohawk). Baada ya kupata changamoto na Kehte Deer, alihamasika kushiriki na kutoa maoni yake baada ya kupandisha video yake:

Tayari ninadhani nimesikiliza lugha zote kutoka mataifa mbalimbali. Ni lazima nikwambie kwamba lugha zote ni tamu. Zungumza lugha yako kama unaweza. Inaleta matumaini. Ninataka kuwahamasisha nyote kuendelea kujifunza, kuendelea kuwafundisha wengine na kwa hakika kuyaanza mapya mapya kwenye lugha mpya, kwa kuizungumza. Ninafuraha sana ninaweza kusema kwa lugha ya Mohawk. Sijafuzu na kuiongea kwa ufasaha, bado kuna ninayohitaji kujifunza, lakini ningependa kumshukuru kila mmoja aliyejirekodi kwa ajili ya Shindano hili, kwa sababu mmenihamasisha.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.