Wabrazili Waingia Mitaani Kumpinga Bolsonaro Kupunguza Fungu la Elimu

Waandamanaji mjini Rio de Janeiro: Elimu ndio silaha yetu. | Picha na: Marianna Cartaxo / Mídia NINJA/Imetumiwa kwa ruhusa

Hapo Mei 15, maelfu ya Wabrazili waliingia mitaani katika majimbo yote 26 wakiandamana kuipinga serikali ya Bolsonaro kukata fedha za elimu ambapo itaathiri mamia ya shule na vyuo.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, serikali ya Brazili ilitangaza kukata kiasi cha asilimia 30 ya kile kinachosemekana ni bajeti ambayo ilikuwa kwa ajili ya gharama za maji, umeme, uendeshaji wa jumla pamoja na tafiti. Wakati ukifiria kuwa jumla ya bajeti kuu ya serikali kwa ajili ya elimu ya juu, makato hayo yanaweza kufikia mpaka asilimia tatu au 5. Hata hivyo, serikali imefuta udhamini kwa wanafunzi wa elimu za juu wapatao 3,500 waliokuwa wakidhaminiwa na serikali..

Kuanzia mtaa wa Paulista huko São Paulo, kituo cha makutano ya maandamano cha kimila mpaka kwenye mashamba ya asili huko Alto Rio Negro, karibu ma mpaka wa Colombia, watu walitoka kwenda kutetea elimu ya umma. Huko Viçosa, Minas Gerais, kundi la watu wapatao 5,000 waliandamana wakiwa na miamvuli huku mvua kubwa ikinywesha.

Brazili inayo vyuo vya umma 69 na idadi kubwa ya vyuo vikuu vya serikali na vyote vinatoa shahada ya kwanza na shahada ya uzamili bure kabisa bila kulipia ada na baadhi ya huduma za kijamii kama vile ofisi za ushauri wa kisheria na hospitali.

Awali, makato hayo yalikuwa yafanyike katika vyuo vitatu lakini baadayr yaliendelezwa kwa vyuo vingine vyote. Waziri wa elimu wa Bolsonaro, Abraham Weintraub alisema kuwa hayo sio “makato” bali ni “kubana matumizi.”

Weintraub alieleza kuwa kuna makato kwa sababu vyuo vya umma ni kama “sehemu ya uharibifu.” Alipoulizwa na wanahabari aleleze mifano ya huo “uharibifu”When alitaja uwepo wa mikusanyiko mikubwa ya kijamii vyuoni na pia uwepo wa “sherehe za watu walio uchi.”

Weintraub aliteuliwa kuwa waziri mapema mwezi Aprili baada ya aliyemtangulia kukaa kwa muda kidogo kuondolewa kwa sababu ya kuhusishwa na baadhi ya migogoro. Waziri huyu mpya mara zote amekuwa akitoa maoni yanayowiana na sera za mrengo wa kulia kama vile madawa ya kulevya yalitambulishwa Brazili kama mkakati wa wakomunisti, na anataka kufuta “utamaduni wa U-Marx” vyuoni..

Baadhi ya wakuu wa vyuouni wamesema kuwa makato hayo yanaweza kuwazuia “milango yao kufunguka” mapema mwanzoni wa muhula wa pili wa 2019. Ofisi ya mwendesha mashataka wa serikali imetuma taarifa kwa mwanasheria mkuu akilalamikia makato ya kuwa ni ukiukwaji wa katiba ya Brazili.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Minas Gerais (UFMG) ambao wanatafiti makundi ya WhatsApp huko Brazili wamegundua kuna mazungumzo mengi kupitia app hiyo hasa baada ya kutangazwa kukatwa kwa bajeti. Utafiti umetengeneza kitumizi ambacho kitafuatilia kwa upana makundi ya WhatsApp na kitatumiwa kwa upana na shirika linalojihusisha na kuuchimbua ukweli nchini Brazili. Mtafiti kiongozi Fabrício Benevuto hapo Mei 8 ukurasa wake wa Facebook alisema :

São monografias/dissertações/eventos ridicularizados por seus títulos e temas. São imagens de pessoas peladas em festas (que nem são nas universidades) e protestos e memes dizendo que os alunos das federais levam mais de 12 anos pra formar, pois só usam drogas. Claramente é um esforço orquestrado. Trabalho de profissional. Segue o mesmo estilo da campanha eleitoral. Quem financia essa fábrica de desinformação?

[Picha ni pamoja] picha zisizo na rangi/machapisho/matukio yaliyobezwa kwa sababu ya vichwa vya habari na mada zake. Kuna picha za watu wakiwa uchi katika sherehe(ambao hawapo hata.vyuoni) na mizaha kadhaa ya waandamanaji inayosema kuwa inawachukua wanafunzi miaka 12 kuhitimu kwa sababu wanabwia dawa za kulevya muda wote. Hili iko wazi kuwa ni kusudi lililopangwa. Kwa mtindo ule ule wa kampeni za uchaguzi. Nani anakidhamini kiwanda hiki cheye kutoa habari za uongo?

Makala katika wavuti ya Ciência na Rua (“sayansi mitaani” kwa Kireno) inadai kuwa vyuo vya umma vinazalisha asilimia 95 ya tafiti za kisayansi nchini Brazili. Utafiti uliofanywa na kamapuni toka Marekani ya Clarivate Analytics mwaka 2018 inaonesha kuwa kati ya vyuo 20 wazalishaji wa tafiti bora, 15 ni sehemu ya mtandao wa serikali.

Katika siku ya maandamano, waziri Weintraub aliitwa kwenda kutoa maelezo kuhusu kukatwa kwa bajeti katika bunge la nyumba ya chini ya Kongresi.

Baadaye Bolsonaro alikuwa jimbo la Texas nchini Marekani ambapo alikutana na Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush. Alipoulizwa kuhusu maandamano hayo Rais alisema:

É natural [que haja protesto], agora a maioria ali é militante,  não tem nada na cabeça, se perguntar 7×8 pra ele, não sabe.  Se você perguntar a fórmula da água, não sabe, não sabe nada. São uns idiotas úteis, uns imbecis, que estão sendo usados como massa de manobra de uma minoria espertalhona que compõe o núcleo de muitas universidades federais no Brasil.

Ni kawaida [kwamba maandamani yametokea], sasa, wengi wa watu pale ni mgambo wasio na kitu kichwani. Kama utawauliza jawabu la 7 mara 8, hawajui. Kama unaju waulize kuhusu muundo wa maji hawatajuwa, hawajui kitu. Ni wajinga na wapumbavu wenye faida na wamekuwa wakitumiwa na watu wachache wenye hila wanaoongoza vyuo kadhaa vya umma nchini Brazili.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.