Kutana na Vijana wa Ecuado Wanaoendesha Kipindi cha Kwanza cha Lugha ya ki-Chwa Radioni Nchini Marekani

Charlie Uruchima in Radio El Tambo Stereo in Bronx, Photo by Itzel Alejandra Martinez for Remezcla. Used with permission.

Charlie Uruchima akiwa kwenye Radio El Tambo Stereo mjini Bronx, Picha na Itzel Alejandra Martinez wa Remezcla. Imetumiwa kwa ruhusa.

Ifuatayo ni sehemu ya makala kamili iliyohaririwa upya iliyoandikwa na mwandishi kwa ajili ya Remezcla, na inaweza kusomwa hapa.

Umbali mfupi kutoka kwenye mitaa ya kona ya Bronx Kusini, eneo lenye idadi kubwa ya wachuuzi, karibu na Kiwanja cha mpira cha Yankee, linaonekana jengo lisilo na mvuto lenye rangi ya kahawia. Huwezi kulifahamu vizuri ukiwa nje, lakini kwenye ghorofa ya chini, panapatikana kituo cha radio na sehemu nzuri maalumu kwa wenyeji wa asili ya Ecuado wanaojulikana kama Kichwa wanaoishi jijini New York. Jamii hii inakadiriwa kuwa na watu wapatao 10,000. Tofauti na lugha za ki-Hispaniola, Kiingereza, na hata ki-Hispania kilichochanganywa na Kiingereza, kuna lugha ya kale ya Kichwa inayotikisa studio hiyo na mashairi, ghani na midahalo.

Ikiwa imeanzishwa 2014, Kichwa Hatari ni kipindi cha kwanza nchini humo kinachoendeshwa kwa lugha ya ki-Chwa, lafudhi ya Quechua inayozungumzwa na wenyeji wa Ecuado wanaofahamika kama Kichwa. Kuanzia miaka ya 1990, jamii za wenyeji kutoka Ecuado wamehamia Marekani, hususani New York na maeneo mengine ya mjini, kukimbia hali mbaya ya uchumi nyumbani iliyowakumba wenyeji. Hata hivyo, pamoja na idadi yao kuwa ya wastani, jamii ya Kichwa imekuwa haionekani miongoni mwa wa-Ecuado na hata jamii kubwa ya wa-Latino.

Kichwa Hatari, ambayo ina maana ya “Jamii ya Kichwa Inayoibukia,” inalenga kurudisha umaarufu na kukuza sauti ya wenyeji wa Ecuado kupitia mitandao ya kijamii, ikiwa imeanzishwa na kuendeshwa na watu wa ki-Chwa. Kila mchana wa ijumaa, watangazaji wa kipindi cha Kichwa Hatari — Charlie Uruchima, Segundo Angamarca, Fabian Muenala, na Renzo Moyano — wanakutana kujadili masuala ya muziki wa wenyeji, utamaduni, lugha na mitazamo ya dunia, pamoja na matatizo ya jamii za wenyeji. Kwa pamoja, wanne hao wanaunda kundi la jamii kubwa ya Kichwa, wakiwakilisha vizazi, historia za maisha, na matakwa —kipindi kinachojieleza kama, “kujieleza na bila kuogopa kufanya hivyo”:

Tunawahamasisha watu na kipindi hiki […] Tumeona mabadilio fulani. Wengi wetu tuliogopa kujieleza sisi ni akina nani, lakini sasa, mitaani, kwenye treni, migahawa, watu wanaongelea jamii ya Kichwa. Wanawake wanavaa nguo za asili. Hakuna ile hofu tena.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.