Wazawa wakolombia weusi na jamii za wakulima wameanza maandamano ya umma nchini Kolombia wakipinga mpango wa maendeleo ya Taifa wa Rais Ivan Duque. Mpango huo unaonesha kuwa utavutia wawekezaji wakubwa wa kigeni wa madini na kilimo ambao utatishia kuchukuliwa kwa mashamba ya wazawa.
Katika mwezi Machi 2019, jamii za wazawa walifunga barabara kuu katika mkoa wa Cauca kwa siku 25. Tarehe 25 Aprili waliungana na maandamano ya jamii zingine ili kuongoza maandamano ya kitaifa. Pamoja na vitisho kwa haki za wazawa, waandamanaji wanapinga dhidi ya kukatwa kwa bajeti ya elimu na utekelezaji unaosuasua wa makubaliano ya amani ya mwaka 2016 ambayo Duque ambaye ana mwaka mmoja madarakani ndiye msemaji mkuu.
Wazawa wameyaita maandamano hayo “mingas,” neno la lugha ya Quechua lenye maana ya “kazi ya wote” linalotumika sana katika maandamno katika Amerika ya Kusini.
#ParoNacional | Comunidades indígenas, campesinos, campesinas y afros de Tado, se movilizan desde tempranas horas a lo largo de la vía Pereira-Quibdo en el marco del Paro Nacional #SeValeProtestar pic.twitter.com/YNOOB1oxNd
— Colombia Informa (@Col_Informa) April 25, 2019
Tafsiri: #Maandamano ya kitaifa | Jamii za wazawa, wakulima na watu weusi wa Tado wanahamasishana mapema kuanzia masaa ya asubuhi kuwa barabarani kutoka Pereira kuelekea Quibdo kama sehemu ya maandamano ya kitaifa # Ni fahari kuandamana
Mpango wa maendeleo wa Taifa unahusisha mageuzi katika sekta mbalimbali kama elimu, nishati na kilimo. Wakati Duque anadai mpango huo utawasaidia na kuwainua wakolombia milioni 3.4 kutoka katika umaskini, wachambuzi wanaona kuwa utawafaidisha hasa makampuni binafsi. Viongozi wa wazawa minga wanahusisha sana na masuala ya mpango ambao unaweza kuleta changamoto kwenye haki zao bila kuwa na ushauri mzuri wa miradi ya maendeleo unaohusu mashamba yao.
Wakati serikali imekubali kuongea na viongozi wa wazawa kuhusu mpango huo, makubaliano ya mwisho bado hayajafikiwa. Kutokana na gazeti la El Espectador, ukubwa wa ardhi ambao serikali inataka kutenga kwa ajili ya wazawa ni pungufu ya kile jamii inachohitaji:
La diferencia entre lo que ofrece el gobierno de Iván Duque y lo que piden las comunidades indígenas para despejar la vía Panamericana es abismal. El Ejecutivo habla de 1 500 hectáreas para resolver las necesidades de todas las organizaciones que integran la minga, mientras que el requerimiento de los organizadores de la protesta es de 40 000 hectáreas
Tafsiri: Tofauti kati ya kile ambacho serikali ya Iván Duque inatoa na kile ambacho jamii za wazawa wanakiomba kwa ajili ya kufungua barabara kuu ya Panamericana ni kidogo mno. Rais anazungumzia keta 1,500 kutatua mahitaji ya taasisi zote ambazo zinaunda minga, ambapo mahitaji ya taasisi ambazo zinaandamana ni hekta 40,000.
MAKUBALIANO YA AMANI
Yalisainiwa kati ya Rais wa zamani Juan Manuel Santos na viongozi wa majeshi la ukombozi ya Kolombia ambalo ni jeshi kubwa la msituni , Makubaliano ya amani ya 2016 yalimaliza msuguano uliodumu kwa miongo mitano nchini humo na kutangazwa kusitishwa kwa mapingano na wanachama wa FARC ya zamani .
Pia, makubaliano ya amani yamezuia watu na makampuni ya nje kujikusanyia ardhi katika maeneo ya vijijini. Zaidi ilihamasisha upangaji na ugawaji upya wa maeneo madogo kwa wazawa, wakolombia weusi na jamii za wakulima ambao waliathirika sana na mgogoro huo wa muda mrefu. Umilki wa ardhi usiosawa katika maeneo ya vijijini ilikuwa ni sababu kuu iliyosababisha kikundi cha FARC kuchukua silaha miaka ya 1960.
Hata hivyo, utekelezaji kamili wa makubaliano umetelekezwa kwa kuwa sekta nyingi zisizobadilika Kolombia zipo kinyume na masharti ya makubaliano. Wakati, vikundi vidogo vidogo vyenye silaha vinaendelea katika maeneo ya nchi na wameanza vita vya kutawala maeneo yalikuwa yanatawaliwa na FARC. Matokeo yake idadi ya viongozi wa jamii za vijijini wanaouwawa imeongezeka tangu kusainiwa kwa makubaliano. Wakati tarakimu zinatofautiana kutegemea namna “kiongozi wa jamii” anavyotafsiriwa, ofisi ya mkuu wa itifaki imetaja kuwa viongozi wa jamii 460 wameuwawa kati ya mwaka 2016 na tarehe 31 Machi, 2019.
Duque pamoja na mshirika wake mkuu, Rais wa zamani Álvaro Uribe, ni miongoni mwa wanaokashifu sana makuabaliano ya amani katika miezi ya hivi karibuni, amejaribu kudhoofisha nguvu ya chombo maalumu (JEP) cha utekelezaji wa mapatano ya amani kilichoundwa na mwanajeshi wa msituni na serikali. Makundi mengi yamekasirika kwa hatua hizo ambazo wanasema zinaweza kudidimiza makubaliano ya kweli.
Watu walishirikishana sababu zilizowafanya waungane kwenye maandamano tarehe 25 Aprili wanaenda kuandamana kwa kuwa nii kazi ya taifa ya pamoja kwa maisha
#VamosAlParoPor la Minga Indígena, porque exijimos protección para los líderes sociales, los excombatientes y en respaldo a la JEP y a la implementación de los acuerdos de paz. Por mejores condiciones laborales para el magisterio y las centrales obreras. @C_Pueblos @cutcolombia pic.twitter.com/3wFAsyTeDZ
— Juan Camilo (@JUANCAELBROKY) April 25, 2019
Tafsiri: Tunaenda kuandamana kwa ajili ya umoja wa wazawa kwa sababu tuanahitaji kuwalinda viom=ngozi wa jamii, wakulima wapiganaji katika kuunga mkono JEP na utekelezaji wa makubaliano ya amani. Pia, kuwepo na mazaingira bora ya walimu na wafanyakazi wa serikali kuu.
La Pulla ambayo ni redio kupitia YouTube inayojihusisha na masuala ya kisiasa. Katika mgogoro huu unaokuwa ilifanya uchunguzi wa kina wa video yenye kichwa cha habari “Hiki ndicho huwa kinatokea pale serikali inaposahau watu wake” wakichunguza historia ndefu ya serikali kutowajali katika maeneo ya nchi, hasa idara ya Cauca, Nariño, La Guajira, na Catatumbo. Mwandishi wa habari anaeleza:
La minga nos recuerda que eso no es el único lugar donde viven incumpliendo la gente y le hacen pistola cada vez que pueda. Vemos cuatro regiones del país que el estado ignora por completa.
Tafsiri: Umoja unatukumbusha kwamba watu hawawezi kuishi bila kutekelezewa ahadi na serikali ikiwapiga muda wote inavyoweza. Tunaona mikoa minne ambayo serikali imeisahau moja kwa moja.
Hakuna suluhusho la kudumu lililotolewa kwa mahitaji ya waandamanaji, kwa hiyo maandamano yanaweza kuendelea katika miezi inayokuja.