Matangazo ya Sauti ya ‘Wiki Ilivyokwenda’ Global Voices: Ndugu, Timiza wajibu Wako

Wiki hii tunakupeleka hadi Urusi, India, na Madagascar. Tumeongea pia na mwakilishi wa Global Voices, Kirsten Han kuhusu matukio ya hivi karibuni ya polisi wa Singapore dhidi ya wanaharakati na machapisho yao kwenye mtandao wa Facebook. Pia, tunaongea na mwakilishi wa Global Voices, Marianne Diaz Hernandez kuhusu namna tatizo la umeme linavyotatiza mawasiliano na kukwamisha uhuru wa kujieleza nchini Venezuela.

Shukrani nyingi kwa waandishi wetu wote, watafsiri pamoja na wahariri waliosaidia kukamilika kwa matangazo haya ya sauti. Makala haya yanahusisha simulizi zilizoandaliwa na Kevin Rothrock ,Rezwan, Lova Rakotomalala, Kirsten Han na Marianne Diaz Hernandez.

Katika Makala haya ya Wiki hii kwenye matangazo ya sauti ya Global Voices, tulijadili kuhusu muziki wenye leseni ya Creative Commons kutoka kenye Hifadhi huru za Muziki, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully ulioimbwa na Jahzzar; Cloud Burst ulioimbwa na Kai Engel, Indian Spice ulioimbwa na Podington Bear; Masculine na David Szesztay pamoja na The Fresh Monday ulioimbwa na Dexter Britain.

Picha iliyotumiwa kwenye Soundcloud ni kwa hisani ya Edu Alarcón kutoka Flickr. Imechapishwa kwa mujibu wa leseni ya Creative Commons (CC BY 2.0).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.