Kupunguza Pengo Kati ya Matajiri na Masikini wa Bara la Afrika

Maelfu ya watu wameingia mitaani kuandamana kupinga mishahara duni, gharama kubwa za maisha na hali ya usalama wa nchi isiyoridhisha.

Mwitio wa hatua za kubana matumizi nchini Ugikiriki? Au kufuatilia Mapinduzi ya Kiarabu? Hapana, haya ni maandamano kupigania usawa zaidi katika eneo la Afrika iliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara, kama ilvyotokea hivi karibuni nchini Burkina Faso.

Pengo linaloongezeka kati ya matajiri na masikini linaleta matatizo barani Afrika kama ilivyo sehemu nyinginezo duniani. Kwa hakika, Waafrika wengi wanaamini kuwa hali ya kutokuwepo usawa inaendelea kuonekana wazi: kikundi cha watu wachache kinaendelea kutajirika wakati wengine wakiendelea kufukarika. Tofauti hiyo inasikitisha zaidi Afrika kwa sababu kiwango cha umasikini kimeendelea kuwa juu kwa miongo mingi mfululizo, pamoja na kukua kwa wastani wa Pato la taifa barani humu.

Boti ya pili kwa ughali wake duniani, ikiwa inamilikiwa na mwana wa Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema Mbasogo – Picha kwa matumizi ya umma

Mwandishi wa safu wa gazeti binafsi la kila siku liitwalo L'Observateur Paalga nchini Burkin Faso anaeleza hisia za jumla za kutokuridhishwa na mwenendo wa mambo [fr]:

Les uns prennent l’avion pour aller soigner un rhume des foins pendant que les autres bouffent les pissenlits par la racine parce qu’ils n’ont pas l’argent pour aller traiter un simple palu.

Baadhi wanapanda ndege kwenda kutibiwa ‘aleji’, wakati wengine wengi wakitegemea mizizi ya mitishamba kwa sababu tu hawawezi kumudu matibabu ya kawaida kabisa ya malaria.

Hata hivyo, ukuaji barani Afrika unategemewa – Benki ya Dunia inajaribu kuchora picha chanya ya uwezo wa Afrika, lakini inatahadharisha juu ya pengo kubwa lililopungua baina ya masikini na matajiri:

Ukuaji wa Uchumi Kusini mwa Jangwa la Sahara unabaki kuwa imara huku ukuaji ukitabiriwa kufikia asilimia 4.9 mwa 2013. Takribani theluthi ya nchi zilizo kwenye eneo hilo zina uchumi unaokua kwa asilimia 6 na zaidi, na nchi za Afrika hivi sasa zimekuwa kati ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani […] [hata hivyo ripoti] inabainisha kuwa umasikini na hali ya kutokuwepo usawa vinabaki kuwa “juu isipokubalika wakati kasi ya kupungua pengo hilo ni dogo mno.” Takribani Mwanfrika mmoja kati ya wawili anaishi katika ufukara uliokithiri leo hii.

Revenue inequality in African towns via French documentation - Public domain

Kutokuwepo kwa usawa wa kimapato katika miji ya Afrika kupitia taarifa ya Ufransa -Picha kwa matumizi ya umma

Denis Cogneau, anayehusika kwa utafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo (IRD), anaeleza kuwa hali hii ya kutokuwepo usawa barani Afrika ina asili ya kihistoria inayoelezeka [fr]:

Les États postcoloniaux ont hérité d’institutions économiques et sociales extractives, caractérisées par un dualisme extrêmement marqué entre un secteur formel de taille réduite, et un vaste secteur informel incluant la paysannerie. De même, beaucoup de pays se caractérisent par un dualisme scolaire et sanitaire, caractérisé par la coexistence d’institutions d’élite publiques et privées coûteuses situées dans la capitale, et d’un secteur de base (écoles primaires et dispensaires) faiblement doté en personnel, médiocrement approvisionné et inégalement réparti sur le territoire. Dans ce contexte, l’école a joué un rôle très dangereux, car elle a été (et est toujours) l’une des clefs d’accès, «non seulement aux emplois dans le secteur moderne, mais aussi aux positions dans l’appareil d’État et au pouvoir politique, suivant en cela les évolutions des sociétés européennes». L’inégalité des chances dans l’accès implique, par conséquent, une reproduction plus accentuée des élites politiques.

Nchi zilizowahi kutawaliwa na wakoloni zilirithi uchumi na taasisi za kijamii zenye misingi ya kinyonyaji, hali inayodhihirishwa na pande mbili zenye tofauti kubwa kati ya sekta ndogo rasmi na sekta kubwa isiyo rasmi, ikiwa ni pamoja na kilimo. Hivyo hivyo, nchi nyingi za Afrika zinasifa ya upacha wa elimu na afya, zinazotofautishwa na uwepo wa taasisi ghali, za binafsi na zile za umma zoete zikiwa mijini, na sekta kubwa (shule za msingi na vituo vya afya) vikikosa wataalamu, vifaa duni, na kutokuwepo maeneo yote ya nchi. Kwa mukhtadha huu, shule zina wajibu wa hatari, kama ilivyokuwa (na bado ndivyo ilivyo) moja ya milango mikubwa ya kuingilia “si tu kwenye ajira katika sekta ya kisasa, lakini pia kwenda kwenye nafsi mbalimbali kwenye vyombo vya serikali na madaraka ya kisiasa, hali inayoakisi mageuzi ya jamii za bara la Ulaya”. Matokeo yake, ni kutokuwepo kwa fursa sawa za kupata nafasi ikimaanisha kuongezeka kwa kada ya juu ya kisiasa.

Hatua gani zichukuliwe kupunguza hali hii ya kutokuwepo kwa usawa?

Katika ngazi za chini kabisa, mara nyingi juhudi hazifanyiki kuelewa hali mahususi zinazosababisha kukua kwa hali hii ya kutokuwepo kwa usawa. Taasisi kadhaa zimekuwa zikitumia zana za kufuatilia hali za maisha ya watu walio katika hatari ili kufahamu sababu nyuma ya hali hizi.

Nchini Madagaska, CIRAD (kituo cha Ufaransa cha Utafiti kinachofanya kazi na nchi zinazoendelea katika kupambana na masuala ya kimataifa ya kilimo na maendeleo) kimependekeza kutengenezwa kwa chombo cha kuchunguza mwenendo wa mambo na kuimarisha hali za maisha ya watu katika maeneo ya vijijini [fr]:

Le Réseau des observatoires ruraux (ROR) constitue un dispositif de suivi et d’analyse des conditions de vie des ménages ruraux. Un des objectifs principaux est d’appréhender l’évolution de la situation des ménages ruraux et l’impact des mesures publiques et des chocs externes sur ces ménages. Chaque observatoire comporte un panel de 500 ménages sur des sites choisis de manière raisonnée avec le bailleur. Le questionnaire couvre les principaux aspects des la vie des ménages sur une période de 12 mois. Les résultats permettent une comparaison des situations dans le temps (par année) et dans l’espace (entre les observatoires).

Mtandao wa wachunguzi wa maeneo ya vijijini (ROR) unajumuisha zana ambazo zinafuatilia na kuchambua hali za maisha katika makazi ya vijijini. Moja wapo ya malengo makuu ni kupata uelewa wa mabadiliko ya hali ya maisha vijijini na athari zinazotokana na hatua za wananchi na matatizo ya nje kwenye hali za maisha. Kila chombo cha uchunguzi kimetengeneza na jopo la kaya 500 katika maeneo yaliyochaguliwa kwa makubaliano na wamiliki wa ardhi. Dodoso huuliza kuhusu maeneo muhimu ya maisha ya haya kwa kipindi cha miezi 12. Matokeo humaanisha kuwa tunaweza kufanya ulinganisho wa muda (kwa mwaka) na achano (kati ya uchunguzi mmoja hadi mwingine).

Kutokuwepo kwa usawa wa kimapendi nchini Burkina Faso umefahamika kuwa kizuizi kikubwa cha maendeleo, kama tafiti zinavyoonyesha kuwa ushiriki wa wanawake katika harakati za kimaisha nchini ambazo zina athari kubwa katika maendeleo ya nchi. Bougnan Naon anaeleza kile kinachofanywa na Umoja wa Dakupa [fr] katika suala hili kwenye Jimbo la Boulgou:

L'enjeu du projet est de permettre la création d'un réseau fonctionnel avec des membres compétents pour influencer les attitudes/pratiques traditionnelles, ainsi que les politiques et stratégies locales de lutte contre les inégalités de genre [..] (L'objectif est de): former 50 acteurs-clefs locaux aux stratégies de prise en compte du genre dans la mise en œuvre des projets et programmes par an, d'organiser des suivis-supervisions pour faciliter l'application effective de l'approche (maîtrise des outils et de l'identification d'actions genre pertinentes) par les ONG au profit de leurs cibles.

Lengo la mradi ni kuwezesha kutengenezwa kwa mtandao unaofanya kazi wenye wanachama wenye ujuzi ili kusababisha mabadiliko ya mitazamo na mienendo ya kimila, ikiwa ni pamoja na sera na mbinu za kupambana na kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia […] (Lengo ni) kutengeneza wataalam muhimu 50 wa ngazi za chini na kuwajengea uwezo wa mbinu za kuhakikisha jinsia inazingatiwa wakati wa kuanzisha miradi na program kila mwaka, na Asasi Zisizo za Kiserikali kufikia malengo yake kwa kuwahamasisha waratibu wake kuwezesha matumizi sahihi ya mbinu (kujifunza zana na kutambua maeneo ili kutambua hatua zinazotakikana za kijinsia).

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.