Habari Kuu kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Habari kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Je, Felix Tshisekedi Atamaliza Machafuko Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo?
President Felix Tshisekedi alisema kwamba hatua ya mahakama kuthibitisha ushindi wake ilikuwa ni ushindi kwa nchi yote na aliahidi kujenga taifa la umoja, amani na usalama.
Wakimbizi Nchini Marekani Wadumisha Tamaduni za Kimuziki kwa Nyimbo za Watoto
Msimuliaji wa hadidhi kwenye Kituo cha Makumbusho ya Sanaa cha Erie Art Museumkilicho kwenye jimbo la Pennsylvania, nchini Marekani alikuja na wazo: kuwasaidia wakimbizi kujifunza ujuzi wa kazi wakati akiwasaidia kukumbuka nyimbo zao.
Mfalme wa Rumba lenye Mahadhi ya ki-Kongo Afariki Dunia. Tunamkumbuka kwa Hili
Tumempoteza Papa Wemba, mwanzilishi wa rumba lenye mahadhi ya Kikongo na "mfalme wa Sape". "Kwaheri na asante sana kwa msanii huyu," tunasema sisi wa Global Voices
Watu 36 Wauawa, Mtandao wa Intaneti Wafungwa Kongo DRC Kufuatia Maandamano ya Kumpinga Rais Kabila
Ghasia na mapigano kati ya Polisi na waandamanaji wanaopinga hatua ya Kabila kurekebisha sheria ya uchaguzi vimesababisha kuuawa kwa watu 36 nchini Kongo DRC katika kipindi cha siku chache.
Mkutano wa Wanawake wa Nchi Zizungumzao Kifaransa 2014 Wafunguliwa Kinshasa, DRC
Mkutano wa wanawake wa nchi zizuingumzao Kifaransa 2014 [fr] Unafunguliwa leo jijini Kinshasa, DRC. Huu ni mkutano wa pili kufuatia ule uliofanyika Paris mwaka 2013. Wakati ule wa kwanza ulijikita katika kupunguza vitendo vya kudhalilisha wanawake katika maeneo yenye migogoro, lengo la mkutano huu wa 2014 litakuwa ni wajibu wa wanawake...
Je, Italia Iko Tayari kwa Waziri Aliyezaliwa Afrika?
“Je, Italia iko tayari kwa Waziri wa Serikalki aliyezaliwa Afrika?,” Donata Columbro anauliza: Miezi miwili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, Italia ina serikali mpya. Na Cécile Kyenge, mwenye umri wa miaka 48, daktari wa upasuaji macho na raia wa Italia aliyezaliwa Kongo, ni Waziri mpya wa Ushirikiano katika baraza la mawaziri la Waziri...
Jaribio la Mapinduzi katika Visiwa vya Comoro
Jeshi la Pilisi nchini Comoro limesema linawashikilia watu wanaosemekana kuwa wahaini raia wa Kongo na Chadi kwa tuhuma za jaribio la kuiangusha serikali lililofanyika mwisho wa wiki. Linfo.re anaongeza kwamba [fr]: Makamanda wa Jeshi hawakutaka kupambana waziwazi na wahaini hao. Waliamini kwamba ” Kujeruhi raia wa Comoro kwa lengo la...
DRC Kongo: Misuguano Kati ya Kinshasa na Paris Mkutano Unapoanza
Le Potentiel anaandika kwamba [fr] tathmini ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu nchini DRC Kongo iliyofanywa na Rais wa Ufaransa Hollande haikuchukuliwa kijuu juu na serikali ya Kongo wakati ambapo Mkutano wa nchi zizungumzazo Kifaransa ndio kwanza umeanza mjini Kinshasa, DRC. SErikali hizi mbili zinaonekana kutofautiana sana kuhusu mambo kama...
Mabadiliko ya Mfumo wa Ustawi wa Jamii ya Kiafrika
Utekelezaji wa mifumo ya hifadhi ya jamii ya taifa bado uko katika hatua za mabadiliko katika nchi nyingi za Afrika. Mafanikio ya mifumo iliyopo yanajadiliwa na wataalamu wa hifadhi za jamii katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Congo (DRC): Video zasaidia kumtia hatiani Thomas Lubanga kwa uhalifu wa kivita
Mnamo tarehe 14, Machi, mahakama ya kimataifa ya makosa ya kivita ilimtia hatiani Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa waasi Kongo (DRC) Mashariki, kwa kosa la kuwatumia watoto katika vita. Jaji alisema picha za video zilizoonyesha mahojiano na askari hao watoto ziliziongeza uzito wa ushahidi ulioisaidia mahakama kutoa hukumu.