Mapema tarehe 12 Agosti, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa taarifa chanya ya maendeleo ya michakato ya kitabibu ya majaribio ya dawa kadhaa za kutibu ugonjwa wa ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Jamhuri ya Congo).
WHO ilitanabaisha kuwa, dawa za ebola zilizojaribiwa zimeonesha “matokeo chanya yatakayoleta matumaini ya kuishi kwa wagonjwa wa Ebola,” na kuendelea kueleza kuwa “dawa mbili kati ya nne zilizojaribiwa zimeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu Ebola.”
Ni nani huyu anayehusika kwenye tiba hii ya Ebola? Mheshimiwa Profesa Jean-Jacques Muyembe-Tamfum, Mkurugenzi Mkuu wa Institut National de Recherche Biomédicale (INRB) DR ya Congo, aliwekeza sehemu kubwa ya Maisha yake katika kutafuta tiba ya kirusi cha Ebola.
Wakati vyombo vya ahabari vya kimataifa vikiwa vinaripoti kwa kiasi kikubwa kuhusu namna ugonjwa wa Ebola unavyosababisha idadi kubwa ya vifo nchini Congo, habari za kumhusu mwanasansi huyu zinazungumzwa kwa kiasi kidogo sana na vyombo hivi vya habari.
Muyembe-Tamfum alieleza : kuwa “hatutasema tena kuwa ugonjwa wa Ebola (EVD) hautibiki.”
Kutokana na kazi adhimu ya Muyembe-Tamfum, wanasayansi walifanya majaribio ya dawa nne za kutibu Ebola: ZMapp, remdesivir, mAb114 and REGN-EB3. Majibu ya majaribio ya kitabibu conducted kwa washiriki 499 wa utafiti yalionesha kuwa wagonjwa waliotibiwa kwa “REGN-EB3 au mAb114 walionesha kuwa na nafasi kubwa ya kupona” ukilinganisha na wale waliotibiwa kwa dawa nyingine mbili.
Utafiti huu uliofanyika chini ya uangalizi wa taasisi ya Institut National de Recherche Biomédicale (INRB), Wizara ya Afya ya Congo pamoja na mashirika mengine matatu yanayojihusisha na utoaji wa huduma za afya: Jumuia ya Kimataifa ya Masuala ya Afya (ALIMA), the International Medical Corps (IMC) na Médecins Sans Frontières (MSF).
Raia wa Congo aliyehusika kwenye upatikanaji wa tiba ya Ebola
Muyembe-Tamfum amekuwa akifanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa wa Ebola tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huu kwa mara ya kwanza nchini Congo ambapo mwaka 1976 alikuwa mtafiti wa kwanza kuzuru eneo ambalo ugonjwa wa Ebola uripotiwa kwa mara ya kwanza.
“Nilitumia miongo minne ya maisha yangu kutafuta tiba kwa aajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Kwa hiyo, haya ni mafanikio katika maisha yangu-Dr Jean-Jacques Muyembe, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Institut National de Recherche Biomedicale ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya #Congo pamoja na wenzake wamegundua tiba mpya ya ugonjwa wa Ebola inayoweza kutibu dalili za ugonjwa huu katika muda wa masaa matatu tu.
“Nilitumia miongo minne ya maisha yangu kutafuta tiba kwa aajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Kwa hiyo, haya ni mafanikio katika maisha yangu-Dr Jean-Jacques Muyembe, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Institut National de Recherche Biomedicale ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya #Congo pamoja na wenzake wamegundua tiba mpya ya ugonjwa wa Ebola inayoweza kutibu dalili za ugonjwa huu katika muda wa masaa matatu tu. ✊???
— Rosebell Kagumire ♉ (@RosebellK) August 13, 2019
Profesa wa maikrobaolojia wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Kinshasa- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hadi sasa ametumia muda wa takribani miaka 40 kutafuta tiba ya ugonjwa huu. Mwaka 1995, alifanya kazi na WHO kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa he worked with WHO in implementing utambuzi mbinu za kukabiliana na ugonjwa huu mara baada ya kuripotiwa kwa mara ya kwanza wagonjwa wa Ebola katika mji wa Kikwit, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kufuatia ugunduzi huu, waathirika wa Ebola kwa sasa wana nafasi kubwa ya kuwa na matumaini ya kupata huduma ya haraka na hivyo kufikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi wangalipo na uhai.
“Kwa kiwa asilimia 90 ya wagonjwa wataweza kufikishwa kwenye vituo vya afya na kupata matibabu na kurejea wakiwa wazima kabisa, watanza kuiamini dawa hii na kujenga imani kwa jamii zao na wananchi wote kwa ujumla.” — Jean-Jacque Muyembe-Tamfum
Sababu za tiba ya ugonjwa wa Ebola kupewa uzito
Wagonjwa wa kwanza wa Ebola waripotiwa mwaka 1976 karibu na mto Ebola huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa Kituo cha Kuzuia na Kupambana na Magonjwa (CDC), tangu wakati huo, kirusi cha Ebola kimekuwa “kikiibuka mara kwa mara kutoka kwenye chanzo asilia (ambacho hadi sasa hakijaweza kufahamika)” na kupelekea watu barani Afrika kuugua ugonjwa huu.
Kati ya mwaka 2014 na 2016 waliripotiwa zaidi ya watu 28,600 walioambukizwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa repoti ya WHO ya mwaka 2015:
- Mwaka 2014 Senegali ilikuwa na kisa kimoja cha maambukizi ya Ebola na bila ya kuripotiwa kifo chochote.
- Nigeria recorded 20 cases with 8 deaths. WHO ilitangaza kuwa hatua ya Nigeria ya kukabiliana na kirusi cha Ebola kama “sehemu ya ya kazi kubwa ya kukabiliana na ugonjwa hatari unaosambaa kwa haraka“.
- Mwezi Januari 2015, Mali iliripotiwa kuwa na wagonjwa 8 wa Ebola na vifo 6.
- Hata hivyo, hali ilikuwa mbaya sana kati ya mwezi Machi na Juni2016 katika nchi tatu: Nchini Sierra Leone: zaidi ya watu 14,000 waliugua ugonjwa wa Ebola pamoja na vifo 4,000; Liberia: takribani watu 10,000 waliugua Ebola na 3,000 kupoteza maisha. Guinea: wangonjwa 3,800 na vifo 2,500.
Maelezo ya jumla kuhusu ugonjwa wa Ebola Kimataifa
Ugonjwa wa Ebola ulioleta madhara makubwa katika nchi za Kiafrika ulizua taharuki na hofu mwaka 2015 pale wagonjwa wawili wa ebola waliporipotiwa kufariki nchini Marekani, mmoja Hispania na mwingine Ujerumani. Gaby‐Fleur Böl, mtafiti katika Taasisi ya Tathmini ya Majanga ya jijini Berlin, Germany, aliripoti taarifa nyingine za wagonjwa wa Ebola katika nchi za Hispania, Ujerumani, Uingereza, Italia na Switzerland. Kwa wakati huo, maambukizi ya Ebola yalichukuliwa kama hukumu ya kifo kutokana na ukosefu wa matibabu yenye tija.
Kama Böl alivyotangulia kusema, kasi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ebola na na pia /a> “wakati mwingine taarifa za upotoshaji kupitia vyombo vya habari” kuhusu Ebola zilichangia kuibua hofu duniani kote.
Taarifa kama hizi zilichangiwa pia na 2017 utafiti ambao walichambua Zaidi ya makala 109,000 zilizochapishwa kwenye vyombo vikubwa vya habari na blogu nchini Marekani kati ya mwezi Julai na Novemba 2014, kiini cha uchambuzi kikiwa ni habari zilizohusu ugojwa wa Ebola.
Waligundua nyakati kuu tatu kuhusu habari za ugonjwa wa Ebola katika vyombo vikubwa vya habari na blogu nchini Marekani “zilitokea Julai 27, Septemba 28, na Octoba 15 mwaka 2014″:
Tarehe 27 Julai, iliripotiwa kwa mara ya kwanza kuwa madaktari kutoka Marekani wanaohudumu nchini Liberia waliambukizwa ugonjwa wa Ebola. Tarehe 30 On Septemba, vyombo vya habari viliripoti kwa mapana kuhusu Thomas Duncan kuugua ugonjwa wa Ebola huko Texas na ikiwa ndio mara ya kwanza ugonjwa huo kuripotiwa nchini Marekani. Mwezi Oktoba tarehe 12, taarifa za mgonjwa wa Ebola ambaye ni ambaye ni mtoa huduma za afya zilisambamba kwa kina nchini Marekani. Baada ya tarehe 12 Oktoba,matuko mengine ya mlipo wa Ebola yaliripotiwa mfululizo hali iliyopelekea utipotiwaji wake kufifia siku hadi siku.
Kuna uwezekano kuwa vyombo vya habari vya nchini Marekani vimeripoti sana kuhusu ugonjwa wa Ebola kwa sababu ya matukio ya uwepo wa ugonjwa huu nchini humo. Pia, kutokana na urahisi wa upashanaji habari kutpia mitandao ya kijamii, ugonjwa wa Ebola umetokea kujadiliwa sana kwenye vyombo vya habari vya Ulaya na Marekani.
Hata hivyo, kinachosubiriwa ni kuona ikiwa taarifa za dawa ya kutibu ugonjwa wa Ebola iliyogunduliwa na Mwafrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayotibu gonjwa hili la “Kiafrika” itapewa nafasi kwenye vyombo vya habari kama ilivyokuwa mwaka 2017.